- Kilimo

Udhibiti wa magonjwa na wadudu kwa kutumia dawa za asili

Sambaza chapisho hili

Hizi ni dawa zinazotokana na mimea ambayo hupatikana katika maeneo ya wakulima. Matumizi ya dawa hizi ni njia mojawapo ya kuepuka dawa za viwandani ambazo huathiri udongo, mazingira na afya za watu na wanyama.

Madawa yasipotengenezwa vizuri na kutumiwa ipasavyo yanaweza yasifanye kazi ipasavyo, hivyo huwa ni vigumu kuwashawishi wakulima kuzitumia.

Inashauriwa kutumia dawa hizi kama kinga kabla mashambulizi hayajashamiri kwani zinafanya kazi taratibu. Hivyo ni vizuri kuzitumia kama kinga kuliko tiba.

Sifa za dawa za asili

  • Upatikanaji wake uwe rahisi na isiwe na ushindani wa virutubisho na mazao.
  • Iwe rahisi kutengeneza na isiyohitaji maandalizi ya kiteknolojia na isichukue muda mrefu kutengeneza.
  • Matokeo yenye kuonekana. Mara nyingi, dawa hizi hufukuza wadudu zaidi kuliko kuua.

Unafuu wa gharama.

Dawa hizi hupatikana bure ila utayarishaji wa dawa hizi lazima upimwe. Kulingana na gharama zitakazojitokeza kulingana na mgongano wa mazingira yakilinganishwa na madawa yaliyokwisha tengenezwa la sivyo wakulima wataendelea kutumia sumu. Uwezo wa kuua wadudu walengwa tu bila kudhuru viumbe hai marafiki.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *