Kudondoka kwa maua kwenye miembe yako inaweza kutokana na upungufu au ukosefu wa aina fulani ya madini. Virutubisho na madini kwenye miembe vinahitaji ufahamu na uelewa wa hali ya juu kwa kile kinachohitajika. Tofauti na hilo, unahitaji kuzingatia kiasi cha fosiforasi ili kuchochea uwezo wa mizizi na ukuaji wa mmea. Mkulima anatakiwa kuweka utaratibu wa kuweka mbolea kwenye mimea yake…
mbolea
Faida na matumizi ya mbolea ya kijani
Mazao ya mbolea ya kijani ni mazao ambayo yanapandwa ili kuongeza rutuba kwenye udongo. Mazao ya mbolea ya kijani ya jamii ya mikunde (ambazo ni zile zinatengeneza mbolea ya naitrojeni kutoka kwenye naitrojeni iliyopo kwenye hewa) zinaweza kuwapa wakulima wadogo faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na: Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni kwa ajili ya udongo, Zinaongeza tani nyingi za…
Kitunguu saumu kama dawa ya asili
Kitunguu saumu pia kinaweza kuwa mbadala wa kudhibiti viwavi, nzi wa matunda, utitiri mwekundu, utitiri mweupe, wadudu wenye magamba laini, kombamwiko wa madoa, magonjwa ya fangasi na minyoo fundo. Menya kilo mbili za kitunguu saumu na uzitwange vizuri (tumia blenda ni vizuri zaidi). Ongeza mililita 500 za maji ili kusaidia kukamua juisi/ mchanganyiko. Tumia chujio kupata mchanganyiko wa kitunguu saumu.…
Tumia mbolea ya asili kukuzia mimea
Kuna faida nyingi zinazotokana na matumizi ya mbolea za asili kama mboji na nyinginezo. Mbolea asili hutokana na kuoza kwa vitu vyenye uhai kama vile majani, miti na mabaki ya vyakula. Vitu hivi vinapooza hugeuka na kutengeneza virutubisho ambavyo husaidia kurutubisha udongo na kupunguza gharama kwa mkulima kwa kuwa vitu vinavvyotumika ni vya asili. Mbolea ya kukuzia mimea inatokana na…
Vyanzo vya virutubisho
Ni vyema kujenga uelewa wa vyanzo vya virutubisho vinavyoweza kutumika katika kilimo hai. Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo. Kuna mwingiliano kati ya uzalishaji wa mimea na mifugo na unachangia katika kurutubisha udongo. Mabaki ya mazao hulisha wanyama na samadi ya wanyama hurutubisha udongo. Pia, mifugo hao, kama madume, wanaweza…
Tengeneza mbolea ya chai ya alizeti pori (Tithonia diversifolia)
Alizeti pori maarufu kisayansi tithionia diversifolia ni aina ya mmea unaomea karibu kila mahali kando ya barabara na hata kwenye kingo za mito katika ardhi isiyokuwa na rutuba au hata katika maeneo ya bustani. Mmea huu ni mrefu na una mashina mengi kuanbzia sehemu ya chini hadi sehemu kunakotoa maua. Kwenye udongo wenye rutuba, mmea huu huweza kufikia urefu wa…
Mazao ya mbolea ya kijani ni mazao ambayo yanapandwa ili kuongeza rutuba kwenye udongo
Mazao ya mbolea ya kijani ya jamii ya mikunde (ambazo ni zile zinatengeneza mbolea ya naitrojeni kutoka kwenye naitrojeni iliyopo kwenye hewa) zinaweza kuwapa wakulima wadogo faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na: Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni kwa ajili ya udongo. Zinaongeza tani nyingi za viumbe hai kwenye udongo, hivyo basi, kuongeza udongo wenye rutuba, uwezo wa kutunza maji,…
Namna ya kutengeneza busta
Busta za asili ni nyongeza ya virutubisho kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa mmea ili kua na uzalishaji mzuri hususani pale ambapo mimea imeanza kuzorota kutokana na kupungua/kukosekana kwa virutubisho vya kutosha kwenye udongo, busta hizi zina sifa ya kuupa mmea virutubisho kwa haraka sana na kuleta matokeo mazuri kwenye mimea ndani ya muda mfupi(siku 3). Aina za busta Busta…
Matumizi mbalimbali ya mlonge
Kusafisha maji I. Kusanya mbegu za mlonge zilizokomaa kisha zimenye kupata kiini II. Twanga kiini mpaka upate unga III. Weka gramu 2 (vijiko viwili vya chai) za unga wa mlonge kwenye maji kiasi (nusu lita) natikisa kwa muda ilikupata mchanganyiko mzuri IV. Changanya kwenye maji lita 20 na koroga sana kwa muda wa dakika 10-15 V. Yaache maji yatulie kwa…
Ijue thamani ya mti wa mlonge
Kila sehemu ya mti wa mlonge inathamani na faida nyingi, faida hizo zinaweza kuwa kwa binadamu, wanyama au mimea. Ni jambo jema kwa mkulima yeyote anayefanya au anayetaka kufanya kilimo hai kujifunza namna atakavyo weza kutumia mti wa mlonge na kunufaika na faida zinazotokana na mti huu. Mti wa mlonge unafaida nyingi ambazo hazifahamiki kwa watu wengi. Faida za mti…







