Katika toleo lililopita tuliona ni kwa namna gani mkulima Bi. Edvesta Yambazi alivyofanikiwa katika kulima canavalia. Katika toleo hili tutaangalia kwa undani zao la canavalia ni zao gani na linalimwaje. Canavalia ni zao jamii ya mikunde ambayo hujulikana kwa majina mengine kama Jackbean au swordbean. Kitaalamu au kisayansi hujulikana kama Canavalia Ensiformis. Zao la canavalia ni moja ya mazao funikizi…
Kilimo
Samadi ya wanyama na mimea na namna ya kutumia
Ubora wa samadi ya wanyama hutegemea zaidi kile kilicholiwa na mnyama. Ikiwa wamelishwa chakula duni au nyasi zilizomea katika udongo usio na rutuba, basi samadi yao pia itakuwa na ubora duni. Ikiwa wanyama wamelishwa chakula kizuri basi samadi pia itakuwa bora na iliyojaa virutubisho. Samadi iliyo tayari kwa matumizi Samadi huhitaji kupevuka kwa majuma au miezi kadhaa kabla ya kuwa…
Zalisha mbolea za asili kwa ajili ya kilimo hai
Ili uweze kufanya kilimo hai ni lazima uwe na mbolea za asili. Bila mbolea za asili huwezi kufanya kilimo cha aina yeyote kwa misingi ya kilimo hai. Mbolea za asili zipo za aina mbalimbali ama huweza kutengenezwa kwa njia mbalimbali na kwa kutumia malighafi mbalimbali kama vile samadi, majani ya kurundika nakadhalika. Baadhi ya mbolea za asili na njia za…
Mbolea hai na madawa ya asili ni muhimu kwa mimea, wanyama na binadamu
Mkulima anapotumia mbolea za viwandani na kemikali kwa muda mrefu, ni dhahiri kuwa udongo hudhoofika na kushindwa kuzalisha. Afya yake pia ipo mashakani kwa kuwa kemikali zina madhara makubwa sana. Kilimo ni lazima kuwezesha na kuongeza afya ya udongo, mimea, wanyama na binadamu. Udongo ni nguzo muhimu katika maisha ya viumbe wote kwa ujumla. Udongo ulioharibiwa hauwezi kuzalisha chakula vizuri,…
Je wajua kuhusu mti wa Mlonge (Moringa)
Moringa (Moringa spp.) maarufu kama mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kwa matumizi ya binadamu, wanyama na hata katika kutengeneza virutubishi kadhaa. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji. Faida na matumizi ya mti wa Moringa 1.Virutubishi Faida na matumizi ya mti wa MoringaKaribu kila …
Fahamu udongo wako ili kuboresha usimamizi wa rutuba
Kuna virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ukuaji wa mmea. Upungufu wa mojawapo ya virutubishi hivi muhimu utapunguza ukuaji wa mimea. Mavuno yanategemea kiwango cha virutubisho muhimu kwa mmea. Mimea yote hutegemea vitu muhimu kukua vizuri. Vitu hivi vinaweza kugawanywa mara mbili; Vitu vya madini, kupitia udongo. Vitu visivyo vya madini: haidrojeni, oksijeni, na kaboni ambazo zinapatikana kwa wingi katika…
Kuanzisha biashara kunahitaji mipango thabiti
Miaka ya hivi karibuni serikali pamoja na wadau wengine wamekuwa na mikakati thabiti ya kuendeleza kilimo na kuwashawishi wakulima kuweka shughuli zao katika mtazamo wa kibiashara. Waliochukua na kuufanyia kazi ushauri huo kisha kufanya shughuli zao za kilimo kitaalamu kwa mtazamo wa kibiashara leo wanapata faida kubwa. Wana pesa inayoingia mifukoni mwao na kuziba mapengo yote yaliyokuwa yametokea kabla na…
Otesha miti kwa manufaa yako na kizazi kijacho
Wanajamii wengi hawatambui umuhimu wa miti katika kilimo, mazingira, kwa binadamu na hata kwa wanyama jambo ambalo wengi wamelipuuzia na kutokulichukulia maanani. Tunapozungumzia miti, kwa ujumla tunamaanisha miti ya asili ambayo zipo katika misitu yetu na hata maeneo yetu ya makazi pamoja na ile ya kuotesha inayotupatia rutuba ya udongo, hewa safi, chakula cha wanyama, kivuli, mbao, kuni, madawa…
Maparachichi yaliyopandikizwa hutoa mavuno bora zaidi
Msukumo wa uhitaji mkubwa wa parachichi kwa wingi na zenye ubora unawasukuma wakulima kutumia teknolojia mpya. Upandikizaji hujumuisha aina mbili za mimea. Unachukua mmea mmoja ambao unadhani hauna tija nzuri, na sehemu ya mmea mwingine ambao una ubora zaidi na kupandikiza kwa kukata na kufunga pamoja ili kupata mbegu bora zaidi. Utaratibu wa kupandikiza hivi sasa umekuwa silaha ya wakulima…
Kua mlemavu isiwe kikwazo cha kutofanya maendeleo
Kumekua na dhana katika jamii zetu kuona mlemavu hawezi kufanya jambo lolote la msaada katika jamii yetu. La hasha, watu wenye ulemavu wanauwezo wa kufanya mambo kadhaa iwapo watapatiwa fursa na msaada. Hata hivyo kuna ulemavu wa aina mbili, ulemavu wa kuzaliwa nao na ulemavu kutokana na ajali katika maisha. Katika makala hii Mkulima Mbunifu inamuangazia mlemavu Bwana Ibrahimu Kajia…