- Mifugo

Namna ya kupata faida kutokana na uzalishaji wa maziwa

Sambaza chapisho hili

Wafugaji huzalisha maziwa na kuyauza moja kwa moja sokoni na mara nyingi maziwa hayo huweza kusalia kwa kukosa wanunuzi. Maziwa hayo kutumika kwa matumizi ya nyumbani na wakati mwingine huweza kuharibika na kupelekea kumwaga.

Hii imekuwa changamoto na kusababisha hasara kwa wafugaji.  Katika makala mbalimbali zilizopita tumejaribu kueleza namna ya kuzalisha maziwa kwa wingi. Pia jinsi ya kufanya usindikaji. Kuna njia ambazo mzalishaji wa maziwa anaweza kujifunza na kumsaidia kupata pato kubwa.

  1. Kugawanya mifugo

Shughuli za uhamishaji wa makundi ya mifugo kutoka sehemu moja hadi nyingine kutafuta malisho na maji hufanya uzalishaji wa maziwa kuwa mgumu. Namna ya kuondokana na tatizo hili ni kugawanya mifugo.

Namna ya kufanya

  • Gawanya mifugo inayokamuliwa na isiyo kamuliwa.
  • Mifugo inayokamuliwa katika eneo ambalo unaweza kuwapa chakula kilichohifadhiwa au chakula kilichonunuliwa na hakikisha ina afya njema na kuwakinga na magonjwa.
  • Mifugo iliyosalia ambayo haikamuliwi unaweza kuwaswaga ili kujitafutia malisho.
  1. Unda kikundi cha masoko

Ikiwa mifugo yako ni michache na hutoa maziwa kila mmoja kwa wakati wake, basi utakuwa na kiwango kidogo cha maziwa kwa ajili ya kuuza.  Hivyo utashindwa kumudu uhitaji wa maziwa kwenye na  wauzaji wadogo ambao wanahitaji maziwa kila siku kwa wingi na kwa ubora unaohitajika.

Namna ya kufanya

Unda kikundi kwaajili ya kuzalisha na kuuza maziwa kwapamoja. Mnaweza kuzalisha kwa wingi na kuwa rahisi kwa mfanyabiashara kununua, kuongezea thamani na kuuza. Kwa njia hii mzalishaji atakuwa na nafasi ya kuzungumza, kusaidiana baadhi ya majukumu, kubadilishana mawazo na hata kupata huduma kama mikopo na mafunzo.

Hakikisha kwamba wanawake wanakuwa sehemu ya kikundi. Hii ni kwasababu mara nyingi wao ndiyo hufanya shughuli za kukamua, kutengeneza siagi na jibini, na kuuza bidhaa zitokanazo na maziwa kwenye masoko ya ndani.  Pia wanahitaji maziwa kupikia na kulisha watoto.

  1. Anzisha kituo cha kukusanyia maziwa

Kuna gharama kubwa na upotevu wa muda kwa mfanyabiashara wa maziwa kuchukua kiasi kidogo kidogo cha maziwa kutoka maeneo yaliyotawanyika. Kuanzisha kituo cha kukusanya, kwani kutahimiza wafanyabiashara na wenye viwanda kuweza kununua maziwa na kuweza kupata bei ya juu.

Namna ya kufanya

  • Anzisha kituo chako cha kukusanyia maziwa wewe pamoja na wanakikundi wenzako katika eneo linalofaa.
  • Weka mpango wa ukusanyaji wa maziwa kila siku asubuhi kwa wanakikundi wazalishaji wote ili yaweze kuchukuliwa haraka na gari mahususi lenye friji.
  • Hakikisha maziwa yanayoletwa na wanakikundi kituoni ni mabichi na hayajachafuliwa.

Vifaa vinavyohitajika

  • Keni, vyungu, ndoo, vifaa vya kukoroga, faneli na chujio vyote vilivyotengenezwa kwa alumini au chuma kisicho pata kutu
  • Mizani kwa ajili ya kupima.
  • Keni kwaajili kusafirishia .
  • Vifaa vya kupima na kusafirishia kama vile Testing tube, glassware, vijiko, kichomea mafuta ya taa, pipettes, laktomita, measuring cylinder, kemikali.
  • Neti kuzuia nzi
  • Maji safi yanayotiririka
  • Vifaa vya kupozea kama vitapatikana.
  • Pata ushauri wa jinsi ya kuanzisha na kusimamia kituo cha ukusanyaji kutoka serikalini au shirika la maendeleo

  1. Anzisha kiwanda kidogo cha usindikaji

Kiwanda kidogo kilichokaribu na jamii kitasaidia jamii husika kunua maziwa lakini pia kupata ajira. Pia itakuwa msaada kwa wahitaji wa karibu pamoja na kuuza bidhaa za maziwa mijini.

Kiwanda hiki kinaweza kufanya kazi katika msimu wa mvua ambapo kuna maziwa mengi na huweza kuongezewa thamini na kufungashwa au kusindikwa kupata bidhaa mbalimbali kama vile yogati, samli na bidhaa zingine.

Namna gani utafanya

  • Tengeneza mpango kazi, hii itakusaidia kufahamu soko na bidhaa hitajika.
  • Anzisha kiwanda kidogo mahali panapostahili.
  • Weka maziwa yawe safi. Unahitaji kuchemsha au kupasha moto kuondoa wadudu kisha kuyapooza. Unaweza kuua wadudu kwa kuyapasha moto kufikia digrii 63 za sentigredi kwa dakika 30 kisha kuacha yapoe kisha weka kwenye jokofu.
  • Vifaa utakavyo hitaji: jiko la gesi, jokofu, kipima joto na saa, kikoroga siagi, chombo ya kutengeneza maziwa mtindi, jibini na sura pamoja na vifaa vya kufungashia yaani mifuko ya plastiki kwa maziwa na vikombe vya plastiki vya yogati.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *