- Kilimo
Sambaza chapisho hili

Zao la maharagwe ni moja kati ya mazao ya chakula na biashara linalolimwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa misimu tofauti kulingana na hali ya hewa ya eneo husika.

Kabla ya kuzalisha zao hili kwa misingi ya kilimo hai, mkulima hana budi kufahamu kanuni sahihi kwa ajili ya kufanya uzalishaji bora na wenye tija.

Kanuni za uzalishaji wa maharagwe

Kabla ya kuotesha zao la maharagwe, kuna baadhi ya kanuni ni muhimu kufuata ili kupata mazao bora;

Ukanda na hali ya hewa Hii inamaanisha kuwa maharagwe yanaweza kuzalishwa katika maeneo mengi nchini lakini kabla ya kuotesha zao hili ni vyema kufahamu hali ya eneo husika kama;

  • Joto: Maharage yanafanya vizuri katika ukanda wa kiasi cha nyuzi joto 12 hadi 32 sentigredi. Joto likiwa chini zaidi au juu zaidi linapunguza ukuaji.
  • Mvua: Kuwe na mvua kati ya 400mm hadi 1800mm kwa mwaka zinazonyesha kwa mtawanyiko mzuri.
  • Mwinuko: Maharage huzalisha vizuri kwenye mwinuko wa mita 400-2000 m kutoka usawa wa bahari.
  • Udongo: Usiwe wa kutuamisha maji na uwe na rutuba ya kutosha.

Mbegu
Chagua mbegu sahihi ili kupata mavuno bora. Chagua mbegu zenye soko, mavuno mengi, kinzani/uvumilivu wa magonjwa na wadudu na maeneo ya mvua chache zinazokomaa haraka. Mapendekezo ya mbegu yatategemea mbegu unazozifahamu kuwa na soko, uzaaji mzuri, na zinazostahimili ukame.

Mbegu bora zinaweza kupatikana kutoka kwa wakulima wanaozalisha mbegu.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *