Mkakati mzuri kwa wakulima wanaozingatia ikolojia ni kujifunza na kuelewa sababu ya magonjwa, athari zake ili kuweza kukabiliana nayo. Hii inasaidia kulinda mazao ya mimea, kudumisha usalama wa uzalishaji wa chakula. Kwa kawaida, ni ngumu kuzuia ama kurekebisha tatizo ikiwa haujaelewa tatizo lenyewe. Ndio maana wakulima wanashauriwa kuwa makini shamba-ni kutambua kwa haraka uvamizi wa wadudu na pia magonjwa. Maana…
Kilimo
Ubunifu wa kilimo hai hushamirisha ujasiriamali
Hivi sasa nchini wakulima wanazalisha matunda na mbogamboga kwa wingi na katika maeneo mengi. Hii ni kwa sababu wanatambua jukumu lao katika kuongeza mapato yao ya kilimo na ustawi wa familia kama lengo la shughuli zao za kilimo. Hivyo ni muhimu wazalishaji kuhakikisha hawakosi mifumo mizuru kwa ajili ya mazao yao. Ni muhimu wakulima kuhakikisha kunakuwepo na mifumo mizuri ya…
Ushuhuda kutoka kwa msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu
Kama ilivyo ada, Mkulima Mbunifu tumeendelea kuwatembelea wakulima na wanufaika wa jarida hili kufahamu ni kwa namna gani elimu wanayoipata kupitia makala za kila mwezi zimeendelea kuleta chachu katika shughuli zao za kilimo na hata kuweza kuwabadilisha kimaisha. Bi. Esther Kitomari ni miongoni mwa wanufaika wa jarida la MkM na anaeleza kuwa amejifunza mengi kupitia makala zinazochapishwa kila mwezi hasa…
Umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji na mazingira
Utunzaji mahiri wa mazingira na vyanzo vya maji, maisha ya kila kiumbe hai yatakuwa hatarini. Hii ni kwa sababu mazingira salama ndiyo chanzo cha uhai kwa viumbe vyote. Ni dhahiri kuwa wote tunafahamu umuhimu wa maji katika kuendesha maisha ya wanadamu, wanyama na viumbe wengine. Ni ukweli usiopingika kuwa viumbe vyote vinategemea maji ili viweze kuishi. Viumbe hai hutegemeana na…
NANE NANE 2022, UNAKOSAJE MAONYESHO HAYA, MKULIMA MBUNIFU KAMA KAWAIDA YETU TUTAKUWEPO KUKUJUZA KUHUSU KILIMO NA UFUGAJI
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, nane nane hiyoo imekaribia. Nchini Tanzania, kila mwaka, wakulima na wafugaji hujumuika kwa pamoja kwa muda wa siku takribani kumi kuadhimisha sikukuu ya wakulima nchini. Sherehe hizi hufikia kilele siku ya tarehe nane mwezi wa nane. Katika kipindi hiki wadau mbalimbali wa kilimo, huandaa mazao na bidhaa mbalimbali za kilimo kwa ajili kushirikisha bunifu mbalimbali na…
Namna ya kusia mbegu kwenye trei
Kila baada ya kujaza udongo katika trei moja, weka punje za mbegu kwenye kila tundu la trei, na tumia kijiti chembamba kiasi kusukumiza mbegu kuzama kwenye udongo ndani ya tundu lakini mbegu isizame sana, wala isifike katikati ya tundu bali juu kiasi na iwe imefunikwa na udongo. Fanya hivyo kwa trei zote mpaka utakapomaliza kusia mbegu zako, tayari kwa ajili…
Madhara ya afya yaletwayo na matumizi ya viatilifu
Katika toleo lililopita la juni tulianza kuangazia madhara yasababishwayo na viatilifu na katika toleo hili tumalizia mada hii kwa kuangalia njia ambazo sumu huingia mwilini. Mara nyingi wakulima hutumia kemikali kwa matumizi tofaut, bila kufahamu kuwa wao pia wanaathiriwa na madawa hayo. Dawa hizo huingia mwilini kwa njia mbalimbali. Kwa sababu kuna aina nyingi za dawa, sumu inaweza kutofautiana sana.…
Maandalizi ya udongo kwa ajili ya kusia mbegu
Wakulima wengi hawaelewi ubora na umuhimu wa kuandaa udongo maalumu kwa ajili ya kusia mbegu za mazao mbalimbali kabla ya kuzipeleka shambani hasa mazao ya bustani. Si kila udongo unafaa kwa ajili ya kusia mbegu. Kuna udongo maalumu unaostahili kutumika kwa ajili ya kusia mbegu, ambao mkulima yeyote anaweza kuutafuta na kuandaa mwenyewe kwa ajili ya matumizi hayo. Bila kutumia…
Ijue thamani ya mti wa mlonge
Kila sehemu ya mti wa mlonge inathamani na faida nyingi, faida hizo zinaweza kuwa kwa binadamu, wanyama au mimea. Ni jambo jema kwa mkulima yeyote anayefanya au anayetaka kufanya kilimo hai kujifunza namna atakavyo weza kutumia mti wa mlonge na kunufaika na faida zinazotokana na mti huu. Mti wa mlonge unafaida nyingi ambazo hazifahamiki kwa watu wengi. Faida za mti…
Kemikali huingia mwilini kwa njia mbalimbali
Kwa muda mrefu wakulima walio wengi wamekuwa wakitumia madawa ya kemikali kwa matumizi tofauti, bila kufahamu kuwa wao pia wanaathiriwa na madawa hayo. Dawa hizo huingia mwilini kwa njia mbalimbali. Ni muhimu kwa mkulima kuelewa vyema jinsi ya kujikinga kutokana na madhara ya madawa ya kuangamiza wadudu, hii ni pamoja na kuacha matumizi ya madawa yenye madhara na namna nzuri…