Mkulima anaezalisha kwa mazao kwa kufuata misingi ya kilimo hai, Bw. Zadock Kitomari alisema kuwa, unapoanza kujishughulisha na kilimo hai ambacho hakitumii kemikali unaona kuwa uzalishaji unakuwa mdogo lakini kwa kadri unavyoendelea uzalishaji unakuwa mkubwa. Anaeleza kuwa, kilimo hai ni aina ya kilimo kinachoangalia uhai wa mazingira, uhakika na usalama wa mlaji na usalama wa chakula jambo ambalo linamuhakikishia mkulima…
Mimea
Vijana wanaweza kujifunza mengi kutokana na ubunifu kwenye kilimo hai
Kilimo hai kinafanyika kwa ufanisi na manufaa endapo wakulima wenyewe wanafanya ubunifu kulingana na mazingira yao. Ili kilimo hai kiwe endelevu ni muhimu ubunifu kutoka kwa vijana kutiliwa mkazo. Kilimo kwa kutumia mifuko (viroba) Kilimo cha kutumia mifuko (viroba), ni kilimo kizuri na chenye manufaa kwa wakulima, kwani unaweza kulima sehemu yeyote pasipo kuathiri mazingira. Watu wengi wanakijua kilimo hiki…
Tushirikiane kupata soko la mazao ya kilimo hai
Kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, ni wazi kuwa shughuli za kilimo hai zimeshika kasi, huku kukiwa na ongezeko la wazalishaji wa bidhaa za kilimo hai. Hili ni jambo jema sana kwa kuwa waswahili wanasema taratibu ndiyo mwendo, na kidogo kidogo hujaza kibaba. Na hapa taratibu tunaona mwanga wa dunia kurudi katika hali yake ya uasili, ya awali…
Usindikaji wa ndizi ili kuongeza kipato
Zao la migomba lina asili ya Philipino. Shina la mgomba limeundwa na vikonyo vya majani 12 hadi 30, kila kimoja kikiwa na urefu wa mita 7.6. Vikonyo hivyo pamoja na majani ya migomba hutumika kutengenezea nyuzi. Pamoja na nyuzi, zao kuu linalotokana na migomba ni ndizi, ambazo pamoja na kuwa ni chakula cha binadamu, lakini pia hutumika kwa njia nyinginezo…
Gliricidia: Mti wenye faida lukuki kwa mkulima
Gliricidia ni mti ambao kisayansi hujulikana kwa jina la gliricidia sepium ambao hutumika kwa ajili ya mbolea au kurutubisha ardhi. Mti huu wa gliricidia ni jamii ya miti ya malisho ambayo majani yake hutumika kurutubisha udongo na kulishia mifugo hasa katika kipindi cha ukame. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kumudu kuzalisha wakati wa kiangazi pamoja na kudumisha hali…
Samadi ya wanyama na mimea
Ubora wa samadi ya wanyama hutegemea zaidi kile kilicholiwa na mnyama. Ikiwa wamelishwa chakula duni au nyasi zilizomea katika udongo usio na rutuba, basi samadi yao pia itakuwa na ubora duni. Ikiwa wanyama wamelishwa chakula kizuri basi samadi pia itakuwa bora na iliyojaa virutubisho. Samadi iliyo tayari kwa matumizi Samadi huhitaji kupevuka kwa majuma au miezi kadhaa kabla ya kuwa…
Mapapai bora hupelekea soko lenye tija
Mapapai ni zao moja kati ya mazao ya matunda yenye vitamin A na madini ya kalsiamu kwa wingi na zao hili hulimwa karibu kila mahali hapa nchini kwa wastani wa tani 2,582 kwa mwaka. Ili kuweza kuzalisha zao la papai kwa wingi na kwa ubora unaotakiwa ni muhimu kuhakikisha unazingatia kanuni zote za kilimo bora za uzalishaji wa mapapai. Ubora…
Nimepiga hatua kwa kulima Canavalia
“Nilikuwa naotesha ekari tatu za mahindi na maharage lakini niliishia kuvuna chini ya gunia 10 za mahindi lakini pia nikipata maharage kidogo sana”. Hivyo ndivyo alivyoanza kueleza Bi. Edvester O. Yambazi (68), mkazi wa Sanya Juu ambaye kwasasa ameamua kufanya kilimo cha mahindi huku akiotesha zao funikizi aina ya Canavalia. Safari ya kilimo Bi. Yambazi anaeleza kuwa, aliteseka kwa muda…
Namna bora ya kuvuna na kusindika mbaazi
Nimelima zao la mbaazi kwa muda mrefu sana, na miaka yote nimekuwa nikipata faida, mpaka hivi karibuni bei ya zao hili ilipoanguka na tukapata hasara. Je ni namna gani naweza kuhifadhi zao hili au kusindika? Msomaji MkM-Arusha. Mbaazi ni kati ya mazao jamii ya mikunde ambayo hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Mtwara, Dodoma, Lindi, Pwani, Morogoro, Arusha, Manyara, Tanga…
Rutuba ya udongo ndio uhai wa udongo na tija kwa mkulima
Ni muhimu kwa mkulima kuhakikisha anauilisha udongo kwa kutumia virutubisho vya asili, ili kuweza kuwa na rutuba na kuzalisha mazao yenye tija. Rutuba ya udongo inafafanuliwa kwa uwezo wake wa kutoa virutubisho vyote muhimu. Hii ni kwa kiasi kinachotosheleza na katika urari sahihi kwa ajili ya ukuaji wa mimea, bila ya kutegemea matumizi ya moja kwa moja ya virutubisho. Vipengele…