Miti ya malisho ni chanzo rahisi cha protini kwa ng’ombe wa maziwa. Miti hii hutoa chakula chenye protini ya kutosha katika msimu wote wa mwaka. Wafugaji wanaweza kuokoa pesa endapo watapanda miti ya malisho jamii ya mikunde kama vile desmodium na lusina. Miti ya malisho pia husaidia kuboresha udongo kwa kutoa matandazo ya kijani au kuongeza nitrojeni kutoka hewani. Kaliandra:…
Mifugo
Mbolea ya mifupa, kwato na pembe
Napenda kuchangia kipengele cha matumizi ya mbolea za asili toka Jarida la mkulima mbunifu toleo la 3 Novemba 11 na Moduli ya 11. Kusanya mifupa, pembe au kwato kutoka kwenye bucha, hotelini, machinjio, mabandani na nyumbani kwako. Rundika kisha choma moto. Kwa kawaida mifupa huwaka kwa urahisi sana na kwa muda mfupi. Baada ya kuungua, acha mifupa, pembe au kwato…
Hakikisha unaweka mipango thabiti katika uzalishaji
Imekuwa ni kawaida kwa wakulima walio wengi kufanya shughuli zao bila kufanya maandalizi thabiti, na bila kuwa na mipango endelevu. Jambo hili ni hatari sana kwa maendeleo, hii ni kwa sababu hautaweza kufanya kazi zako kwa malengo. Utakuwa mtu wa kuchukua kila linalokuja mbele yako, na mwishowe unajikuta haujaweza kufanya jambo la maendeleo na kutokufikia malengo pia. Mwaka umeanza, endapo…
Ni muhimu kuzingatia utunzaji bora wa vifaranga
Kwa karne na miaka mingi, ufugaji wa kuku imekuwa ni kazi muhimu na inayokubalika katika jamii nyingi. Ni kazi isiyohitaji gharama kubwa sana, ambayo imekuwa na mafanikio kwa kiasi kikubwa kwa wanaiofanya kibiashara. Tatizo ambalo limekuwa sugu na kusababisha hasara kwa wafugaji walio wengi, ni kutofahamu namna bora ya kuwatunza vifaranga kuanzia siku ya kwanza wanapoanguliwa hadi kuwa kuku wakubwa.…
Namna bora ya kutunza ndama kwa uzalisha wenye tija
Utunzaji wa ndama mfugaji anapaswa kutunza ndama vizuri kwa lengo la kupata ng’ombe wengi na bora kwa ajili ya maziwa. Mambo muhimu ya kuzingatia katika utunzaji wa ndama tangu kuzaliwa hadi kuachishwa maziwa ni pamoja na; Kuhakikisha kuwa ndama anapakwa dawa ya kuzuia maambukizi ya viini ya magonjwa kupitia kwenye kitovu, kwa mfano dawa joto (Tinture of Iodine) mara baada…
Tumia Teknolojia Rahisi Kuboresha Uzalishaji
Teknolojia ifaayo ina sehemu kubwa katika kuboresha mapato ya wakulima kwa kutoa suluhisho na kuongeza uendelevu yanayoendana na mahitaji na masharti mahususi ya wakulima wadogo. Ikiwa wakulima watatumia teknolojia inayofaa basi wanaweza kuongeza kipato chao hasa katika kuongeza thamani mazao yao. Kutokana na hilo, kwa miaka mingi sasa, kumekuwa na jitihada nyingi kwa ajili ya kuleta mabadiliko na ukombozi wa…
HERI YA MWAKA MPYA WA 2025!!!!!!
Ni matumaini yetu kuwa tumevuka wote salama na tuko tayari kuanza mwaka kwa kishindo na kwa mafanikio makubwa. Mkulima Mbunifu tumejiandaa vyema kuendelea kufikisha elimu kwako na kwa kushirikiana na wewe katika kuhakikisha tunatatua changamoto zote za kilimo na ufugaji na kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora na salama huku tukilinda afya zetu, afya za wanyama, afya ya mimea pamoja na…
Masomo kupitia jarida ni suluhisho la changamoto za wakulima
“Mimi ni mkulima na mfugaji, Ninazalisha kwa misingi ya kilimo ikolojia. Situmii pembejeo sumu za viwandani kuanzia ninapootesha zao husika au kuanza uzalishaji wa mifugo yangu mpaka ninapovuna, kuhifadhi na kuuza mazao yangu. Ninafanya uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali kama vile ndizi, kahawa, njugu, maharage, mahindi, mbogamboga, na pia ninafanya ufugaji wa kuku pamoja na mbuzi.’’ Hayo ni maneo…
Wakulima waungana kufanikisha mradi wa ufugaji wa kuku
Umoja ni nguvu na wakulima wanapoungana pamoja, mambo mazuri hufanyika. Wanatiana nguvu, kuleta rasilimali pamoja na kuanzisha miradi ambayo ni ngumu kwa mkulima mmoja kuanzisha. Kikundi cha Shangushangu kilichopo kijiji cha Narunyu, kata ya Tandangongoro, mkoani Lindi lina wanachama 16 (wanawake 8 na wanaume 8) na kilianzishwa mwezi wa saba mwaka 2023 likiwa na lengo la kujifunza kilimo na ufugaji…
MWENENDO WA MVUA MKOA WA ARUSHA
Ndugu Mkulima, kama tunavyofahamu huu ni msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini, ni muhimu kupata na kufahamu taarifa za mwenendo mzima wa msimu, nini kifanyike au kisifanyike katika uzalishaji na mwenendo wa maisha kwa ujumla. Tafadhali soma kwa kubonyeza hapa chini kupata taarifa kamili kwa mkoa wa Arusha https://www.meteo.go.tz/uploads/publications/sw1724331524-Downscaled%20OND%202024%20Rainfall%20Season%20Outlook%20(Swahili)%20for%20Arusha%20Region%20and%20Districts.pdf