- Mifugo

Zalisha matunda kwa malengo

Sambaza chapisho hili

Moja ya mazao ambayo wakulimwa wamekuwa wakizalisha kwa ufanisi mkubwa na kupata mavuno mazuri, ni matunda ya aina mbalimbali. Ambapo kulingana na mazingira waliyopo, wakulima wamekuwa wakizalisha aina mbalimbali na kwa misimu tofauti.

Pamoja na mafanikio hayo, wakulima wamekuwa wakizalisha aina hizo za matunda bila kuwa na malengo kamili kuwa ni nini wanachohitaji kutokana na matunda hayo, jambo ambalo mwisho wake huishi kwa matunda hayo kuoza na kutupwa bila wakulima kufaidika.

Njia pekee ambayo mkulima anaweza kuepukana na hasara hiyo ni kwa kujifunza usindikaji wa aina mbalimbali za matunda, ili endapo atazalisha kwa kiasi kikubwa bila kupata soko, aweze kusindika na kuuza ikiwa bidhaa kamili, jambo ambalo litasaidia katika kuongeza kipato na kuepuka upotevu wa matunda hayo.

Unaweza kujifunza njia za usindikaji kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari, kutoka kwa wakulima wenzako, pamoja na kujiunga kwenye vikundi ili kuweza kupatiwa mafunzo mtakayohitaji kutoka kwa wahisani mbalimbali.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *