Ufugaji wa samaki umeendelea kukua hata katika maeneo ambayo hakuna ziwa, bahari, bwana na kusaidia jamii kujipatia kipato kinachokidhi mahitaji muhimu, na hata kufanya maendeleo binafsi. Mafanikio ya ufugaji wa Samaki ni kutokana na uhakika mkubwa wa soko. Katika Makala hii Mkulima Mbunifu inakuletea Ufugaji mesto wa Kuku, Samaki na uzalishaji wa mboga katika mbinu rahisi. Ufugaji wa mesto ni…
Mazingira
Je, wajua kuwa unaweza kulima mboga kwenye matairi na ukafanikiwa?
Hupunguza uchafuzi wa mazingira Kila siku watumiaji wa vyombo vya usafiri hubadilisha matairi. Mbali na kuwa matairi hutumika kutengeneza vitu kama viatu, mipini ya mapanga n.k, pia matairi yanaweza kutumiwa katika kilimo cha mbogamboga na matunda badala ya kuchoma matairi na kuzalisha kemikali zenye sumu kwa binadamu. Ni rahisi kutumia Ukilinganisha na kulima kwa kutengeneza matuta ya mbao au mawe,…
MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE; TUAMBIE UMEJIFUNZA NINI? JE, UNAKWAMA WAPI?
Kama umeweza kuhudhuria maonyesho ya wakulima Nanenane katika kanda yeyote, njoo utuambie ni kipi umejifunza kipya, au ni maarifa ama ujuzi gani umeongeza? Je, ni wapi unakwama au changamoto uliyonayo ni ipi? Njoo tusemezane ewe mkulima!!!!!!!!!!!!!
Utunzaji wa udongo kwa ajili ya kilimo hai
Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo. Utunzaji wa udongo unategemeana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya kibiolojia. Kazi kubwa ya baadhi ya viumbe hai waliomo kwenye udongo, ni kumeng’enya mabaki ya mimea na viumbe hai wengine. Mtiririko huu hufanya uwepo wa nguvu, virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa pamoja…
HIVI UKISIKIA WAKULIMA WAKISEMA MBEGU UNAFIKIRIJE? AMA KWA UFAHAMU WAKO MBEGU NI NINI
Mbegu ni nini? Mbegu ni sehemu ya mmea ambayo ina uwezo wa kuota na kutoa mmea mpya. Kuna makundi makuu mawili ya mbegu tunayoyazungumzia katika kilimo ambayo ni punje na shina/ mizizi. Punje Hizi ni mbegu za nafaka au za matunda, ambazo huzalishwa kwa uchavushaji. Kawaida huwa na kiini na chakula chake huhifadhiwa ndani ya ganda gumu la mbegu. Mfano,…
Wakulima vinara wa MkM ni mabalozi wa kilimo endelevu
Nchini Tanzania, kilimo si kazi tu, ni sehemu ya maisha ya kila siku. Kilimo kinatoa ajira kwa takribani asilimia 80 ya Watanzania na kuchangia takribani asilimia 30 ya pato la taifa. Kiasi kikubwa cha chakula chetu kinazalishwa na wakulima wadogo. Hata hivyo, licha ya mchango wao mkubwa, wakulima hawa hukumbwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na udongo kupoteza rutuba,…
Unaweza kutengeneza mbolea ya mboji kwa njia rahisi
Zipo aina nyingi za takataka zin-azoweza kutumika kwa ajili ya kuzalisha mbolea ya mboji kama vile mabaki ya malisho, unga wa maranda unaotokana na shughuli za useremala, majivu na masalia ya ziada baada ya kuvuna mazao shambani. Kwa kutengeneza mboji, kiasi cha mbolea kitakachopelekwa shambani kitaongezeka kwani samadi itachanganywa na takataka zingine na kuozeshwa. Ni jambo zuri zaidi kama mkulima…
Mvua zinaelekea ukingoni: Panda miti kwa ajili ya mazingira
Kwa mara nyingine tena, wakulima katika maeneo mbalimbali hapa nchini, wanapanda mazao na hata wengine kukazana kufanya palizi ili kutumia mvua ambazo zimenyesha sehemu mbalimbali. Mbali na kupanda mazao, shughuli nyingine muhimu ambayo wakulima wanaweza kujihusisha nayo katika msimu huu wa mvua ni upandaji wa miti. Ni jukumu la kila mkulima kuhakikisha kuwa shamba lake lina miti mipya kila mwaka.…
Matumizi ya mabaki ya mimea na wanyama katika kurutubisha udongo na kupelekea uzalishaji bora wa mazao
Je, unafahamu kuwa unatakiwa kujua sifa za udongo ulio katika shamba lako na changamoto zake? Je, udongo una upungufu wa naitrojeni? Je, una upungufu wa fosiforasi? Je, kuna uwepo wa mabaki ya miti au wanyama ya kutosha? Ikiwezekana, udongo huo upimwe na mtaalamu au afisa kilimo ili kuonyesha kwa usahihi udongo una mapungufu ya virutubishi vipi na nini kifanyike ili…
Rutuba ya udongo ndiyo msingi wa kilimo hai
Kwa muda mrefu sasa tumekuwa mstari wa mbele katika kuzungumzia na kuhimiza uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai, ikiwa ni moja ya nguzo za kilimo endelevu. Katika makala zote zilizochapishwa katika jarida hili pamoja na machapisho mengine yanayotolewa na Mkulima Mbunifu, tumehimiza pia matumizi sahihi ya dawa za asili na mbolea za asili. Hii inatokana na ukweli kwamba, huwezi kusema…







