- Kilimo

Udhibiti wa wadudu kwenye zao la mihogo

Sambaza chapisho hili

Kwa mtazamo wa kiekolojia, viumbe wote ni sehemu ya mfumo asilia bila kujali vinafanya nini. Kwa mkulima, viumbe vyote ambavyo hupunguza mavuno ya mazao yake huchukuliwa kuwa ni wadudu waharibifu.

Kilimo cha zao la mhogo, kama ilivyo kwa mazao mengine ya mizizi, kina­zongwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wadudu na magonjwa ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiasi cha mavuno, na ubo­ra wa mazao.

Pia changamoto hii ya wadudu na magonjwa ya mihogo inaongeza gha­rama za uzalishaji ambazo hazikutara­jiwa. Ni muhimu kwa mkulima kuwa na ufahamu wake ili aweze kuandaa mazingira bora ambayo yatachochea maambukizi na kuenea kwa wadudu na magonjwa ya mihogo.

Utitiri kijani wa mihogo

Utitiri kijani wa mihogo ni wadudu waharibifu wa mhogo nchini Tanzania na maeneo mengine ya Africa ambao husababisha hasara kubwa katika mavuno. Utitiri unaweza kuenezwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa urahisi kupitia majani, vikonyo na upepo. Mfumo wa mseto unahita­jika ili kudhibiti wadudu na kupungu­za uharibifu.

Njia za kitamaduni kama vile ku­tumia vikonyo safi, kupanda mapema katika msimu wa mvua na kilimo cha mseto na mbaazi, kunaweza kupu-nguza idadi ya wadudu.

Dalili muhimu

  • Utitiri kijani wa mihogo huwa na rangi ya kijani mpaka manjano na huwa vigumu kuonekana kwa ma­cho (huonekana kama vidoa vido­go vya rangi ya kijani-manjano).
  • Utitiri hula upande wa chini wa majani machanga na mashina ya mhogo ya kijani kibichi. Tumia le-nsi ya mkono ili kuweza kuwaanga­lia utitiri upande wa chini wa ma­jani, kwenye mishipa na karibu na mwanzo wa jani.
  • Idadi ya utitiri huongezeka kwenye majani machanga wakati wa mwanzo wa msimu wa ukame na hushambulia mmea kwa kufyonza utomvu kutoka kwenye seli za ti-shu za mmea, ambayo husababi­sha madoa ya rangi ya manjano kuonekana kwenye majani kuto­kana na upungufu wa chlorophyll (kijani kibichi). Majani yanaweza kuwa na mabato na kufa.
  • Dalili hizi zinaweza kuchanganywa na dalili za virusi vya cassava mosa­ic, lakini virusi vya cassava mosaic husababisha mabaka makubwa ya rangi ya kijani-manjano na umbo la majani huharibika. Mashambu­lizi makali ya utitiri kijani wa miho­go husababisha majani ya juu (au mapya) kufa na kuanguka na kilele cha mti wa mhogo huonekana kama mshumaa.

Kinga

Mambo ya kufanya kabla ya dalili kuonekana

Mbinu za kitamaduni

  • Hakikisha kuwa vipandikizi safi vi­natumika.
  • Kagua chomozo mpya kwenye vikonyo vya mihogo kwa karibu ili kubaini uwepo wa utitiri.
  • Panda mapema, mwanzoni mwa msimu wa mvua, ili kuwezesha ukuaji wa majani na mimea amba-yo inaweza kuhimili mashambulizi. Mimea ya mihogo ya umri kati ya miezi 2 na 9 hushambuliwa kwa urahisi.
  • Panda mseto na mbaazi, kila mira­ba miwili au mitatu, ili kupunguza uharibifu na pia kuongeza uzalisha­ji.

Udhibiti na mambo ya kufanya baada ya dalili kuonekana

Mbinu za kitamaduni

  • Utitiri kijani wa mihogo unaweza kudhibitiwa kiasili na kibaiolojia ikiwa ni pamoja na wadudu wana­okula utitiri kama Typhlodromalus manihoti Moraes.
  • Wakati wa msimu, majani ambayo yanaonesha ishara ya utitiri lazima kuondolewa na kuharibiwa mba­li na shamba. Baada ya kuvuna, haribu mabaki yote ya mazao yali­yoathirika.

Athari

Utitiri kijani wa mihogo ni wadudu waharibifu wakubwa wa mihogo. Wanaweza kupunguza mazao sana kwa kupunguza majani na kupunguza uwezo wa mmea kujitengezea chaku­la.

Kutokana na kupungua kwa ukuaji wa mimea, majani machache yanapa­tikana kwa mavuno kama mboga ya kijani na hasara ya mavuno ya miho­go inaweza kuwa kati ya asilimia 10- 80. Vipindi virefu vya ukame vinawe­za kusababisha kuongezeka kwa idadi ya utitiri na kupunguza mazao zaidi.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *