- Kilimo, Mifugo

Anzisha miradi tofauti kuongeza pato lako

Sambaza chapisho hili

Kuna msemo mmoja maarufu sana wa Kiswahili usemao, kidole kimoja hakivunji chawa. Hii inamaanisha kuwa endapo unategemea jambo moja tu, inakuwa ni vigumu sana kutimiza malengo yako au kufanikiwa kufanya jambo fulani.

Hii ni changamoto kwako mkulima kuhakikisha kuwa unatumia nafasi uliyo nayo ipasavyo. Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unaanzisha miradi ya aina mbalimbali kulinganga na uwezo wako. Hiyo itakuwezesha kuwa na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo, na endapo itatokea mradi mmoja ukaanguka basi hautadhurika sana kwa kuwa aina nyingine ya miradi utakayokuwa nayo itawezesha maisha kusonga mbele.

Kwa mfano, unaweza ukawa na mradi wa ufugaji kuku, mbuzi wa maziwa, ng’ombe wa maziwa, nyuki, bustani za mbogamboga na aina nyinginezo kadha wa kadha za uzalishaji kulingana na eneo lako.

Katika miradi hiyo, kuna mingine ambayo gharama zake za uzalishaji ni ndogo lakini ina faida kubwa, mfano ufugaji wa nyuki, jambo ambalo linasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua  miradi mingine ambayo kwa kiasi fulani gharama zake ni kubwa.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *