- Mifugo

Mkulima Mbunifu imenihamasisha kuanza kufanya kilimo hai

Sambaza chapisho hili

“Nimeamua kuanza kufanya kilimo hai kwani ni rahisi, sitatumia dawa za kemikali wala mbolea za viwandani.  Nilikua nikifanya kilimo cha mazoea bila kujali afya yangu na watu wengine. Sikufahamu madhara kwa mazingira yani ardhi, mimea na hata wanyama”.

Hayo ni maneno ya Godwin Zakaria Axwesso (52) anayeishi kijiji cha Bashay, wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha.   Alifanya kilimo cha kawaida cha (msimu) kutegemea mvua, lakini nimeshuhudia madhara kadhaa kutokana na matumizi ya viuatilifu vya kemikali na mbolea za viwandani.

Umepata wapi elimu ya kilimo hai

‘’Mimi ni msomaji wa taarifa mbalimbali za kilimo kupitia kwenye mitandao ya kijamii, na ndipo nilipoweza kukutana na Mkulima Mbunifu na kupata mawasiliano. Nilisafiri hadi ofisi ya Mkulima Mbunifu Arusha kupata maelezo kwa undani.

Nilipata elimu kutoka kwao na pia kupokea majarida kadhaa ambayo yalisheheni makala mbalimbali za kilimo hai.  Niliongeza elimu ya kilimo hai kwa kujiunga na mafunzo kutoka shamba la kilimo hai huko Kwanyange_Mwanga (Saint James Sustainable Organic farm) ambapo nilifanya mafunzo kwa vitendo na  kuongezea mwamko wa kuanza kilimo hiki” alisema.

Aliongeza kuwa, jamii inayomzunguka haifanyi kilimo hai, kwa hiyo  anatumaini mafanikio yake katika kilimo hai yatahamasisha na jirani zake, kwani wengi wanafanya kilimo cha mazoea.  Hivyo ameamua kuanza katika eneo dogo kisha atumie kama shamba darasa kuwaelimishe wengine ili waachane na kilimo cha mazoea na kujikita katika kilimo hiki chenye manufaa kwa afya ya kizazi cha sasa na kijacho.

Kwanini kilimo hai

Nikiwa na mke wangu tunakula ugali na mboga ya majani, nilihisi ladha ya tofauti katika kinywa changu, nikamuuliza mke wangu mahali alinunua mboga. Kiuhalisia ile mboga ilikuzwa kwa dawa  hivyo kubadili ladha kabisa.

Mbali na kwamba watu duniani wanategemea mazao toka shambani, ni vema kuzalisha mazao salama kwaajili ya afya zetu.  Kilimo hai ndio njia sahihi kwani njia hii inazalisha chakula salama wakati wote wa maisha yako.

Bw. Axwesso anasema kuwa, babu zetu walitumia njia za asili kuzalisha chakula hivyo, magonjwa kama kansa na mengineyo hayakuepo kama ilivyo sasa.

Unaanzaje kilimo hai

Kwanza kabisa nimetafuta elimu ya maarifa na jinsi ya kufanya kilimo hai. Taarifa ya jinsi ya kufanya jambo ni muhimu kwani hii imeniwezesha kujua jinsi ya kupanga kilimo hiki, malighafi nilizonazo na zinazohitajika kufanya kilimo hai ikiwa ni pamoja na eneo.

“Kwa sasa ninaandaa shamba tayari kwaajili ya kulima kwani nilipata mafunzo katika jarida la Mkulima Mbunifu kuniwezesha kufanya kwa vitendo. Ninategemea kuendelea kupata ushauri wa moja kwa moja kupitia Mkulima Mbunifu”kwani jarida pekee halitoshi nitapenda kutembelewa ili nikaguliwe.

Ninapenda kufanya kilimo cha pilipili hoo, kwani inasoko hapa wilayani karatu.  Nimeotesha miche, nimeandaa mirija ya umwagiliaji wa matone kwakua eneo hili kuna changamoto ya maji.   Hivyo, nimeandaa nyumba kitalu ya ukubwa wa mita 15 kwa mita 8 na hii ni baada ya kupata mafunzo ya kilimo hai. Nitatumia matandazo kutokana na uhaba wa maji.

Kwakua nimepata elimu ya utengenezaji wa mboji, na nimepata elimu ya kutengeneza dawa za kibaiolojia za asili kwaajili ya kurutubisha udongo na pia kudhibiti wadudu wasumbufu wa mazao.

Je unafikiri kuna changamoto katika kilimo hai

Bw. Axwesso anaeleza kuwa, changamoto  haikosekani kwa aina yoyote ya mradi.  Kutokana na uzoefu wangu, kwakua watu wengi wanafanya kilimo cha kawaida, ni vigumu wao kuamini katika kilimo hai na hivyo sidhani kama kutakua na utofauti wa bei kati ya bidhaa nitakazo zalisha na zile watazalisha wengine.

Hivyo elimu ya kilimo hai bado inahitajika ili kuamasisha watu kwani ni muhimu kutanguliza afya kwanza kwa kua hii ndio chachu ya nguvu kazi itakayoleta mabadiliko kiuchumi.

Hata hivyo, tayari ninaufahamu sitakata tamaa na ninaimani kutakuepo na wale watapenda kuiga. Ninaomba Mkulima Mbunifu msiniache njiani nikihitaji ushauri kwani elimu hii ya bure mnayoitoa sio kila mtu anatoa bure.

Wito kwa Mkulima Mbunifu

Nashukuru sana Mkulima mbunifu kwani imekuwa chachu na imenifungua macho na kunipa msukumo zaidi wa kuanza kujikita katika uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai.

Asante pia kunitembelea pamoja na kwamba bado sikua na chochote shambani nipo katia hatua za maandalizi karibuni tena.

 

 

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *