UNAFAHAMU KUHUSU UGONJWA HUU! USIACHE KUSOMA JARIDA LA MKULIMA MBUNIFU TOLEO LIJALO LA APRILI!
Mifugo
Vyanzo vya virutubisho
Ni vyema kujenga uelewa wa vyanzo vya virutubisho vinavyoweza kutumika katika kilimo hai. Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo. Kuna mwingiliano kati ya uzalishaji wa mimea na mifugo na unachangia katika kurutubisha udongo. Mabaki ya mazao hulisha wanyama na samadi ya wanyama hurutubisha udongo. Pia, mifugo hao, kama madume, wanaweza…
Busta ya asili
Busta za asili ni nyongeza ya virutubisho kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa mmea ili kua na uzalishaji mzuri hususani pale ambapo mimea imeanza kuzorota kutokana na kupungua/kukosekana kwa virutubisho vya kutosha kwenye udongo, busta hizi zina sifa ya kuupa mmea virutubisho kwa haraka sana na kuleta matokeo mazuri kwenye mimea ndani ya muda mfupi(siku 3). Aina za busta 1.…
Ufugaji wa ng,ombe wenye tija
Naomba ushauri, nina ng’ombe mmoja ambaye namfuga ndani. Amezaa uzao wa kwanza ndama dume. Kwa sasa, ninapata lita 10 kwa siku. Ng’ombe ana uzito wa kilo 400. Gharama za utunzaji ni 70%. Nifanye nini ili awe na tija? Faida zinazotokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa zinatokana na kujumuisha mambo mawili muhimu; aina ya ng’ombe na utunzaji wake. Utunzaji huchukua…
Mkulima hupaswi kuwa maskini
Swali hili limekuwa likijirudia mara kwa mara, kuwa ni kwa nini wakulima wawe maskini? Kwa watu walio wengi hata wakulima wenyewe, wana majibu mengi sana ambayo wamekuwa wakiyatoa, hasa katika kutetea huko hiyo, huku wakiweka kuwa wao ni watu wa chini na wanaokubaliana na hali hiyo ya umaskini. Kuna wale ambao watasema kuwa ni maskini kwa sababu ya zana duni…
Namna ya kufanya candling (uchunguzi wa mayai yanayototoleshwa)
Makala hii ni muendelezo wa makala iliyopita ambapo ilijikita katika kuelezea namna ya kutotolesha mayai kwa njia ya asili na pia kwa njia ya mashine (Incubator). Katika muendelezo huu tutaangalia kwa undani jinsi ya kuchunguza yai kwa kutumia mwanga. Candling ni njia ya kuchunguza mayai kwa kutumia mwanga aidha wa mshumaa au tochi. Tochi ambayo ni kifaa cha kisasa ni…
Mambo muhimu ya kuzingatia kwa unenepeshaji wa nguruwe
Nguruwe wanaonenepeshwa wanahitaji kutunzwa vizuri ili waweze kufikia uzito wa kuchinjwa mapema. Nguruwe waanze kunenepeshwa wakiwa na umri wa wiki 9 hadi 14 na uzito wa kilo 25 hyadi 30. Nguruwe wana uwezo wa kuongezeka uzito wa hadi gramu 700 na 800 kwa siku kuitegemeana na aina ya nguruwe na matunzo. Nguruwe wanaweza kunenepeshwa na kufikisha uzito wa kuchinjwa yaani…
Maharagwe ya ngwara: Muunganiko wa lishe ya kiafrika
Ngwara ambalo pia hujulikana kama Fiwi, ni aina ya maharagwe katika familia ya Fabaceae. Asili yake ni katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na hulimwa katika maeneo ya kitropiki. Zao hili lenye utajiri wa virutubisho, ambalo kwa muda mrefu lilisahaulika, sasa limeanza kupata umuhimu mkubwa kutoka kwa wadau wa kilimo. Zao hili linastawi katika hali ya hewa…
Je, unajua unaweza kutengeneza maziwa ya unga nyumbani?
Maziwa ni bidhaa ya chakula ambayo kila mtu anahitaji. Ni moja ya lishe bora yenye protini nyingi za hali ya juu, kalsiamu na vitamin B12. Aidha kuongezeka kwa wafugaji na wazalishaji maziwa kumeibua changamoto kwa baadhi yao ambao wamekuwa wakiuza maziwa na kuyagandisha na mengine kubaki. Hali hii imewafanya baadhi ya wafugaji kupata hasara kutokana na maziwa kuharibika. Lakini maziwa…