Binadamu
Mimi nasoma Jarida la Mkulima Mbunifu, wewe Je?
Hebu tazama tabasamu la mama huyu usoni, mara tu aonapo jarida la Mkulima Mbunifu na azidi pale anapokutana na taarifa muhimu kwake? Ni furaha iliyoje? Hebu na wewe kuwa mmojawapo wa wanufaika wa jarida hili, nakuahidi hutajutia….. Jarida pekee lililosheheni taarifa za kilimo hai, ufugaji wa mifugo aina mbalimbali, utunzaji wa udongo, mazingira na afya ya mwadamau kwa ujumla…… Mkulima…
TUNAOMBA RADHI KWA KUCHELEWA KUTUMA JARIDA LA OKTOBA
Habari ndugu msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu. Ni matumaini yetu kuwa uko salama na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Tunaomba radhi kwa kuchelewa kukutumia nakala yako ya jarida la Mkulima Mbunifu. Hii ni kutokana na kuwepo kwa changamoto kidogo zilizokuwa nje ya uwezo wetu ambazo zimepelekea kusindwa kuchapisha nakala ya mwezi Oktoba kwa wakati. Jarida hili…
Tunaomba radhi kwa kutokusikika hewani
Ndugu msikilizaji na mfuatiliaji wa vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu/SAT, tunaomba radhi kutokana na kipindi chetu kilichokusudiwa kurushwa hewasi siku ya jumamosi tarehe 30 Oktoba 2021 kutokusikika. Hii ni kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu. Sasa kipindi hicho cha kilimo kilichokuwa kinahusu kilimo mseto na kilimo cha mzunguko wa mazao kitarushwa upya siku ya jumamosi ya tarehe…
Sikiliza vipindi vya redio vya Mkulima Mbunifu
Tunapenda kuwataarifu na kuwakumbusha wasomaji wetu kusikiliza vipindi vya radio vya Mkulima Mbunifu Vinavyosikika kupitia TBC Taifa kila siku ya jumamosi saa mbili na robo usiku (2:15) na marudio siku ya alhamisi saa tisa na nusu mchana (9:30) Kupitia vipindi hivi, MkM inatoa elimu stahiki kwa kurusha mada mbalimbali kwa wakulima wadogo na hata wakubwa, kuweka kipaumbele katika kuthamini misingi…
Gugu karoti lina madhara makubwa
Gugu karoti (Parthenium hysterophorus) ni mmea vamizi ambao una madhara mengi kwa binadamu, mazao, wanyama au mifugo pamoja na kuharibu uoto wa asili. Gugu hili lina madhara mengi kama; Muwasho unaoweza kusababisha kujikuna na kupata malengelenge, ugonjwa wa pumu ukivuta vumbi lake, muwasho wa macho, mnyama kupasuka na kuvimba midomo kama akila majani. Aidha gugu karoti husababisha maziwa ya ng’ombe…
Sindika togwa kwa matumizi ya muda mrefu
Togwa ni kinywaji cha asili kinachonyweka kwenye maeneo mengi Tanzania pamoja na nchi zingine lakini ikitumika zaidi katika maeneo ya wakulima. Kinywaji hiki chenye asili ya ubaridi kinatengenezwa kwa kutumia nafaka kama vile mahindi, ulezi, mtama (isipokuwa ngano) japo inasadikika pia kuwa kuna maeneo mengine wanatengeneza kwa kutumia matunda. Asili ya togwa hapa nchini inasadikika kuwa imetokana na wanajamii wa…
Imarisha afya ya mifupa kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali za kilimo hai
Mifupa yetu inarekebishwa kila wakati na tishu za mfupa zinavunjwa na kujengwa mara kwa mara. Uzani wa mfupa kawaida huongezeka hadi wakati wa utu uzima, lakini baada ya hapo, shida inaweza kukupata. Mifupa huupa mwili mwonekano sahihi, hulinda viungo vya ndani ya mwili (mfano Fuvu linalinda ubongo na kifua na mbavu zinalinda mapafu), hukusaidia kutembea, hutunza madini muhimu ya mwili…
Miaka kumi ya Mkulima Mbunifu
Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011. Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini…
Miaka 10 ya huduma kwa wakulima wadogo
Maoni kutoka kwa wakulima yanaonyesha kuwa wakulima wadogo wana hamu ya kujifunza njia mpya na endelevu za kilimo ambazo zinaboresha mapato yao. Inaonyesha kwamba wanatambua na kuthamini mchango wa MkM katika kuendeleza na kupanua kilimo biashara na kutunza mazingira. Tangu kuanzishwa kwa jarida hili mnamo Julai 2011, Mkulima Mbunifu, maarufu kwa wakulima kama MkM limejikita katika kuwaelimisha wakulima kuthamini msingi…