Wakulima wanaowekeza kwenye mradi wa kuku, hupata hasara pale ambapo hawatunzi mayai ipasavyo. Mayai ni bidhaa hafifu na inayoharibika kwa haraka, hivyo, ni lazima ishikwe kwa uangalifu na kutunzwa vizuri baada ya kutagwa ili yasivunjike au kuharibika. Watu wengi wanaonunua mayai kutoka dukani watatambua mara moja kuwa mayai hayo yamevunjika au yameoza. Tatizo hili linaweza kutokana na utunzaji na uhifadhi…
Mifugo
Wanafunzi wa shule ya msingi kioga nao hawako nyuma katika kilimo
Ni miaka tisa sasa tangu kuanzishwa kwa jarida la Mkulima Mbunifu likiwa limejikita katika kutoa elimu kuhusu kilimo, ufugaji, pamoja na kilimobiashara kwa lengo la kusaidia jamii kujikimu kimaisha. Jarida hili, limeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, katika kufikisha elimu kwa wadau mbalimbali na kuonesha fursa nyingi zilizopo kwenye kilimo na ufugaji hasa katika kilimo hai. Mkulima Mbunifu pia limewafikia wanafunzi…
Wanafunzi washirikishwe katika masuala ya kilimo
Shule ya Sekondari Shambalai ‘‘Tuna furaha sana kukutana na Mkulima Mbunifu katika utoaji wa elimu kwani tuna bustani yetu tuliyoianzisha kwa msaada wa mwalimu mkuu, na tumeshindwa kuiendeleza kwa muda mrefu sasa kulingana na kuwa kila tulichokuwa tukijaribu kuotesha tulikosa mavuno lakini jarida hili limetupa nguvu ya kuanza kwa upya.’’ Hayo ni maneno ya mmoja wa wanafunzi wa shule hii…
Ufugaji wa Sungura: Aina mpya ya ujasiriamali wenye tija kwa mfugaji
Kabla hujaamua kufuga sungura hakikisha ya kwamba umejitoa na unamuda wa kuwahudumia wanyama hawa. Ufugaji wa sungura si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa. Sungura wanahitaji uangalizi hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira mabaya na machafu. Mabanda Kuna aina mbili ya mabanda ya kufugia: • Kwanza ni mabanda ya kufugia ndani muda…
Punda anahitaji kutunzwa kama mifugo mingine
Punda ni mnyama anayefugwa na wengi lengo likiwa kutumika kutoa msaada wa nguvu kazi nyumbani hasa kwa kuwa njia nzuri ya kubebea mizigo. Mnyama huyu ambaye hutumiwa hasa na kina mama na watoto wa jamii ya kimasai na nyinginezo kwa ajili ya kubebea maji, kuni, majani, kupelekea mizigo sokoni na shughuli zote zile za nyumbani amekuwa hana thamani kama waliyonayo…
Chokaa au majivu huweza kuangamizi kiwavijeshi vamizi
Wakulima walio wengi katika mikoa mbalimbali hapa nchini wamekuwa wakisumbuliwa sana na kiwavijeshi vamizi, mdudu ambaye husababisha hasara kubwa kwa wakulima hasa wa mahindi kwani hupoteza maelfu ya hekari za mazao endapo watavamiwa na mdudu huyu. Kuna mbinu mbalimbali za kudhibiti mdudu huyu kama vilekufanya kilimo bora mfano kupanda kwa wakati, matumizi ya mbegu kinzani (tolerant/resistant varieties), matumizi ya viumbe…
Dume bora ni chanzo cha uzalishaji bora
Unapojipanga kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe kwa ajili ya uzalishaji wa maziwa au nyama, jambo la msingi ni kuhakikisha ni aina gani ya ng’ombe utachagua/utanunua au utatumia katika uzalishaji. Aina hii ya ng’ombe pia pamoja na kuwa utanunua lakini hutokana na dume bora hivyo ni jambo la msingi sana kujua aina ya uzalishaji wako umetokana na dume mwenye ubora.…
Ongeza lishe kwa kutumia njia rahisi za ufugaji samaki
Ufugaji wa samaki ni moja ya shughuli ambazo hivi karibuni imejipatia umaarufu mkubwa sana miongoni mwa wafugaji. Kazi hii imekuwa ikifanywa na makundi mbalimbali bila kujali wanafanya shughuli gani nyingine. Kutokana na uhitaji mkubwa wa lishe inayotokana na samaki, kumekuwa na aina mbalimbali za ugunduzi unaosaidia ufugaji wa samaki kwa njia rahisi. Katika makala hii tutaeleza ugunduzi mpya wa kutengeneza…
Utaratibu wa kinga za magonjwa kwenye kuku wa asili/kienyeji
Kuku wa kienyeji nao wanahitaji kupata chanjo ya magonjwa na kwa utaratibu unaofaa. Ugonjwa Jinsi ya kuudhibiti Mdondo/kideri (Newcastle disease) Kama tete lilichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki tatu za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hawa dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18. Vifaranga ambao historia…
Uzalishaji wa minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki
Minyoo redworms ni chakula kizuri sana kwa kuku, bata na samaki kwani minyoo wana protini nyingi sana na kuku wakipewa au kulishia minyoo wanakua kwa haraka sana na huwafanya kuwa na maumbile makubwa sana (wanakuwa na uzito mkubwa pia). Kutengeneza minyoo ya chakula ni utaratibu wa kuzalisha minyoo kwa ajili ya kuku, bata na samaki. Namna ya kuzalisha Chukua mavi…