Epuka kutengeneza loshoro itakayokaa muda mrefu sana kwenye kibuyu na kuendelea ongeza maziwa. Epuka kuloweka mahindi kwa muda mrefu na kutwanga kwa matumizi hii hupoteza nguvu na ubora wa wanga. Kuosha mahindi au maharage kwa kutumia magadi, hakikisha utayapika kwa kuongeza viungo au kutumia mboga za majani pembeni ili kurudisha virutubisho ulivyopoteza. Kuna baadhi ya vyakula hutumiwa sana nchini Tanzania…
Binadamu
Ni muhimu kuhakikisha usalama na kuzuia upotevu wa chakula
Umakini wa uzalishaji huzuia upotevu wa chakula Upotevu wa chakula hutokea katika mnyororo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji. Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi. Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla…
HERI YA MWAKA MPYA WA 2025!!!!!!
Ni matumaini yetu kuwa tumevuka wote salama na tuko tayari kuanza mwaka kwa kishindo na kwa mafanikio makubwa. Mkulima Mbunifu tumejiandaa vyema kuendelea kufikisha elimu kwako na kwa kushirikiana na wewe katika kuhakikisha tunatatua changamoto zote za kilimo na ufugaji na kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora na salama huku tukilinda afya zetu, afya za wanyama, afya ya mimea pamoja na…
Kilimo ikolojia kimeniongezea tija katika uzalishaji
Mbegu bora ya asili huchangia pakubwa katika usalama wa chakula na lishe kwa familia na jamii kwa ujumla. Hii inaambatana na matumizi ya mbinu bora za kilimo endelevu ili kumhakikishia mkulima uzalishaji wa juu nyakati zote na kwa muda mrefu. “Kabla ya kushiriki katika mradi wa CROPS4HD (Mazao yenye afya yasiyopewa kipaumbele), Mama Regina Mrope, kutoka Kijiji cha Mpindimbi, Masasi,…
Zalisha kwa malengo ili kupanua kilimo biashara
Kama kawaida jarida hili linatoa wito kwa wakulima kuanzisha na kujenga kilimo kuwa biashara inayoweza kuleta faida na kukidhi mahitaji ya kila siku hapo nyumbani. Hata hivyo, imekuwa ni kawaida kwa wakulima wengi kufanya shughuli zao bila kufanya maandalizi thabiti, na bila kuwa na mipango itakayowawezesha kupanua uzalishaji na kuifanya kuwa endelevu. Swala hili ni kikwazo kikubwa sana kwa sababu…
MWENENDO WA MVUA MKOA WA ARUSHA
Ndugu Mkulima, kama tunavyofahamu huu ni msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini, ni muhimu kupata na kufahamu taarifa za mwenendo mzima wa msimu, nini kifanyike au kisifanyike katika uzalishaji na mwenendo wa maisha kwa ujumla. Tafadhali soma kwa kubonyeza hapa chini kupata taarifa kamili kwa mkoa wa Arusha https://www.meteo.go.tz/uploads/publications/sw1724331524-Downscaled%20OND%202024%20Rainfall%20Season%20Outlook%20(Swahili)%20for%20Arusha%20Region%20and%20Districts.pdf
Maharagwe ni chanzo bora cha virutubisho
Maharage sehemu ya familia ya kunde. Mmea wa mikunde hutoa mbegu kwenye ganda; maharagwe ni mbegu zilizokomaa ndani ya maganda haya. Maharagwe ni chanzo cha virutubishi vingi; zina aina mbalimbali za vitamini, madini na virutubisho vingine huku zikitoa kiwango cha wastani cha nguvu (carbohydrates). Maharage ni chanzo cha protini ambayo husaidia kujenga mwili, nyuzinyuzi ambayo husaidia umeng’enyaji wa chakula, madini…
Mwelekeo wa mvua za vuli (Oktoba – Disemba) na nini wakulima wafanye (Taarifa na TMA)
Uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba – Disemba 2024, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja…
Tutunze mazingira na tusichome misitu hovyo
Katika maeneo mengi nchini Tanzania, uharibifu wa mazingira hasa unaotokana na ukataji miti ovyo kwa ajili ya kuchoma mkaa, ujenzi na shughuli za kilimo umekithiri kwa kiasi kikubwa. Jamii nyingi zimekuwa zikifanya hivyo bila kufahamu kuwa umaskini walio nao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa misitu. Imekuwa ni kawaida kwa watu wengi wanaoishi kuzunguka misitu katika maeneo mbalimbali hapa…
Hifadhi nafaka kwa njia sahihi kuepuka upotevu
Ni wazi kuwa wakulima wengine wamevuna nafaka mbalimbali kama vile maharage na mahindi katika msimu huu wa mavuno hivyo wasipokuwa makini na kuhifadhi kwa usahihi mavuno yote yatapotea kwa kuharibiwa na wadudu, panya, au hata ukungu unaotokana na unyevu. Ili kuepukana na hasara ni muhimu kuhakikisha unahifadhi mazao yako katika njia salama kama unavyoshauriwa na Mkulima Mbunifu au wataalamu wa…