Kuna faida nyingi zinazotokana na matumizi ya mbolea za asili kama mboji na nyinginezo. Mbolea asili hutokana na kuoza kwa vitu vyenye uhai kama vile majani, miti na mabaki ya vyakula. Vitu hivi vinapooza hugeuka na kutengeneza virutubisho ambavyo husaidia kurutubisha udongo na kupunguza gharama kwa mkulima kwa kuwa vitu vinavvyotumika ni vya asili. Mbolea ya kukuzia mimea inatokana na…
Kilimo
Anzisha miradi tofauti kuongeza pato
Kuna msemo mmoja maarufu sana wa kiswahili usemao, kidole kimoja hakivunji chawa. Hii inamaanisha kuwa endapo unategemea jambo moja tu, inakuwa ni vigumu sana kutimiza malengo yako au kufanikiwa kufanya jambo fulani. Hii ni changamoto kwako mkulima kuhakikisha kuwa unatumia nafasi uliyo nayo ipasavyo. Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unaanzisha miradi ya aina mbalimbali kulingana na uwezo wako. Hiyo itakuwezesha…
Jifunze kusindika kiazi sukari/ kiazi chekundu
(Beetroot) Kiazi sukari ama hufahamika kama kiazi chekundu ni zao jamii ya mizizi. Kiazi sukari hutumika kama dawa kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali kama kuvimbiwa, majeraha, pamoja na matatizo mbalimbali ya Ngozi (mizizi ndiyo hutumika). Hadi kufikia karne ya 16, zao hili lilikuwa tayari limekwishapata umaarufu hasa katika Amerika ya Kati na Ulaya ya Mashariki na baadaye kupokelewa katika…
Jifunze kusindika bamia
Bamia ni aina ya tunda mboga lenye utajiri wa virutubishi ambavyo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu hasa katika usagaji wa chakula. Faida za ulaji wa bamia Umeng’enyaji na uwekaji sawa wa mfumo wa sukari mwilini. Kulainisha choo na kuzuia kuvimbiwa. Kuondoa lehemu katika mishipa ya damu kwenye mwili. Kuwepo kwa wingi wa virutubisho vya protini ambavyo vinahitajika katika…
Namna ya kusindika boga lishe
Boga lishe ni miongoni mwa vyakula vilivyopo katika kundi la mimea ya Cucurbitaceae au familia ya squash. Boga hili huwa na umbo la kibuyu na rangi yake huwa ni ya kijani mpauko kabla ya kukomaa na likikomaa huwa na rangi ya chungwa kwa nje na ndani. Kwa sehemu ya nje, gamba lake huwa ngumu lakini likipikwa hulainika. Ndani ya mboga…
Jifunze kilimo cha mwani na faida zake
Mwani wa bahari si mmea mgeni kwa wakaazi wa maeneo ya pwani. Wengi hukusanya kwa matumizi ya biashara na wachache hujumuisha katika mlo wao. Hivi karibuni, katika mitandao ya kijamii, wataalamu wa lishe wamekua wakishawishi watu kujumuisha mwani katika milo yao, wakisema kuwa mwani una faida nyingi kwa afya. Mwani ni aina ya mimea inayoota na kukua kwenye maji chumvi…
Nimefanikiwa katika kilimo na ufugaji kupitia Jarida la Mkulima Mbunifu
Mimi ni msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu (MkM) toka mwaka 2011, na nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza shughuli zangu za kilimo na ufugaji kwa ufanisi kutokana na elimu inayotolewa na jarida hili. Hayo ni maneno ya Bw. Silvester Gideon Mbulla (63), mkazi wa Kongwa (Hogoro), mkoani Dodoma, ambaye hakusita kuonyesha furaha yake mara tu alipokutana na mwandishi wa jarida…
Thamini na kuendeleza mbegu za asili ili kuleta tija katika kilimo
Mbegu ni pembejeo ya muhimu katika uzalishaji wa mazao. Upatikanaji wa mazao bora hutegemea matumizi ya aina na ubora wa mbegu za mazao husika. Baadhi ya wakulima nchini Tanzania wamesahau matumizi ya mbegu za asili na kujikita zaidi katika mbegu za kisasa. Mbegu ni nini? Mbegu ni sehemu ya mmea ambayo mmea mpya unaweza kuota. Kuna makundi makuu mawili ya…
Sindika mazao mbalimbali kwa ajili chakula na tiba lishe
Kupitia makala mbalimbali katika jarida la Mkulima Mbunifu, tumeweza kutoa elimu juu ya usindikaji wa mazao mbalimbali yatokanayo na wanyama na mimea. Hii ni kwa madhumuni ya kusaidia jamii kujifunza na kufanya kwa vitendo kisha kuongeza pato na kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno. Katika makala hii, tunafundisha namna ya kusindika baadhi ya mazao ambayo yatatumika kama chakula, hivyo…
Nyuzinyuzi ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu
Nyuzinyuzi hupatikana kirahisi kwa familia kwa wakulima. Hii ni pamoja na nafaka zisizokobolewa,njugu karanga, kunde, matunda na mboga. Ni chanzo muhimu cha chakula kwa bakteria chenye faida kwenye utumbo. Inaweza kusaidia kudhibiti uzito na kupunguza hatari kwa ugonjwa wa moyo. Nyuzinyuzi (Roughage) Roughage, pia inajulikana kama nyuzinyuzi, ni sehemu ya wanga ya mimea ambayo haiwezi kumeng’enywa na mwili wa binadamu.…




