Kilimo

- Kilimo

Umuhimu wa udongo kwa uzalishaji wenye tija

Udongo wenye afya ni udongo ulio hai, ambao unazalisha mazao bora na yenye afya. Udongo lazima uwe na minyoo na viumbe vingine. Viumbe hawa hufanya kazi ya kulainisha udongo kwa kuvunjavunja masalia ya majani, mimea na mabua yaliyokufa kisha kubeba masalia hayo hadi chini ya udongo na kuichanganya kisha kuzalisha virutubishi vya kwenye mimea. Viumbe hawa huongeza kasi ya kuoza…

Soma Zaidi

- Kilimo

Ni muhimu kuzingatia soko la mazao kabla ya uzalishaji

Suala la soko ni la msingi na ni la wakati wote, kuanzia kipindi cha utafutaji taarifa ya zao husika, wakati zao likiwa katika hatua ya awali ya uzalishaji na hata linapokuwa tayari kwenda sokoni. Ni muhimu kwa mkulima kutafuta soko la mazao yake ili aweze kuuza kwa bei iliyopo sokoni na ikiwa bei imeshuka kwa ghalfa bila kutarajiwa, aweze kufikiri…

Soma Zaidi

- Kilimo

Dawa za asili

Majivu Weka majivu moja kwa moja kwenye mashina ya mimea michanga baada ya kuotesha ili kuzuia wadudu wakatao mimea kama vile sota (cutworms). Majivu yataonyesha matokeo mazuri endapo yatachanganywa na mafuta ya taa kidogo Pilipili kali Chukua gramu 55 za pilipili kisha katakata Chemsha kwa dakika ishirini kwenye maji lita 5. Chuja kisha ongeza maji lita 5. Dawa hii huua…

Soma Zaidi

- Kilimo

Udhibiti wa magonjwa na wadudu kwa kutumia dawa za asili

Hizi ni dawa zinazotokana na mimea ambayo hupatikana katika maeneo ya wakulima. Matumizi ya dawa hizi ni njia mojawapo ya kuepuka dawa za viwandani ambazo huathiri udongo, mazingira na afya za watu na wanyama. Madawa yasipotengenezwa vizuri na kutumiwa ipasavyo yanaweza yasifanye kazi ipasavyo, hivyo huwa ni vigumu kuwashawishi wakulima kuzitumia. Inashauriwa kutumia dawa hizi kama kinga kabla mashambulizi hayajashamiri…

Soma Zaidi

- Kilimo

Namna ya kutengeneza mbolea ya asili au mbolea hai

Kuna faida nyingi zinazotokana na matumizi ya mbolea za asili kama mboji na nyinginezo. Mbolea asili hutokana na kuoza kwa vitu vyenye uhai kama vile majani, miti na mabaki ya vyakula. Vitu hivi vinapooza hugeuka na kutengeneza virutubisho ambavyo husaidia kurutubisha udongo na kupunguza gharama kwa mkulima kwa kuwa vitu vinavvyotumika ni vya asili. Mbolea ya kukuzia mimea inatokana na…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo

Anzisha miradi tofauti kuongeza pato

Kuna msemo mmoja maarufu sana wa kiswahili usemao, kidole kimoja hakivunji chawa. Hii inamaanisha kuwa endapo unategemea jambo moja tu, inakuwa ni vigumu sana kutimiza malengo yako au kufanikiwa kufanya jambo fulani. Hii ni changamoto kwako mkulima kuhakikisha kuwa unatumia nafasi uliyo nayo ipasavyo. Ni muhimu sana kuhakikisha kuwa unaanzisha miradi ya aina mbalimbali kulingana na uwezo wako. Hiyo itakuwezesha…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara, Usindikaji

Jifunze kusindika kiazi sukari/ kiazi chekundu

(Beetroot) Kiazi sukari ama hufahamika kama kiazi chekundu ni zao jamii ya mizizi. Kiazi sukari hutumika kama dawa kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali kama kuvimbiwa, majeraha, pamoja na matatizo mbalimbali ya Ngozi (mizizi ndiyo hutumika). Hadi kufikia karne ya 16, zao hili lilikuwa tayari limekwishapata umaarufu hasa katika Amerika ya Kati na Ulaya ya Mashariki na baadaye kupokelewa katika…

Soma Zaidi

- Kilimo, Usindikaji

Jifunze kusindika bamia

Bamia ni aina ya tunda mboga lenye utajiri wa virutubishi ambavyo ni muhimu sana katika mwili wa mwanadamu hasa katika usagaji wa chakula. Faida za ulaji wa bamia Umeng’enyaji na uwekaji sawa wa mfumo wa sukari mwilini. Kulainisha choo na kuzuia kuvimbiwa. Kuondoa lehemu katika mishipa ya damu kwenye mwili. Kuwepo kwa wingi wa virutubisho vya protini ambavyo vinahitajika katika…

Soma Zaidi

- Kilimo, Usindikaji

Namna ya kusindika boga lishe

Boga lishe ni miongoni mwa vyakula vilivyopo katika kundi la mimea ya Cucurbitaceae au familia ya squash. Boga hili huwa na umbo la kibuyu na rangi yake huwa ni ya kijani mpauko kabla ya kukomaa na likikomaa huwa na rangi ya chungwa kwa nje na ndani. Kwa sehemu ya nje, gamba lake huwa ngumu lakini likipikwa hulainika. Ndani ya mboga…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara

Jifunze kilimo cha mwani na faida zake

Mwani wa bahari si mmea mgeni kwa wakaazi wa maeneo ya pwani. Wengi hukusanya kwa matumizi ya biashara na wachache hujumuisha katika mlo wao. Hivi karibuni, katika mitandao ya kijamii, wataalamu wa lishe wamekua wakishawishi watu kujumuisha mwani katika milo yao, wakisema kuwa mwani una faida nyingi kwa afya. Mwani ni aina ya mimea inayoota na kukua kwenye maji chumvi…

Soma Zaidi