Kilimo

- Kilimo

Msimu wa mavuno; Hakikisha umefuata kanuni sahihi za kuvuna na kuhifadhi nafaka

Nafaka mbalimbali ambayo ni mazao makuu ya chakula na kibiashara hapa nchini kama vile mahindi, maharage, mikunde mara nyingi wakulima hupoteza hasa wakati wa mavuno kutokana na uvunaji usiokidhi viwango pamoja na uhifadhi duni. Ukiwa huu ni msimu wa mavuno katika maeneo mbalimbali nchini, Mkulima Mbunifu inatoa rai kwa wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia kanuni sahihi za mavuno ili waweze kupata mavuno bora…

Soma Zaidi

- Kilimo

Ni muhimu kwa wakulima kuwa na maandalizi sahihi kuelekea mavuno

Wakulima wamekuwa wakipoteza mavuno yatokanayo na mazao kutokana na uvunaji hafifu usiokidhi viwango pamoja na uhifadhi duni. Ikiwa wakulima wanajiandaa kuelekea kwenye mavuno ni vyema kuhakikisha wanaandaa na kuzingatia kanuni bora za uvunaji ili waweze kupata mavuno bora na yanayokidhi chakula na soko kwa ujumla. Wakulima hawana budi kuwa makini na kutambua ni kwa namna gani watavuna mazao yao ikiwa…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara

Umakini wa uzalishaji huzuia upotevu wa chakula

Upotevu wa chakula hutokea katika wigo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji.   Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi. Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla ya chakula kumfikia mlaji. Kwani chakula…

Soma Zaidi

- Kilimo

Sindika viazi vitamu kuongeza thamani na pato

Ni muhimu kusindika viazi vitamu ili kuongezea thamani, ubora na matumizi yake. Viazi vitamu husindikwa kupata viazi vitamu vilivyokaushwa, unga, wanga na jamu. Ukaushaji wa viazi vitamu kwa ujumla wake huhitaji au hutumia nishati ya jua ambapo ni lazima mkulima kuzingatia kanuni  kwa ajili ya kukausha mazao yake. Kanuni muhimu za ukaushaji Ukaushaji hupunguza maji kwenye zao la viazi vitamu…

Soma Zaidi

- Kilimo

Dawa za asili kwaajili ya kudhibiti wadudu kwenye mbogamboga

Kama ilivyo kwa aina nyingine ya kilimo kuwa na changamoto, wadudu pia ni moja ya changamoto inayowakabili wakulima wa kilimo hai na mara nyingi wamekuwa wakipambana kutafuta utatuzi. Aidha, dawa mbalimbali za asili zimeonekana kufanya vizuri katika kudhibiti mashambulizi ya wadudu hawa kwenye mimea. Phytolacca Dodecandra Mmea huu hutumika kama dawa ya kuulia wadudu kama vile aphids, mealy bugs, caterpillars,…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara, Mazingira, Udongo

Kanuni ya haki na uangalizi katika misingi ya kilimo hai

Kama ambavyo maandalizi sahihi hufanyika katika shughuli yeyote ya kimaendeleo, katika kilimo hai pia kanuni ya haki na usawa pamoja na uangalizi visipozingatiwa vyema mkulima hawezi kufaidika na kilimo hai. Kanuni ya haki na usawa Kilimo hai sharti kizingatie msingi wa mahusiano yatakayohakikisha usawa katika mazingira na fursa ya kuishi.Usawa unaojali na kuzingatia heshima, haki na kujituma kwa kila mmoja…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Mazingira, Mifugo, Udongo

Re-Thinking Food: Transforming Food Systems for People and Planet | Frank Eyhorn | TEDxIHEID

Just click here to watch Climate change, biodiversity loss, poverty, health issues: what we eat and how we produce our food is shaping the face of our planet and of our societies like no other human activity. The hidden costs of cheap food are mind-blowing. At the same time, food is currently one of the most powerful levers for changing…

Soma Zaidi

- Kilimo

Umuhimu wa wataalamu kwa wakulima na wafugaji

Wataalamu wa kilimo na mifugo wamepata mafunzo ili kuendeleza mbinu za kilimo na mifugo kwa lengo la kutoa faida kwa wakulima na wafugaji. Baadhi ya wataalamu wanaweza kuona upungufu fulani au kuona kuwepo kwa mantiki kwenye baadhi ya mbinu za asili ambazo bado zinatumiwa katika uendeshaji wa kilimo na ufugaji na kuweza kuafikiana na wakulima hao juu ya kuziendeleza au…

Soma Zaidi

- Kilimo

Mambo muhimu ya kuzingatia unapoanzisha kilimo biashara

Mkulima ni mfanyabiashara, na mfanyabiashara yeyote analenga faida kubwa au hasara kidogo sana. Ni muhimu kwa mkulima kujua thamani ya mazao yake ili aweze kujua ni bei gani anayotakiwa kuuzia mazao yake lakini pia ajue bei ambayo akiuza kwayo itamletea hasara. Unapoanzisha mradi wa kilimo biashara, unatarajia mwisho wa siku umalizike kwa kupata faida. Kuna mambo mawili makubwa miongoni mwa…

Soma Zaidi

- Kilimo

Kilimo cha kiikolojia kwa wakulima wadogo

Kilimo cha kiikolojia cha wakulima wadogo ni aina ya maisha yanayoichukulia dunia kwa heshima na kuithamini, na siyo kama kitu cha kunyonywa. Ni mfumo wa maisha unaonyesha kuwa upo uhusiano wa karibu kati ya binadamu na mazingira yanayowazunguka na hivyo mazingira hayo yasithaminishwe kwa pesa. Mfumo huu unaoelewa kuwa matumizi mabaya ya mazingira na kuyafanya chanzo cha pesa kutaangamiza watu…

Soma Zaidi