Kilimo

- Kilimo

Kula vizuri upate nguvu ya kufanya kazi

Chakula na lishe ni muhimu kwa afya ya binadamu, hasa wakulima wanaotumia nguvu kazi nyingi shambani. Wakati mwingi wakulima wanazalisha na kuuza, wanasahau kwamba pia wao wanahitaji lishe bora ili kuwa na nguvu ya kuendelea kufanya kazi na kuhakikisha usalama wa chakula. Ili kuwa na lishe bora tunapaswa kula mlo kamili na wa kutosha. Unapotafuta na kutayarisha chakula, zingatia makundi…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara

Kilimo ikolojia kimeniongezea tija katika uzalishaji

Mbegu bora ya asili huchangia pakubwa katika usalama wa chakula na lishe kwa familia na jamii kwa ujumla. Hii inaambatana na matumizi ya mbinu bora za kilimo endelevu ili kumhakikishia mkulima uzalishaji wa juu nyakati zote na kwa muda mrefu. “Kabla ya kushiriki katika mradi wa CROPS4HD (Mazao yenye afya yasiyopewa kipaumbele), Mama Regina Mrope, kutoka Kijiji cha Mpindimbi, Masasi,…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara

Siku ya chakula duniani October 2024

Siku ya chakula duniani ni maadhimisho ambayo yaliwaleta pamoja wadau wa kilimo na chakula kutoka sehemu mbalimbali. Hata hivyo siku hii ilikuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora.…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo

Masomo kupitia jarida ni suluhisho la changamoto za wakulima

“Mimi ni mkulima na mfugaji, Ninazalisha kwa misingi ya kilimo ikolojia. Situmii pembejeo sumu za viwandani kuanzia ninapootesha zao husika au kuanza uzalishaji wa mifugo yangu mpaka ninapovuna, kuhifadhi na kuuza mazao yangu. Ninafanya uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali kama vile ndizi, kahawa, njugu, maharage, mahindi, mbogamboga, na pia ninafanya ufugaji wa kuku pamoja na mbuzi.’’ Hayo ni maneo…

Soma Zaidi

- Kilimo

Mbolea ya BOKASHI inapambana na mbadiliko ya tabianchi

Kutana na mkulima Giranta Giranta, kutoka kijiji cha Bungurere, kata ya Muriba, wilaya ya Tarime, mkoani Mara. Tulizungumza naye kuhusu mbinu za kilimo endelevu anazotumia shambani mwake. “Najishughulisha na kilimo mseto ambacho imenipa tija kubwa kwenye uzalishaji wa mahindi na maharage. Ninashirikiana na wakulima katika eneo langu na pamoja tumeansiha kikundi kinachijulikana kama Tabukomu”. Umekumbana na changamoto gani? Rutuba ya…

Soma Zaidi

- Kilimo

Nimesoma MkM na kupiga hatua katika uzalishaji

Wakulima wengi wamenufaika kutokana na elimu ya bure inayotolewa kupitia jarida hili. Wanasoma na kufanyia majaribio mbinu mbalimbali zinazosimuliwa, uzoefu wa wakulima na watalamu wa kilimo endelevu. “Tangu mwaka wa 2012, nimekuwa msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu (MkM) na nimepiga hatua kubwa katika uzalishaji”, hivyo ndivyo alivyoanza kujitanabaisha Bw. Godwin Kimaro kutoka Karansi, mkoani Kilimanjaro, alipotembelewa na mwandishi wa…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara

Zalisha kwa malengo ili kupanua kilimo biashara

Kama kawaida jarida hili linatoa wito kwa wakulima kuanzisha na kujenga kilimo kuwa biashara inayoweza kuleta faida na kukidhi mahitaji ya kila siku hapo nyumbani. Hata hivyo, imekuwa ni kawaida kwa wakulima wengi kufanya shughuli zao bila kufanya maandalizi thabiti, na bila kuwa na mipango itakayowawezesha kupanua uzalishaji na kuifanya kuwa endelevu. Swala hili ni kikwazo kikubwa sana kwa sababu…

Soma Zaidi

- Kilimo

Tushirikiane kutafuta masoko na tutumie bidhaa za kilimo hai

Kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, ni wazi kuwa shughuli za kilimo hai zimeshika kasi, huku kukiwa na ongezeko la wazalishaji wa bidhaa za kilimo hai. Hili ni jambo jema sana kwa kuwa waswahili wanasema taratibu ndiyo mwenda, na kidogo kidogo hujaza kibaba. Na hapa taratibu tunaona mwanga wa dunia kurudi katika hali yake ya uasili, ya awali…

Soma Zaidi

- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Mazingira, Mifugo

MWENENDO WA MVUA MKOA WA ARUSHA

Ndugu Mkulima, kama tunavyofahamu huu ni msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini, ni muhimu kupata na kufahamu taarifa za mwenendo mzima wa msimu, nini kifanyike au kisifanyike katika uzalishaji na mwenendo wa maisha kwa ujumla. Tafadhali soma kwa kubonyeza hapa chini kupata taarifa kamili kwa mkoa wa Arusha https://www.meteo.go.tz/uploads/publications/sw1724331524-Downscaled%20OND%202024%20Rainfall%20Season%20Outlook%20(Swahili)%20for%20Arusha%20Region%20and%20Districts.pdf

- Kilimo

Bei za mazao makuu ya chakula

Kama ilivyo ada tunawaletea habari za taarifa za mazao makuu ya chakula katika mikoa mbalimbali hapa nchini kama ilivyotayarishwa na wizara ya kilimo. Tafadhali bonyeza hapa kusoma zaidi https://www.viwanda.go.tz/uploads/documents/sw-1731069832-Wholesale%20price%206th%20November,%202024..pdf