chakula

- Kilimo

Ni muhimu kuzingatia soko la mazao kabla ya uzalishaji

Suala la soko ni la msingi na ni la wakati wote, kuanzia kipindi cha utafutaji taarifa ya zao husika, wakati zao likiwa katika hatua ya awali ya uzalishaji na hata linapokuwa tayari kwenda sokoni. Ni muhimu kwa mkulima kutafuta soko la mazao yake ili aweze kuuza kwa bei iliyopo sokoni na ikiwa bei imeshuka kwa ghalfa bila kutarajiwa, aweze kufikiri…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara

Kilimo bustani huongeza pato nyumbani

Kilimo cha bustani kinahusika na uzalishaji wa mazao ya aina ya mboga, matunda, viungo na mimea ya mapambo. Kilimo cha bustani ni chanzo cha ajira na pato kwa wakulima na watu wengine. Mboga na matunda vinatupatia virutubisho vya kujenga, kutia nguvu na kulinda mwili. Unapowaangalia wakulima utagundua wengi wamejikita katika uzalishaji wa mazao ya bustani, kwa lengo la kukidhi mahitaji…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo

Matokeo ya lishe duni kwa watoto na jinsi ya kuboresha afya

Kila mwaka, watoto wengi chini ya miaka 5 nchini Tanzania hufa kwa sababu ya lishe duni na chakula. Watoto hawa hawapati chakula chenye vitamini, madini ya iodini na chuma ambayo yanahitajika kwa afya na ukuaji mzuri. Hali hii inasababisha utapiamlo. Watoto wenye umri wa miezi 6 na zaidi, wapewe chakula cha ziada tofauti-tofauti kwa viwango vidogo mwanzoni na kuongeza kadri…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo

Umakini wa uzalishaji huzuia upotevu wa chakula

Upotevu wa chakula hutokea katika mnyororo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji. Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi. Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla ya chakula kumfikia mlaji. Kwani chakula kinachofaa…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo Biashara

MKULIMA MBUNIFU INAKUTAKIA HERI YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI: Hakuna wa kuachwa nyuma; uzalishaji bora, lishe bora, mazingira bora, maisha bora

Ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya chakula duniani, ni muhimu kwa kila jamii kuangalia namna ya kuondokana na baa la njaa linaloikabili ulimwengu kwasasa. Kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni; Hakuna wa kuachwa nyuma: uzalishaji bora, lishe bora, mazingira bora, maisha bora inahamasisha jamii kuhakikisha inafanya uzalishaji wenye kupelekea kuwepo kwa lishe bora, mazingira na maishaya mwanadamu kwa ujumla.…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo Biashara

Kupambana na mfumko wa bei ya vyakula

Wakati jarida hili lilipozinduliwa mwaka wa 2011, moja ya mambo yaliyowakera wasinduzi na ambalo linaendelea kusumbua jamii ni mfumko wa bei ya vyakula. Jambo hili linawatatiza wakulima na walaji au watumiaji wa mazao ya kilimo. ˮ Kuna sababu mseto zinazochangia kupanda na wakati mwingi kutotabirika kwa bei ya vyakula, na ambavyo lazima nchi kwa jumla ipambambane kudhibiti. Nishati Bei ya…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo

Zingatia lishe sahihi na mifumo endelevu ya uzalishaji wa chakula salama

Tunapozungumzia lishe tunamaanisha kupata kiasi na ubora wa chakula na maji kwa vipindi vinavyofaa ili kuruhusu mwili kufanya kazi vizuri “balanced diet” yaani mlo kamili. Mahitaji ya lishe hutofautiana kulingana na jinsia, umri, shughuli za kila siku, ujauzito/kunyonyesha na hali ya afya ya mtu binafsi. Chakula kinapovunjwa, hutoa nishati ya kujenga mwili na kuupa kinga. Nishati hupimwa kwa kilokari au…

Soma Zaidi

- Binadamu

Afya ya mwili hutengenezwa na ulaji wa chakula unaofaa wa kila siku

Chakula kinachofaa tunamaanisha ulaji unaofaa ambao ni ulaji wa chakula mchanganyiko, cha kutosha na chenye virutubisho vyote kwa uwiano unaotakiwa. Ulaji unaofaa ni lazima uzingatie matumizi ya mafuta kwa kiasi kidogo sana. Mafuta ya nyama sio mazuri kwani yanahusishwa na magonjwa ya moyo, badala yake inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea kama vile alizeti. Matumizi ya sukari na chumvi…

Soma Zaidi

- Mifugo

Tambua kwanini chakula cha kuku kinaharibika

Kila nikihifadhi chakula cha kuku baada ya muda fulani nakuta kimeanza kupata ukungu na wakati mwingine kuwa na harufu kali sana kama ya kuchacha, naombeni msaada wenu. 0654 624229 Dodoma Chakula cha kuku kinapozalishwa katika hali nzuri na kwa kufuata kanuni sahihi huweza kuhifadhiwa na kutumika kulishia kwa muda mrefu sana bila kuharibika. Tatizo ambalo mara nyingi huwakuta wafugaji walio…

Soma Zaidi