- Mifugo

Ulishaji wa majani makavu: Usisahau maji

Sambaza chapisho hili

Kabla ya kulisha wanyama majani makavu ni muhimu sana kufahamu ni kwa namna gani yanahitajika kulisha kwani majani haya ni tofauti na majani mabichi.

Kiwango cha majani makavu kiwe kidogo zaidi ya majani mabichi. Robota moja la kilo 15 la majani makavu ni sawa na kilo 75 za majani mabichi, na yanaweza kulishwa kwa ng’ombe anaetoa maziwa vizuri mara moja kwa siku.

Ikumbukwe pia kuwa usagaji wa chakula kikavu tumboni unahitaji kiwango kikubwa sana cha maji, vinginevyo itaathiri utoaji wa maziwa kutokana na kukosa maji ya kutosha.

Ukaushaji wa majani

Majani jamii ya mikunde yaliyokaushwa ni malisho mazuri wakati wa kiangazi yenye virutubisho vya protini. Kata majani wakati yakiwa yanapatikana kwa wingi hasa kipindi cha mvua. Yaanike katika eneo safi kwa siku tatu sawa na ulivyokausha malisho ya kiangazi. Majani hayo yanapokauka vizuri yanaweza kuhifadhiwa katika mifuko. Wape ng’ombe kati ya kilo 3-4 kwa siku na ½ kilo kwa mbuzi au kondoo.

Hesabu mifugo wadogo kama nusu ya mfugo mkubwa wa wastani.

Usisahau mifugo wadogo unapofanya hesabu ya kiasi cha malisho unachohitaji kuhifadhi kwa ajili ya kiangazi.

Mifugo wadogo pia wanahitaji virutubisho vya kutosha ili kuendeleza afya zao.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *