Vitoto vya mbuzi na kondoo wanahitaji uangalizi mzuri kwa sababu wao ni mbuzi na kondoo wa kesho. Utunzi mzuri unawafanya kuwa wenye nguvu na afya. Utunzaji wa mbuzi huanza mara tu baada ya kuzaliwa. Mfugaji ahakikishe yafuatayo; Kitoto cha mbuzi/kondoo kinapata maziwa ya mwanzo (dang’a) ndani ya masaa 24 tangu kuzaliwa na kwa muda wa siku 3. Kama kinanyweshwa maziwa,…
Mifugo
Nguruwe wanahitaji kupata chakula chenye virutubisho sahihi
Nguruwe huhitaji kulishwa vizuri ili waweze kukua haraka na kufikia uzito wa kuchinjwa mapema. Ikiwa watatunzwa vizuri watafikia uzito wa kilo 60 hadi 90 wakiwa na umri wa miezi sita hadi tisa. Nguruwe ana uwezo wa kula vyakula vya aina mbali mbali ikiwa ni pamoja na mabaki ya vyakula vya nyumbani, shambani na viwandani. Pamoja na vyakula hivyo, ni muhimu…
Ukweli kuhusu ufugaji wa ng’ombe wa maziwa
Ikiwa wewe siyo mfugaji wa ng’ombe na unahitaji kufanya hivyo ila unaogopa kulingana na habari toka kwa wafugaji wengine, hebu soma baadhi ya taarifa hizi huenda zikakushawishi kufanya mradi huu kwa furaha na kwa ufanisi zaidi. Unaweza kuanzisha mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa ukiwa na eneo dogo. Unachotakiwa ni kuwa na sehemu inayotosheleza kuwafugia idadi ya ng’ombe ulionao.…
Ni muhimu mkulima kuelewa magonjwa ya mimea
Tafsiri rahisi ya magonjwa ya mimea ni hii: Ni kuwepo kizuizi, au usumbufu fulani unaosababishwa na magonjwa au viumbe fulani kusababisha vichocheo vya ukuaji wa mimea kutokufanya kazi katika hali yake ya kawaida. Kutokana na sehemu ya mmea kupata usumbufu huo, seli za mmea zinaweza kufa au hata kusababisha mmea kufa kabisa. Jambo hili kwa kawaida husababisha kuathirika kwa kiwango…
Tumia mihogo kulisha kuku
Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa nyuzi za mihogo zinaweza kutumika kwa ajili ya chakula cha kuku wanaotaga. Sekta ya kuku hapa Tanzania hutegemea nafaka pamoja na jamii ya kunde kwa ajili ya kutengeneza lishe ya kuku. Nafaka kama vile mahindi, mtama, ngano na shayiri ni chanzo kikubwa cha vyakula vya nguvu katika ulishaji wa kuku. Jamii ya kunde kama…
Kwa nini tunafanya kilimo? Falsafa na umuhimu
Kilimo kimekuwepo tangu zama za mababu zetu. Binadamu wa kwanza walipata chakula chao kwenye mazingira yanayowazunguka na kwa juhudi kama uwindaji kabla ya kuanza kulima ardhi, kupanda mazao na kufuga mifugo kama vyanzo vya lishe. Hii ni pamoja na nafaka, mazao ya mizizi, karanga, matunda, nyama, maziwa, na hata mayai. Kilimo kimebadilisha maisha na maisha pia yamebadilisha muundo wa kilimo.…
Uzoefu husaidia kutambua mnyama anapokuwa kwenye joto
Uzalishaji wenye faida kwa ng’ombe wa maziwa huhitaji uangalizi wa karibu, unaowezesha kutambua ni wakati gani ng’ombe ana joto, hivyo kufanya uhamilishaji kwa wakati unaotakiwa. Kushindwa kutambua joto ni chanzo kikubwa cha urutubishaji hafifu. Mbali na Tanzania, kulingana na utafiti uliofanywa na chuo cha PennState huko Marekani, takriban nusu ya joto hushindwa kutambulika katika uzalishaji wa maziwa nchini humo. Hata…
Fuga kondoo kisasa uboreshe pato lako
Kwa siku za nyuma, jumla ya idadi ya kondoo wanaofugwa hapa nchini Tanzania ilikaribiana kuwa sawa na idadi ya mbuzi nchini kote. Kwa sasa, idadi ya kondoo imepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na idadi ya mbuzi. Hii imetokana na wafugaji kuhamishia mapenzi yao kwenye ufugaji wa mbuzi. Kama walivyo mbuzi, kondoo pia wanaweza kufugwa na wafugaji wadogo wadogo na kwenye…
Ulishaji wa majani machanga ni hatari kwa afya ya mifugo
Mabadiliko ya hali ya hewa ni jambo muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku, hata katika ufugaji mabadiliko haya ya hewa yanaweza kuleta athari katika mifugo yetu. Ukame wa muda mrefu unasababisha kupungua au kuisha kwa malisho ya wanyama. Majani machanga ni yapi Majani machanga ni yale yanayo chipua baada tu ya mvua kunyesha. Majani haya ni hatari sana…
Sumu zinazoweza kuathiri mbuzi
Pamoja na kuwa kuna magonjwa mengi yanayoweza kuathiri mbuzi, pia sumu zinazopatikana katika baadhi ya miti, mimea, dawa au hata wanyama, huweza kusababisha mbuzi kufa mara atakapokula. Baadhi ya sumu zinazoweza kusababisha mbuzi kufa ni kama zifuatayo; 1. Sumu ya lukina Mmea huu una sumu iitwayo mimosine, ambayo ikiliwa kwa kiasi kikubwa huleta madhara kwa mbuzi. Dalili Mbuzi aliyekula sumu…