Mwaka umeanza ukiwa na baraka tele na habari njema kwa wakulima na wasomaji kwa ujumla. Kuanzia mwezi huu jarida lako ulipendalo la Mkulima Mbunifu (MkM) litakuwa likichapishwa na kuletwa kwako kila baada ya miezi miwili. Tangu jarida hili lilipozinduliwa mwezi Julai 2011, limekuwa likichapishwa na kusambazwa kwa wakulima kila baada ya miezi miwili. Hata hivyo sababu ilikua ni kujenga msingi…
Kilimo
Panda miti kupunguza madhara ya mabadiliko ya tabia nchi
Wakulima wanaweza kuchangia uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti na kutumia mbinu za kilimo hai. Kupanda miti ina manufaa nyingi ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira, kuwa chanzo cha malisho ya mifugo, asali, mbao, na hewa safi. Kipindi kirefu cha ukame ambacho kimeripotiwa katika kanda hii ya Afrika Mashariki imesababisha maeneo mengi kuwa kavu na hata ardhi kumomonyolewa na upepo…
Weka mipango thabiti kwa kuzalisha kibiashara
Kilimo kinachangia kwa kiasi kikubwa kutoa ajira, na mchango mkubwa katika kuondoa umasikini, hasa katika nchi zinazoendelea, nyingi zikiwa Barani Afrika. Hivi sasa kuna msukumo mkubwa kutoka kwa serikali na wadau mbalimbali wanaohimiza wakulima kuangali kilimo katika mtizamo wa kibiashara. Kwamba, wakulima wasizalishe tu kwa minajili ya chakula. Kuanzisha kilimo cha biashara ni tofauti na kulima tu kawaida, kupanda na…
Bustani ya nyumbani inaweza kukukwamua kiuchumi na kuboresha afya yafamilia
Bustani ya nyumbani, ni eneo dogo lililokaribu na nyumba linaloandaliwa na wanafamilia na kupandwa mazao mbalimbali ya mbogamboga kwaajili ya familia. Hata hivyo, katika maeneo mengi wanawake ndio wamekua wakijishughulisha na bustani ndogo za nyumbani. Mara nyingi bustani ya nyumbani hujumuisha uzalishaji wa mazao ya muda mfupi hasa mbogamboga kwani ni rahisi kuyahudumia kwa gharama nafuu lakini pia yanazalisha kwa…
Soko la mbogamboga hutokana na uzalishaji
Soko ni mahali au njia ambayo muuzaji na mnunuzi hukutana na kubadilishana mali au huduma. Ni fursa ya kuuza na kununua. Kwa kawaida tunapozungumzia soko, tunagusia mambo kadha wa kadha, ikiwa ni pamoja na ukubwa wake, yaani wingi wa wauzaji na wanunuzi katika soko husika, ushindani, washindani, bidhaa na bei zake, changamoto, pamoja na mabadiliko yanayotegemewa. Kwa upande mwingine, tunaweza…
Hakikisha unafahamu namna ya kupata mbegu bora kwa mavuno yenye tija
Hasara inayotokana na ununuzi wa mbegu isiyokuwa na ubora ni pamoja na upotevu wa pesa walizotumia kununua mbegu, kuandaa shamba, nguvu kazi iliyotumika kupanda pamoja na muda ambao ungeweza kutumika kwa mambo mengine ya maendeleo. Mbali na hayo, hali hiyo pia inaashiria hali ya hatari hapo baadaye ambayo inatokana na ukosefu wa mavuno ambayo yangetumika kwa ajili ya chakula pamoja…
Benki za mbegu za asili zinazosimamiwa na jamii
Sekta ya kilimo nchini inachangia takribani asilimia 26 ya pato la taifa na kuajiri asilimia 75 ya idadi ya watu huku ikisaidia kuongeza mapato na kuboresha maisha. Katika kuhakikisha wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji mbegu na mavuno mengi, serikali kupitia waziri wa kilimo, Hussein Bashe wakati akiwasilisha bajeti ya wizara mwaka 2022- 2023 bungeni alisema, mikakati yao ni kuwa na benki…
Umejipanga vipi kusheherekea maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani?
Unafahamu kuwa chakula kinatokana na mbegu bora? Bila mbegu hakuna chakula Chakula hakitokani na mbegu tu, Bali mbegu bora na salama, yaani Mbegu bora za asili Kama mkulima, Je, unatumia mbegu bora za asili katika uzalishaji wa mazao mbalimbali shambani mwako? Je, unahifadhi mbegu kwa ajili ya msimu ujao? Mbegu yangu, Chakula changu
SIKU YA CHAKULA DUNIANI
Mboga salama kwa afya bora
Mbinu za uhifadhi wa udongo wa kilimo na mimea
Udongo ni sehemu kubwa ya kilimo. Tunaweza kusema bila udongo hakuna kilimo lakini bila bila udongo wenye rutuba hakuna mavuno bora. Mara nyingi mvua, upepo na matumizi ya mbolea za viwandani, uharibifu wa mazingira kama kukata miti, wanyama n ahata shughuli zingine za kibinadamu ndiyo hupelekea kuharibika kwa udongo. Kuna njia nyingi za zinazotumia kilimo za kuhifadhi udongo na maji…