Kwa sasa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania, ni wazi kuwa shughuli za kilimo hai zimeshika kasi, huku kukiwa na ongezeko la wazalishaji wa bidhaa za kilimo hai. Hili ni jambo jema sana kwa kuwa waswahili wanasema taratibu ndiyo mwenda, na kidogo kidogo hujaza kibaba. Na hapa taratibu tunaona mwanga wa dunia kurudi katika hali yake ya uasili, ya awali…
Kilimo
MWENENDO WA MVUA MKOA WA ARUSHA
Ndugu Mkulima, kama tunavyofahamu huu ni msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini, ni muhimu kupata na kufahamu taarifa za mwenendo mzima wa msimu, nini kifanyike au kisifanyike katika uzalishaji na mwenendo wa maisha kwa ujumla. Tafadhali soma kwa kubonyeza hapa chini kupata taarifa kamili kwa mkoa wa Arusha https://www.meteo.go.tz/uploads/publications/sw1724331524-Downscaled%20OND%202024%20Rainfall%20Season%20Outlook%20(Swahili)%20for%20Arusha%20Region%20and%20Districts.pdf
Bei za mazao makuu ya chakula
Kama ilivyo ada tunawaletea habari za taarifa za mazao makuu ya chakula katika mikoa mbalimbali hapa nchini kama ilivyotayarishwa na wizara ya kilimo. Tafadhali bonyeza hapa kusoma zaidi https://www.viwanda.go.tz/uploads/documents/sw-1731069832-Wholesale%20price%206th%20November,%202024..pdf
Aina mbalimbali za maharage yanayolimwa Tanzania
Aina Sifa Uwezo wa uzaaji Kilo/Ekari Kiasi cha mbegu Kilo/Ekari 1. Kabanima Nyekundu yenye mistari, inavumilia magonjwa ya kutu nan dui. Hukomaa baada ya siku 87 600-1000 Wastani 26-28Kg 2. Uyole 84 Rangi ya maziwa, yanatambaa na hukomaa baada ya siku 105 600-1000 Wastani 26-28Kg 3. Uyole 94 Rangi ya maziwa na mistari nyekundu, Hukomaa baada ya siku 84 480-800…
Maharagwe ni chanzo bora cha virutubisho
Maharage sehemu ya familia ya kunde. Mmea wa mikunde hutoa mbegu kwenye ganda; maharagwe ni mbegu zilizokomaa ndani ya maganda haya. Maharagwe ni chanzo cha virutubishi vingi; zina aina mbalimbali za vitamini, madini na virutubisho vingine huku zikitoa kiwango cha wastani cha nguvu (carbohydrates). Maharage ni chanzo cha protini ambayo husaidia kujenga mwili, nyuzinyuzi ambayo husaidia umeng’enyaji wa chakula, madini…
Mazao funika na faida katika kilimo
Mazao funika ni aina ya mazao ambayo huoteshwa ili kufunika udongo na kwa lengo la kuongeza rutuba ya udongo na kuzalisha chakula na malisho. Mazao funika huoteshwa wakati wa kiangazi au huoteshwa pamoja na zao kuu wakati wa msimu wa kulima. Mazao haya huweza kuachwa kuendelea kuota katika msimu wote wa mazao mseto au yanaweza kungolewa na kuachwa juu ya…
Changamoto katika kufunika udongo
Kuna baadhi ya changamoto zilizopo katika ufunikaji wa udongo lakini pia kuna namna ya kukabiliana nazo. Maeneo yenye mvua kidogo Katika maeneo yenye mvua kidogo ambapo mara nyingi hunyesha kwa msimu mmoja tu, kutekeleza mbinu ya zao funika ni ngumu kwa kiasi fulani. Hii ni kutokana na sababu kuwa, mazao, miti na hata vichaka hubakiza masalia machache sana na ambayo…
Umuhimu wa mboga kiafya
Mboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, mboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za mboga kwenye chakula…
BEI YA MAZAO MAKUU YA CHAKULA
TAFADHALI FUNGUA KIAMBATANISHI HIKI KUJUA BEI YA BIDHAA YA MAZAO MAKUU YA CHAKULA HAPA NCHINI KATIKA MASOKO MAKUBWA KATIKA MIKOA MBALIMBALI https://www.viwanda.go.tz/uploads/documents/sw-1729766851-Wholesale%20price%2023rd%20October%202024-1.pdf
Faida za chaya kiafya
Amedeus Willium anauliza: Naomba kuuliza faida za chaya kwenye mwili wa binadamu Mkulima Mbunifu: Majani ya chaya ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma, protini, kalshiamu, Vitamini A, C, foliki, asidi na Vitamini B. Protini: Inajenga misuli. Mlo mmoja tu wa chaya ni sawa na kiwango cha protini kinachopatikana kwenye yai. Madini ya chuma: Kwa afya ya damu na nguvu…