Mimea

- Kilimo, Mimea

Mapapai bora hupelekea soko lenye tija

Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamin A na madini ya kalsiamu kwa wingi na zao hili hulimwa karibu kila mahali hapa nchini kwa wastani wa tani 2,582 kwa mwaka. Ili kuweza kuzalisha zao la papai kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa ni muhimu kuhakikisha unazingatia kanuni zote za kilimo bora za uzalishaji wa mapapai. Ubora…

Soma Zaidi

- Mimea

Nimepiga hatua kwa kulima Canavalia

“Nilikuwa naotesha ekari tatu za mahindi na maharage lakini niliishia kuvuna chini ya gunia 10 za mahindi lakini pia nikipata maharage kidogo sana”. Hivyo ndivyo alivyoanza kueleza Bi. Edvester O. Yambazi (68), mkazi wa Sanya Juu ambaye kwasasa ameamua kufanya kilimo cha mahindi huku akiotesha zao funikizi aina ya Canavalia. Safari ya kilimo Bi. Yambazi anaeleza kuwa, aliteseka kwa muda…

Soma Zaidi

- Mimea

Namna bora ya kuvuna na kusindika mbaazi

Nimelima zao la mbaazi kwa muda mrefu sana, na miaka yote nimekuwa nikipata faida, mpaka hivi karibuni bei ya zao hili ilipoanguka na tukapata hasara. Je ni namna gani naweza kuhifadhi zao hili au kusindika? Msomaji MkM-Arusha. Mbaazi ni kati ya mazao jamii ya mikunde ambayo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mtwara, Dodoma, Lindi, Pwani, Morogoro, Arusha, Manyara, Tanga…

Soma Zaidi

- Binadamu, Mazingira, Mimea

Rutuba ya udongo ndio uhai wa udongo na tija kwa mkulima

Ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha anauilisha udongo kwa kutumia virutubisho vya asili, ili kuweza kuwa na rutuba na kuzalisha mazao yenye tija. Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu. Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho. Vipengele…

Soma Zaidi

- Binadamu, Mimea

Tumia mazao funikizi kwa chakula na kulisha mifugo

Mazao funikizi siyo mageni sana kwa wakulima walio wengi isipokuwa kwa wale ambao ndio kwanza wanaanza kujiingiza katika kilimo hifadhi. Si mazao yote funikizi yanayoweza kutumika kulishia mifugo moja kwa moja mara baada ya kuvuna kutoka shambani. Mengine ni lazima yafanyiwe maandalizi fulani ndipo yatumike kulishia. Mazao funikizi kama vile, canavalia yanahitajika kukaushwa kwanza na kuandaliwa vyema kabla ya kulisha…

Soma Zaidi

- Binadamu, Mimea

Mbolea ya asili inayotokana na magugu maji

Hii ni aina ya mbolea ya asili isiyokuwa na madhara yoyote kwa binadamu na wanyama. Mbolea hii hutengenezwa kwa kuvundika mimea ya baharini au maotea ya majini. Aina hii ya mbolea inafaa kutumika kwa kuchanganya na viua wadudu vyovyote ambavyo ni asidi au basic kwani utendaji kazi wake hauwezi kupote endapo itachanganywa. Viambata vya mbolea Mbolea hii ina vichocheo vya…

Soma Zaidi