- Kilimo

Magonjwa na wadudu wanaoshambulia tikiti maji

Sambaza chapisho hili

Nimekuwa mkulima wa matikiti kwa muda mrefu, ila bado suala la wadudu na magonjwa yanayoshambulia zao hili ni tatizo kwani hubadilika badilika. Naomba kufahamu wadudu na magonjwa yaliyozoeleka. Mduma Hiza wa Mkuranga Pwani.

Katika jarida hili toleo la 10 Januari 2013, tulichapisha makala iliyoeleza vizuri namna nzuri ya uzalishaji wa tikiti maji. Hii ilijumuisha hatua zote muhimu kuanzia utayarishaji wa shamba, magonjwa kwa uchache.

Katika makala hii utaweza kujifunza kwa undani magonjwa na wadudu kama alivyoomba msomaji wetu kutoka Mkuranga ambapo kwa kushirikiana na Nd Dagras Mwamlima ambae ni mwanafunzi Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) utapata kufahamu hayo kwa undani.

Magonjwa na wadudu waharibifu

Kuna aina mbalimbali za wadudu ambao hushambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda.

Pia kuna magonjwa ya ukungu (fangasi), ambayo hushambulia mimea. Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi.

Wadudu wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu za majani na maua, na wengine hushambulia matunda. Pia kuna magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea.

Magonjwa kama ukungu wa unga (powdery mildew) na ukungu wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.

Ili kujua dawa za magonjwa ni vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo za kilimo ili kupata dawa sahihi. Unaweza kutumia dawa za asili au itakavyoelekezwa na mtaalamu wa kilimo katika eneo lako ili kudhibiti magonjwa yaliyotajwa hapo juu.

Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda. Dawa aina ya karate itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.

Magonjwa ya tikiti

(1) Ubwiri chini (downy mildew)

Huu ungonjwa husababishwao na ukungu(fangasi). Ni kati ya mangonjwa yanayoshambulia majani na hupendelea sana wakati wa baridi.

Dalili zake: Majani yaliyoshambuliwa hugeuka rangi na kuwa kama ya njano, huku baadhi ya majani yakiwa kama yanakauka  na madoadoa meusi kwa mbali..

Tiba: Unaweza kutibika kwa dawa yenye viambato vya Metalaxyl na mancozeb.

(2) Ubwiru juu (powdery mildew)

Dalili: Dalili za ungonjwa huu ni pamoja na majani kuwa kama yamemwagiwa unga ua majivu.

Tiba: Unaweza kutibika kwa  dawa yenye kiambato cha Difenoconazole.

3) Kata kiuno (damping off)

Hii ni aina nyingine ya ugonjwa unaoshambulia tikiti maji. Ugonjwa huu husumbua sana miche midogo. Huanzia ardhini, husababisha miche midogo kuanguka chini baada ya kula sehemu ya shina.

Tiba: Inapendekezwa kutumia majivu kwenye kitalu, au tumia Ridomil gold. Anza kupulizia mara tu baada ya mimea yako kuota.

Wadudu wanaoshambulia tikiti

(1) Wadudu mafuta (Aphid)

Wadudu hawa hushambulia majani na kufyonza juisi ya mmea na baada ya kushambulia majani hujikunja na baadaye kusababisha mangonjwa ya virusi.

Dawa: Tumia dawa za asili zinazoua wadudu wa mafuta au Actara na pulizia majani pamoja na udongo. Wadudu wengine ni; Inzi weupe (whitefly).Actara hutokomeza Utitiri mwekundu (Redspidermites).

Kuvuna

Tikitimaji huvunwa baada ya miezi miwili na nusu hadi mitatu kutoka siku ya kupanda. Kuna aina ya tikiti maji ambayo hukomaa kwa siku 60-75 kutokana na aina ya mbegu.

Utambuzi endapo yamekomaa

Ili kujua matikiti yamekomaa inahitaji ujuzi kidogo. Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano, pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu.

Njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake kama tunavyofanya kwenye mafenesi. Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti. Matikiti yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *