Mifugo

- Kuku, Mifugo

Maswali ya wafugaji wa kuku na majibu ya wataalamu

Swali: Endapo nitachanja kuku wangu dhidi ya mdondo lakini jirani zangu hawakuchanja kuku wao, je kuku wangu hawataathirika na ugonjwa unapotokea kwa majirani? Jibu: Kinga itokanayo na chanjo hufikia kiwango cha juu kabisa siku ya 14 na endapo ugonjwa utafika kwa jirani yako wakati kuku wako wamekwisha fikia kiwango kizuri cha kinga basi ni dhahiri kwamba hawataathirika kwa ugonjwa huo.…

Soma Zaidi

- mbuzi, Mifugo, Ng'ombe

Matatizo yanayoweza kumpata ng’ombe baada ya kuzaa

Mara nyingine ng’ombe anapozaa, huweza kupatwa na matatizo machache kama vile kizazi kutoka nje, kondo la nyuma kushindwa kutoka na hata wakati mwingine kupooza miguu na kushindwa kusimama. Kushindwa kutoka kwa kondo la nyuma Kwa kawaida mara baada ya kuzaa, kondo la nyuma pamoja na majimaji yaliyobakia kwenye tumbo la uzazi hutolewa nje kutokana na msukumo wa misuli ya tumbo.…

Soma Zaidi

- Kuku, Mifugo

Ni rahisi sana kutunza kuku wa kienyeji na kupata faida kubwa

Unaweza kutunza kuku wa kienyeji na ukawa na kipato cha uhakika, pamoja na lishe nzuri kwa ajili ya familia. Ulishaji: Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika sehemu safi au kwa kutumia vyombo vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia kuku.…

Soma Zaidi

- Kuku, Mifugo

MATUNZO SAHIHI YA VIFARANGA VYA KUKU

Ni muhimu mfugaji kufahamu kuwa kifaranga wa leo ndiye kuku wa kesho atakaesababisha mafanikio yake na kufanya maisha yasonge mbele bila kikwazo. Ufugaji wa kuku ni moja ya shughuli ambayo imejipatia umaarufu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wakulima na hata wanaofanya shughuli nyinginezo tofauti na ufugaji peke yake. Ili kuwa na mafanikio ya uhakika ni muhimu kwa mfugaji kuzingatia…

Soma Zaidi

- Mifugo, Ng'ombe

Namna ya kuzuia vimelea kwa mifugo

Minyoo ya ndani ya mwili na hasa ile inayoishi kwenye maini pamoja na ile ya mviringo huathiri sana afya za wanyama wa dogo kama ndama na kwa ujumla husababisha udhaifu wa mwili, ukosefu wa nguvu, ukuaji duni na hatimaye vifo vya maelfu ya mifugo ya wafugaji wadodgowadogo kila mwaka. Hali hii ni ya kusikitisha kwasababu mifugo hiyo ingeweza kuokolewa kwa…

Soma Zaidi

- Kuku, Mifugo

Msimu huu wa mvua na baridi kali, hakikisha unawachanja kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali

Watu wengi wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa kuku bila kuzingatia kanuni bora za utekelezaji wa mradi huo. Moja ya mambo ambayo wafugaji mara nyingi husahau kuzingatia ni utoaji wa chanjo sahihi na kwa muda muafaka. Ni muhimu kufahamu mambo unayotakiwa kuzingatia katika kuwapatia kuku chanjo. Wakati wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya magonjwa,…

Soma Zaidi

- Mifugo

Tengeneza chakula kwa ajili ya nguruwe kwa kutumia comfrei na upupu

Ni kwa namna gani ninaweza kutengeneza chakula cha nguruwe kwa njia kutumia comfrei na upupu? Resheni ya chakula inahusiana moja kwa moja na ulishaji. Hili ni jumuiko la aina mbalimbali ya vyakula vinavyotumika kwa malisho, ikionesha ni kiasi gani cha kila aina ya lishe iliyopo kimetumika ili kuwa na chakula bora. Hii inamaanisha kuwa resheni inakamilika inapokuwa na aina zote…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo, Nyuki, Nyuki

Ikiwa bado tuko kwenye wiki siku ya nyuki, fahamu wadudu wanao athiri uzalishaji wa asali

Siafu Siafu ni miongoni mwa wadudu wanaoshambulia nyuki wanaozalisha asali. Ni wadudu wapole wasiokuwa na shida lakini huvamia mzinga na kuwauwa nyuki. Kutokana na uharibifu huo, humuumiza na kumvunja moyo mfugaji, na mara nyingine wanaweza kuuma na kusababisha maumivu. Kuweka mizinga sehemu yenye siafu inaweza kusababisha utunzaji kuwa mgumu. Kukiwa na kundi dhaifu la nyuki linaweza kusababisha nyuki kuondoka, na…

Soma Zaidi

- mbuzi, Mifugo

Ni hatari kumfunga mbuzi kamba shingoni

Ni dhahiri kuwa wafugaji wengi wana bidii sana na kuwa na matumaini makubwa kutokana na kazi zao. Hari ya kuwa na uzalishaji mzuri kutokana na mifugo yao pia ni dhahiri. Pamoja na hari hiyo, wafugaji wengi wamekuwa hawazingatii kanuni bora za ufugaji na utunzaji wa mifugo yao. Mbuzi wa aina zote wawe wa kisasa au kienyeji wana tabia ya kupenda…

Soma Zaidi