Majivu yana kiwango cha wastani wa madini kwa mgawanyiko tofauti, potasiamu 5% – 7%, kalishamu 25% – 50%, fosiforasi 1.5% – 2% na madini mengine kwa kiasi kidogo. Pia mabaki ya chenga za mkaa kwenye majivu yanasaidia kunyonya baadhi ya sumu kwenye ardhi.

Matumizi
Tumia kiasi cha kilo 2.5 mpaka 5 kitumike kwenye eneo la mita za mraba 33 au futi 100 za mraba, na majivu yamwagwe wiki 3 – 4 kabla ya kupanda kitu chochote ardhini.
Madhara
Kila kitu kikitumiwa zaidi ya kiasi kina madhara na majivu pia yana madhara kwenye udongo kwa sababu yana hali ya kuwa alkaline zaidi (10 – 12 pH) kwa sababu baadhi ya mchanganyiko wake hauyeyuki kwenye maji.
Endapo utahitaji kuongezea kwenye mimea yenye upungufu wa madini kama fosforasi na potasiamu basi hakikisha majivu hayagusi mashina kwani yanaweza kuuungua hasa kama mimea ni michanga.
Pia majivu yana kiasi kidogo sana cha naitrojeni ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya mmea wowote ule, kwa hiyo hakikisha pia unatumia vyanzo vingine kwa ajili ya naitrojeni. Mimea jamii ya mikunde inafaa zaidi.





Asante nimejifunza vzr matumizi ya majivu
Habari,
Karibu sana Mkulima Mbunifu. Tunafurahi kusikia kuwa umejifunza kupitia makala ya majivu na sasa umefahamu umuhimu na matumizi ya majivu shambani.
Karibu sana Mkulima Mbunifu
Shamba langu Lina chanzo la maji ya chumvi na natakuotesha mazao matunda kama parachichi na maembe pamoja na mbogamboga.
Naomba ushauri nafanyeje
Habari karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kutufuatilia na kusoma makala zetu.Maji ya chumvi kwa ujumla hayafai kuoteshea au kumwagilia mimea ya matunda kwa sababu chumvi nyingi huzuia mizizi kufyonza maji na virutubisho, jambo linaloweza kusababisha mmea kukauka na kufa