Suala la soko ni la msingi na ni la wakati wote, kuanzia kipindi cha utafutaji taarifa ya zao husika, wakati zao likiwa katika hatua ya awali ya uzalishaji na hata linapokuwa tayari kwenda sokoni. Ni muhimu kwa mkulima kutafuta soko la mazao yake ili aweze kuuza kwa bei iliyopo sokoni na ikiwa bei imeshuka kwa ghalfa bila kutarajiwa, aweze kufikiri…
Kilimo
Umuhimu wa udongo kwa uzalishaji wenye tija
Udongo wenye afya ni udongo ulio hai, ambao unazalisha mazao bora na yenye afya. Udongo lazima uwe na minyoo na viumbe vingine. Viumbe hawa hufanya kazi ya kulainisha udongo kwa kuvunjavunja masalia ya majani, mimea na mabua yaliyokufa kisha kubeba masalia hayo hadi chini ya udongo na kuichanganya kisha kuzalisha virutubishi vya kwenye mimea. Viumbe hawa huongeza kasi ya kuoza…
Kilimo bustani huongeza pato nyumbani
Kilimo cha bustani kinahusika na uzalishaji wa mazao ya aina ya mboga, matunda, viungo na mimea ya mapambo. Kilimo cha bustani ni chanzo cha ajira na pato kwa wakulima na watu wengine. Mboga na matunda vinatupatia virutubisho vya kujenga, kutia nguvu na kulinda mwili. Unapowaangalia wakulima utagundua wengi wamejikita katika uzalishaji wa mazao ya bustani, kwa lengo la kukidhi mahitaji…
Matokeo ya lishe duni kwa watoto na jinsi ya kuboresha afya
Kila mwaka, watoto wengi chini ya miaka 5 nchini Tanzania hufa kwa sababu ya lishe duni na chakula. Watoto hawa hawapati chakula chenye vitamini, madini ya iodini na chuma ambayo yanahitajika kwa afya na ukuaji mzuri. Hali hii inasababisha utapiamlo. Watoto wenye umri wa miezi 6 na zaidi, wapewe chakula cha ziada tofauti-tofauti kwa viwango vidogo mwanzoni na kuongeza kadri…
Umakini wa uzalishaji huzuia upotevu wa chakula
Upotevu wa chakula hutokea katika mnyororo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji. Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi. Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla ya chakula kumfikia mlaji. Kwani chakula kinachofaa…
Ijue Mbinu ya Kilimo Ikolojia Fanya Juu Fanya Chini
Fanya Juu ni kingamaji ambalo linachimbwa upande wa chini wa shamba, udongo uliochimbwa unawekwa upande wa juu wa shamba ili kutengeneza tuta ambalo litasaidia kubakiza maji ya mvua shambani na kuongeza upatikanaji wa maji kwa mimea. Mwishoni inasaidia kuijanisha ardhi yako! HATUA 1: Angalia Baini uelekeo wa mtiririko wa maji katika shamba lako kwa kuangalia au kwa kutumia vipimo. •…
DAWA YA ASILI YA MWAROBAINI
Mohd Rafii anauliza: Waungwana nisaidieni, Matumizi ya mwarobaini kwa kuulia wadudu katika mimea niuchemshe au niusage tu na kuuloweka? Mwarobaini ni mti unaostahimili ukame, unatoa kivuli na pia umeonekana kuwa na manufaa makubwa kama tiba kwa binadamu na mafuta yake hutengeneza sabuni. • Kati ya dawa zote za asili, mwarobaini umeth ibitika kufanya vizuri zaidi kutokana na uwezo wake…
Zao la maharagwe ni moja kati ya mazao ya chakula na biashara linalolimwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa misimu tofauti kulingana na hali ya hewa ya eneo husika. Kabla ya kuzalisha zao hili kwa misingi ya kilimo hai, mkulima hana budi kufahamu kanuni sahihi kwa ajili ya kufanya uzalishaji bora na wenye tija. Kanuni za uzalishaji wa maharagwe Kabla…
Namna ya kutengeneza busta
Busta za asili ni nyongeza ya virutubisho kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa mmea ili kua na uzalishaji mzuri hususani pale ambapo mimea imeanza kuzorota kutokana na kupungua/kukosekana kwa virutubisho vya kutosha kwenye udongo, busta hizi zina sifa ya kuupa mmea virutubisho kwa haraka sana na kuleta matokeo mazuri kwenye mimea ndani ya muda mfupi(siku 3). Aina za busta Busta…
Mbolea za asili
Kuna mbolea nyingi za asili ambazo zinaweza kutumika shambani kama vile samadi, mboji, chai ya mmea na bioslari. Namna ya kutayarisha mboji/mbolea vunde Mboji ni sehemu ya viumbe (mabaki ya mimea na wanyama) ambayo imeozeshwa kwa muda mrefu na kusazwa na viumbe wadogowadogo. Sehemu za vitu kama majani, matunda na mabaki ya shambani na ya jikoni hutengeneza mbolea ya mboji.…