Mimi ni msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu (MkM) toka mwaka 2011, na nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza shughuli zangu za kilimo na ufugaji kwa ufanisi kutokana na elimu inayotolewa na jarida hili. Hayo ni maneno ya Bw. Silvester Gideon Mbulla (63), mkazi wa Kongwa (Hogoro), mkoani Dodoma, ambaye hakusita kuonyesha furaha yake mara tu alipokutana na mwandishi wa jarida…
Kilimo
Thamini na kuendeleza mbegu za asili ili kuleta tija katika kilimo
Mbegu ni pembejeo ya muhimu katika uzalishaji wa mazao. Upatikanaji wa mazao bora hutegemea matumizi ya aina na ubora wa mbegu za mazao husika. Baadhi ya wakulima nchini Tanzania wamesahau matumizi ya mbegu za asili na kujikita zaidi katika mbegu za kisasa. Mbegu ni nini? Mbegu ni sehemu ya mmea ambayo mmea mpya unaweza kuota. Kuna makundi makuu mawili ya…
Sindika mazao mbalimbali kwa ajili chakula na tiba lishe
Kupitia makala mbalimbali katika jarida la Mkulima Mbunifu, tumeweza kutoa elimu juu ya usindikaji wa mazao mbalimbali yatokanayo na wanyama na mimea. Hii ni kwa madhumuni ya kusaidia jamii kujifunza na kufanya kwa vitendo kisha kuongeza pato na kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno. Katika makala hii, tunafundisha namna ya kusindika baadhi ya mazao ambayo yatatumika kama chakula, hivyo…
Nyuzinyuzi ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu
Nyuzinyuzi hupatikana kirahisi kwa familia kwa wakulima. Hii ni pamoja na nafaka zisizokobolewa,njugu karanga, kunde, matunda na mboga. Ni chanzo muhimu cha chakula kwa bakteria chenye faida kwenye utumbo. Inaweza kusaidia kudhibiti uzito na kupunguza hatari kwa ugonjwa wa moyo. Nyuzinyuzi (Roughage) Roughage, pia inajulikana kama nyuzinyuzi, ni sehemu ya wanga ya mimea ambayo haiwezi kumeng’enywa na mwili wa binadamu.…
Udhibiti wa wadudu na magonjwa katika kilimo hai
Katika uzalishaji wa mazao kwa misingi ya kilimo hai ambacho ni aina ya kilimo kinachozingatia usalama wa chakula na kuondokana na matumizi ya kemikali za viwandani changamoto ya magonjwa na wadudu pia hutokea, jambo linalohitaji usimamizi mzuri ili kuleta uzalishaji wenye tija. Faida ya kuzalisha kwa misingi ya kilimo hai hasa katika kukabiliana na magonjwa na wadudu ni kuwa njia…
MKULIMA MBUNIFU INTERN ADVERT
S.L.P 14402, Arusha, Tanzania Simu :+255 (0) 0714 266 0007 Barua pepe: info@mkulimambunifu.org TERMS OF REFERENCE FOR MKULIMA MBUNIFU INTERN Mkulima Mbunifu is seeking to recruit suitably qualified intern to support MkM work in content development and distribution of MkM magazine. The intern will also support monitoring activities of the project, data management and feedback from users of knowledge products…
Fursa ya kibiashara kwa misingi ya Kilimo hai
‘’Mimi ni mkulima wa mfano, ninazalisha mazao mbalimbali kwa misingi ya kilimo hai na nimefaidika sana’’. Hayo ni maneno ya mkulima wa kilimo hai, Bw. Michael Laizer (73), toka Kijiji cha Emaoi, Ngaramtoni, mkoani Arusha ambaye anajishughulisha na uzalishaji wa mazao ya biashara kwa misingi ya kilimo hai. Bw. Laizer, ambaye jina la kibiashara linalotambulika kama nembo kwenye bidhaa zake…
Mkulima atumia kilimo hai kujiendeleza baada ya kustaafu
“Naitwa Felister Mangalu (64) mkulima wa kilimo hai. Nilikua mfanyakazi wa serikali na nikastaafu mwaka wa 2019. Kabla ya kustaafu nilikuwa nikijiuliza maswali kuhusu nini nitafanya ili kuendelea kujikimu kimaisha endapo muda wangu wa ajira ukiisha. Najua hili ni swali ambalo watu wengi hujiuliza wakiwa na sababu kama zangu. Hata hivyo, najua tumejaliwa vipawa mbalimbali na tuna uwezo tofauti tofauti.…
Soko la mazao ya kilimo hai Tanzania
Ingawa taasisi nyingi zinasisitiza kilimo hai nchini Tanzania, kuna walaji wachache sana walio na uelewa wa bidhaa za kilimo hai. Soko la mazao ya kilimo hai lipo tu na kufahamika katika miji mikubwa kama vile Dar es Salaam na Arusha, na mashirika machache yaliyoidhinishwa katika kuuza mazao kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya soko la ndani na hata…
Zingatia lishe sahihi na mifumo endelevu ya uzalishaji wa chakula salama
Tunapozungumzia lishe tunamaanisha kupata kiasi na ubora wa chakula na maji kwa vipindi vinavyofaa ili kuruhusu mwili kufanya kazi vizuri “balanced diet” yaani mlo kamili. Mahitaji ya lishe hutofautiana kulingana na jinsia, umri, shughuli za kila siku, ujauzito/kunyonyesha na hali ya afya ya mtu binafsi. Chakula kinapovunjwa, hutoa nishati ya kujenga mwili na kuupa kinga. Nishati hupimwa kwa kilokari au…