Ng’ombe ni mifugo ambayo inategemewa sana na wananchi walio wengi hapa nchini. Kuna aina tatu za ng’ombe wafugwao hapa nchini ambayo ni ng’ombe wa kisasa, kienyeji, na machotara. Zifuatazo ni faida zipatikanazo na ufugaji wa ng’ombe Chakula kama vile maziwa na nyama Mbolea Ngozi ambayo hutumika kama malighafi kutengeneza, viatu, mikanda, mikoba, nguo na vitanda Kujipatia pesa, pia ni akiba…
Mifugo
Chakula rahisi kwa utunzaji wa nguruwe wadogo wanaokuwa
Nguruwe ni mnyama anaeweza kuishi sehemu za vijijini kwani mijini kule wengi huwa hawapendelei sanaana ufugaji huu. Nguruwe hubeba mimba kwa muda wa miezi mitatu na wiki mbili. Ili kuwa na ufanisi na kwa gharama ndogo, mfugaji anapaswa kuzingatia matunzo na kufahamu njia sahihi za ulishaji wa nguruwe wadogo, ili waweze kukua kwa haraka. Mfugaji anaweza kutumia malighafi zifuatazo ili…
Ni muhimu kuzingatia ubora wa chakula cha kuku kabla ya kununua na kulisha
Ili kuku waweze kuishi, kukua na kuleta matokeo chanya ni lazima wale chakula kingi chenye ubora unaotakiwa. Uwingi na ubora wa chakula cha kuku ni lazima uzingatie makundi ya chakula ambazo ni, vyakula vya kutia nguvu, kujenga mwili, kuimarisha mifupa, kulinda mwili pamoja na maji. Vyakula vya kutia nguvu Vyakula vya kutia nguvu vinaweza kuwekwa katika makundi matatu; Kundi la…
Namna ya kuandaa udongo kwa ajili ya kusia mbegu
Wakulima wengi hawaelewi ubora na umuhimu wa kuandaa udongo maalumu kwa ajili ya kusia mbegu za mazao mbalimbali kabla ya kuzipeleka shambani hasa mazao ya bustani. Si kila udongo unafaa kwa ajili ya kusia mbegu. Kuna udongo maalumu unaostahili kutumika kwa ajili ya kusia miche, ambao mkulima yeyote anaweza kuutafuta na kuandaa mwenyewe kwa ajili ya matumizi hayo. Bila kutumia…
Ufugaji wa kuku unaweza kumpa mkulima kipato kikubwa
Hii inawezekana ikiwa mfugaji mdogo wa kuku atapanua kiwango na idadi ya kuku anaowafuga. Kuku ni ndege maarufu na ana-yefugwa sana nchini Tanzania. Karibu kaya nyingi zinafuga kuku, kwa ajili ya nyama yake yenye ladha nzuri, mayai, pia ni ishara muhimu ya kitamaduni katika baadhi ya jamii. Kwa nini ni vigumu kuongeza kipato kutokana na ndege huyu mwenye umaarufu mkubwa…
Matumizi ya molases na faida zake kwa uzalishaji wa mazao
Katika kilimo, matumizi ya Molases ni muhimu kwa kuboresha hali ya udongo, kdhibiti wadudu, kuwezesha udongo kuwa na rutuba, kurekebisha hali ya udongo na pia kupunguza matatoizo kwa mimea inayopandikizwa. Matumizi ya Molases husaidia kusafisha mipira ya umwagiliaji. Utafiti unaonyesha kuwa Molases husaidia kuboresha ubora wa udongo. Matumizi na kiasi cha kutumia Kuboresha umbile la udongo molases husaidia kuboresha udongo…
Nyasi aina ya Boma ni chakula kizuri kwa ng’ombe
Nyasi ni rahisi kukua na endapo yatatunzwa vizuri, hukuhakikishia uzalishaji wa hali ya juu wa maziwa. Nchini Tanzania, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya malisho, bado ni dogo ikilinganisha na umuhimu unaoweza kuwepo kwenye uzalishaji wa maziwa kutokana na kuwa na eneo la malisho. Matete na nyasi ni moja ya malisho muhimu, yanayotoa kiasi kikubwa cha malisho kwa ajili ya…
Namna ya kuwavutia nyuki kuingia mzinga mpya
Tatizo kubwa linalowakabili wakulima wanaotaka kuanzisha ufugaji wa nyuki ni mzinga mpya kukaa muda mrefu bila nyuki. Tatizo hili linapotokea ni vizuri kuzingatia yafuatayo; Weka nta kwenye mizinga yako. Weka mizinga yako katika hali ya usafi na kusiwe na wadudu. Nyuki hawapendi mzinga mchafu. Hakikisha hakuna siafu wala panya wanaoishi kwenye mzinga. Ning’iniza mzinga msimu ambao kuna makundi mengi ya…
Ndege wenye manufaa kwa mkulima
Ufugaji wa bata na bata mzinga hauonekana kuwa si kazi yenye manufaa sana kwa mfugaji. Ingawa ndege hawa ni rahisi sana kuwalisha kwa kuwa huwa wanakula majani na magugu ya aina nyingi. Bata mzinga wanaweza kutumika kama walinzi kwa kuwa ni wakali sana, mtu mgeni anapoingia katika eneo lao. Bata hula wadudu kama konokono na babaje kwenye vitalu vya mbegu.…
Mambo msingi ya kuzingatiwa katika utunzaji bora wa mazingira
Mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa ni Dhahiri na hatarishi kwa Maisha ya binadamu kila uchwao. Hii inatokana na uduni katika kutunza mazingira yetu, ambayo kwa kiasi kikubwa yanatawaliwa na miti. Ili kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ni muhimu kahakikisha kuwa katika mazingita yetu, imepandwa miti ya kutosha na kutunzwa vyema. Yafuatayo ni mambo muhimu katika upandaji…