Mwaka umeanza ukiwa na baraka tele na habari njema kwa wakulima na wasomaji kwa ujumla. Kuanzia mwezi huu jarida lako ulipendalo la Mkulima Mbunifu (MkM) litakuwa likichapishwa na kuletwa kwako kila baada ya miezi miwili. Tangu jarida hili lilipozinduliwa mwezi Julai 2011, limekuwa likichapishwa na kusambazwa kwa wakulima kila baada ya miezi miwili. Hata hivyo sababu ilikua ni kujenga msingi…
Binadamu
Bustani ya nyumbani inaweza kukukwamua kiuchumi na kuboresha afya yafamilia
Bustani ya nyumbani, ni eneo dogo lililokaribu na nyumba linaloandaliwa na wanafamilia na kupandwa mazao mbalimbali ya mbogamboga kwaajili ya familia. Hata hivyo, katika maeneo mengi wanawake ndio wamekua wakijishughulisha na bustani ndogo za nyumbani. Mara nyingi bustani ya nyumbani hujumuisha uzalishaji wa mazao ya muda mfupi hasa mbogamboga kwani ni rahisi kuyahudumia kwa gharama nafuu lakini pia yanazalisha kwa…
Athari za upungufu wa vitamini A
Kushindwa kuona vizuri hasa kunapokuwa na giza au mwanga hafifu. Ngozi kukauka au kupauka na wakati mwingine kuwa na vidonda huku nywele zikikosa afya. Kupata maambukizi ya magonjwa mara kwa mara hasa katika mfumo wa njia ya hewa na mfumo wa mkojo. Watoto wadogo kuugua surua kwa urahisi. Kudumaa kwa watoto kutokana na kukoma kukua na kuongezeka uzito. Ukuaji wa…
Kula matunda kwa wingi ili kuboresha afya yako
Tunda ni sehemu ya mmea ilio na mbegu au isio na mbegu ndani yake. Tunda ni sehemu ya chakula ambacho hujumuishwa katika lishe ya kila siku. Matunda mbalimbali huwa na virutubisho tofauti vinavyohitajika mwilini. Ulaji wa matunda unategemea na na jinsi mtu anavyopenda, kwa mfano, unaweza kula tunda lenyewe kama lilivyo ama kuchanganya na matunda mengine na hii huitwa saladi…
SALAMU ZA SIKUKUU ZA CHRISTMASS NA MWAKA MPYA WA 2023
Tunawatakia heri na baraka msimu huu wa kusherehekea sikukuu za Christmas na mwaka mpya wa 2023
SIKU YA CHAKULA DUNIANI? Unaelewa nini kuhusu ulaji wa mbogamboga kiafya
Je, unakula mbogamboga katika mlo wako wa kila siku? Je, unafahamu kuwa nusu ya sahani yako ya chakula cha kila siku kinatakiwa kiwe kimesheheni mbogamboga za kila aina?
SIKU YA CHAKULA DUNIANI
Mboga salama kwa afya bora
Jifunze kutengeneza keki ya asili ya ndizi na kuongeza pato
Ndizi ni zao la chakula maarufu sana katika mikoa mbalimbali hapa nchini kama vile Kilimanjaro, Arusha, Bukoba na sehemu zingine. Mbali na chakula zao hili pia limepata umaarufu sana katika ulaji kama matunda lakini pia uzalishaji wa kaukau (crips) pamoja na unga. Aidha matumizi ya zao hii yamezidi kuongezeka na hhata sasa kuweza kutumika kutengeneza keki. Keki ya ndizi Hii…
Afya ya mwili hutengenezwa na ulaji wa chakula unaofaa wa kila siku
Chakula kinachofaa tunamaanisha ulaji unaofaa ambao ni ulaji wa chakula mchanganyiko, cha kutosha na chenye virutubisho vyote kwa uwiano unaotakiwa. Ulaji unaofaa ni lazima uzingatie matumizi ya mafuta kwa kiasi kidogo sana. Mafuta ya nyama sio mazuri kwani yanahusishwa na magonjwa ya moyo, badala yake inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea kama vile alizeti. Matumizi ya sukari na chumvi…
Athari za kuzidi kwa matumizi ya vitamini A mwilini
Vitamini A ni mchanganyiko wa vyakula tofauti pamoja na baadhi ya matunda. Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza kila mmoja katika familia ale matunda na mboga za kutosha ilikupata vitamin A ya kutosha katika mlo wake kila siku, ilikuongeza kinga ya mwili, kuongeza uwezo wakufikiri na kupunguza hatari ya magonjwa. Ni kwa namna gani Vitamini A inatufanya tuwe na afya iliyobora?…





