Kabla ya kuzalisha uyoga inabidi kuwa na chumba chenye paa ambalo litazuia jua, mvua na vumbi. Chumba hiki kinatakiwa kiwe na sakafu inayohifadhi unyevunyevu pamoja na sehemu ya giza ambayo ni muhimu kwa kuotesha utando wa Uyoga. Mkulima wa kawaida anaweza kutumia kasha kama sehemu ya giza. Hatua muhimu katika kuotesha Uyoga Mkulima anatakiwa kwanza kutafuta mbegu, na baada ya…
Binadamu
Kula chakula bora chenye kukupatia afya
Mwongozo uliotolewa na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO unasema japo lishe hutofautiana sana kutokana na mahali na kulingana na upatikanaji wa chakula, tabia za kula na tamaduni, lakini linapokuja suala la chakula, kuna mengi ambayo tunajua juu ya nini na nini sio nzuri kwetu na hii ni kweli bila kujali tunaishi wapi. Mabadiliko ya kijamii,…
Lishe bora husaidia ukuaji wa mtoto hivyo ni muhimu kuzingatia
Kila familia na jamii inapaswa kufahamu nini huhusu lishe hii ni kwasababu karibu nusu ya vifo vya watoto wa umri wa chini ya miaka mitano kila mwaka hutokana na ukosefu wa lishe bora na ya kutosha, unaosababisha kudhoofika kwa kinga mwili na kushindwa kupambana na magonjwa. Endapo mama hakupata lishe ya kutosha wakati wa ujauzito au mtoto wake hakupata lishe…
HERI YA MWAKA MPYA WA 2022
Heri ya mwaka mpya 2022 Ni matumaini yetu kuwa sote tumevuka salama na tumejiandaa vyema katika kuukabili tena mwaka huu kwa kishindo katika kilimo na ufugaji ili kuongeza tija na kukuza uchumi lakini pia tukizalisha kwa misingi ya kilimo hai kwa ajili ya kulinda afya zetu, wanyama, mazingira na mimea. Ni hakika, mwaka uliopita haukuwa mbaya sana kwani pamoja na…
Uzalishaji wa mafuta ya karanga
Karanga hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali au kukaangwa ili kutumika kama vitafunwa lakini pia kusindikwa ili kupata mafuta, siagi na rojo. Karanga zina virutubisho vingi kama vile; maji asilimia 7, nguvu kilokari 570, protini gramu 23, mafuta gramu 45, wanga gramu 20, kalishamu miligramu 49, chuma miligramu 3.8, patasiamu miligramu 680, vitamini B miligramu 15.5 na vitamini A (I.U…
Utengenezaji wa jibini ngumu
Hii ni jibini aina ya cheddar ambayo asili yake ni huko Uingereza lakini kwasasa hutengenezwa katika nchi mbalimbali dunian. Hatua za utengenezaji Pima ubora wa maziwa Pasha moto maziwa kufikia nyuzi joto 65C yaache katika joto kwa dakika 30 au nyuzi joto 71.5C kwa sekunde 15 Poza maziwa kufikia nyuzi joto 22 hadi 25C Weka kimea cha mtindi (mesophilic) asilimia…
Uzalishaji wa malisho
Bonyeza hapa na sikiliza kuhusu malisho aina ya matete na faida zake
Mimi nasoma Jarida la Mkulima Mbunifu, wewe Je?
Hebu tazama tabasamu la mama huyu usoni, mara tu aonapo jarida la Mkulima Mbunifu na azidi pale anapokutana na taarifa muhimu kwake? Ni furaha iliyoje? Hebu na wewe kuwa mmojawapo wa wanufaika wa jarida hili, nakuahidi hutajutia….. Jarida pekee lililosheheni taarifa za kilimo hai, ufugaji wa mifugo aina mbalimbali, utunzaji wa udongo, mazingira na afya ya mwadamau kwa ujumla…… Mkulima…
TUNAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KUTUMA JARIDA LA OKTOBA
Habari ndugu msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu. Ni matumaini yetu kuwa uko salama na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Tunaomba radhi kwa kuchelewa kukutumia nakala yako ya jarida la Mkulima Mbunifu. Hii ni kutokana na kuwepo kwa changamoto kidogo zilizokuwa nje ya uwezo wetu ambazo zimepelekea kusindwa kuchapisha nakala ya mwezi Oktoba kwa wakati. Jarida hili…