Mifugo

- Mifugo

Kupe wanahatarisha afya ya mifugo

Kupe ni wadudu wanaoonekana kuwa ni wadogo lakini wanaweza kusababisha kushuka kwa uchumi wa wafugaji kwa kiwango cha juu endapo hawatadhibitiwa kwa wakati. Pamoja na kuwepo kwa aina mbalimbali za kupe, kupe wa rangi ya kahawia ni wabaya zaidi. Hii ni kwa sababu kupe wanabeba vimelea vinavyosababisha homa ya ndigana (East Coast Fever). Kupe wanaonekana kuwa wababe wa maisha kutokana…

Soma Zaidi

- Mifugo

Zuia ndama kuhara kutokana na unyweshaji maziwa

Muda wa kumlisha au kumnywesha ndama unatakiwa uwe sawa kila siku na joto la maziwa lisibadilike, liwe hilohilo kila siku. Aidha, unyweshaji wa maziwa sharti ufanywe katika hali ya usafi ili kuondoa uwezekano wa ndama kuharisha au kupata ugonjwa wa pneumonia na magonjwa mengine. Tahadhari za kuchukua wakati wa kumnywesha ndama Hakikisha maziwa unayomlisha ndama hayajazidi kiwango kinachostahili ndama kulisha…

Soma Zaidi

- Mifugo

Namna ya kupata faida kutokana na uzalishaji wa maziwa

Wafugaji huzalisha maziwa na kuyauza moja kwa moja sokoni na mara nyingi maziwa hayo huweza kusalia kwa kukosa wanunuzi. Maziwa hayo kutumika kwa matumizi ya nyumbani na wakati mwingine huweza kuharibika na kupelekea kumwaga. Hii imekuwa changamoto na kusababisha hasara kwa wafugaji.  Katika makala mbalimbali zilizopita tumejaribu kueleza namna ya kuzalisha maziwa kwa wingi. Pia jinsi ya kufanya usindikaji. Kuna…

Soma Zaidi

- Mifugo

Umuhimu wa maji katika mnyororo wa ongezeko la thamani

Kwa muda mrefu sasa sehemu kubwa ya nchi ya Tanzania imekumbwa na ukame. Hali hii imefifisha kwa kiasi kikubwa shughuli za wakulima na wafugaji kwa kuwa asilimia kubwa hutegemea mvua. Kama wasemavyo maji ni uhai sio kwa binadamu peke yake, hata kwa wanyama na mimea pia.  Kwa mkulima kutegemea mvua hawezi kuwa na kilimo cha kibiashara kwa kuwa hana uhakika…

Soma Zaidi

- Mifugo

Chukua hatua kuboresha udongo ili kuinua kilimo hai

Uelewa wa mahitaji ya mimea humwezesha mkulima kuchukua hatua kuimarisha udongo ili kulisha mimea na kuongeza mavuno. Katika kilimo, rutuba kwenye udongo na upatikanaji wa maji ni mambo muhimu ya kuzingatia kwani huweza kuathiri uzalishaji, usalama wa chakula, na wa mazingira. Hivyo basi, mkulima anapotunza udongo anatarajia kwamba udongo huo utaweza kulisha mimea na kuzalisha mimea, inayoweza kustahimili magonjwa, athari…

Soma Zaidi

- Mifugo

Athari za ukame kwa mifugo na namna ya kukabiliana nayo

Ukosefu wa mvua umeathiri wafugaji na mifugo yao kwani maeneo ya malisho yanakauka na maji hayapatikani. Hii imepelekea maeneo mengi ya malisho kukauka na pia wafugaji wengi kuhama na mifugo yao ili kutafuta maeneo yenye maji na malisho.   Athari za ukame zimeonekana wazi katika maeneo mengi ya wafugaji. Mifugo kukonda, afya za mifugo imezidi kuwa mbaya kutokana ukosefu wa…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Mifugo

Biovision Foundation visit to Tanzania [Mkulima Mbunifu]

MkM project had an opportunity to meet with Biovision foundation, the donors of FCP program [Dr. Franklin Eyhorn [Executive Director] and [Martin Schmid] Co-Head Development Projects on 14th and 15th March 2022. The team selected farmer groups and partners to visit [within Arusha and Kilimanjaro] to allow for Biovision Foundation  explore the project engagement with different partners and how useful has been…

Soma Zaidi

- Mifugo

Fahamu maandalizi muhimu kabla ya nguruwe kuzaa

Nguruwe wanaozaa kwa mara ya kwanza wanaweza kupelekwa kwenye nyumba ya kuzalia masaa machache kwa siku kutoka siku kumi kabla ya siku ya kuzaa ili waweze kuzoea mazingira. Mara nyingi tumekuwa na makala zinazoelezea ufugaji wa nguruwe katika nyanja tofauti, ikiwa ni pamoja na aina, matunzo na magonjwa ya nguruwe na hata bidhaa zinazotokana na nguruwe na usindikaji wake. Katika…

Soma Zaidi

- Mifugo

Kinga dhidi ya magonjwa

Magonjwa yaenezwayo na kupe Ndigana kali, ndigana baridi, kukojoa damu na moyo kujaa maji. Kinga:  Ogesha wanyama wako  kwa  kutumia dawa ya kuua kupe mara moja kwa wiki. Magonjwa yaenezwayo na mbung’o Ndorobo   ni   ugonjwa   mkuu   uletwao   na mbung’o Kinga:  Wachanje ng’ombe kwa kutumia dawa iitwayo samorini kila baada ya miezi mitatu. Magonjwa yasababishwayo na virusi Ugonjwa wa midomo na…

Soma Zaidi