Ubuyu ni tunda ambalo hupatikana kwenye miti jamii ya Adansonia. Ubuyu umekua na matumizi mbali-mbali wengi tukiutumia kama matunda. Wengine hutumia juisi yake kutengenezea barafu (ice cream). Pia kuongeza ladha kwenye vyakula.
Ubuyu umekuwa tunda lenye faida nyingi kwa mwili wa binadamu. Ni tunda la asili na linapatikana porini hasa katika kanda kame (semi-arid). Vitu vyote vilivyomo kwenye ubuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
Faida za ubuyu
Ubuyu una uwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili, kuimarisha mifupa, kusaidia mfumo wa umeng’e-nyaji chakula kupunguza maumivu, uvimbe na kusisimua utengenezaji wa seli na tishu mpya. Pia, husaidia kupu-nguza shinikizo la damu na kuzuia magonjwa sugu.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine
- Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
- Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kalisiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu a-mbayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
- Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini.
- Virutubisho vya kulinda mwili
- Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambazo ni muhimu katika kuo-ndoa sumu mwilini na ume-ng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili wa binadamu huwa pia na vitamin B2.
- Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
- Huongeza nuru ya macho
- Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
- Ina maginesiamu ambayo husai-dia kujenga mifupa na meno
- Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo
Juice ya ubuyu
Juisi ya ubuyu ni moja kati ya juisi zilizopata wanywaji wengi duniani kote katika miaka ya hivi karibuni, Juisi ya ubuyu ina virutubisho vya kalsiamu (Calcium) na madini ya chuma (Iron) ambavyo ni muhimu katika miili yetu hasa kwa watoto, wajawazito na wazee.
Jinsi ya kuandaa juice ya Ubuyu
- Katika kuandaa juisi ya ubuyu unahitajika kuwa na unga wa ubuyu au ubuyu wa mbegu, maji safi, sufuria, kijiko au mwiko, sukari, chujio, jagi na jiko.
- Ubuyu wa unga;changanya vikombe 6 na maji vikombe 9.
- Ubuyu wa mbegu; changanya vikombe 3 na maji vikombe 12.
- Weka sukari kiasi unachotaka, changanya vizuri na mwiko kisha bandika jikoni acha iche-mke kwa kiasi cha kutosha ili kuuwa vijidudu vya magonjwa kama vitakuwemo na itakuwa tayari kwa matumizi.
- Acha ipoe, alafu koroga na uweke katika jagi tayari kwa kunywa.
Matumizi
Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.
NGALIZO: Ili upate faida za juisi ya ubuyu, kama inavyoelezwa hapa, lazima upate ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.