Vitamini A ni mchanganyiko wa vyakula tofauti pamoja na baadhi ya matunda. Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza kila mmoja katika familia ale matunda na mboga za kutosha ilikupata vitamin A ya kutosha katika mlo wake kila siku, ilikuongeza kinga ya mwili, kuongeza uwezo wakufikiri na kupunguza hatari ya magonjwa.
Ni kwa namna gani Vitamini A inatufanya tuwe na afya iliyobora?
- Inasaidia ukuaji na ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu na ubongo.
- Inasaidia macho kuona vizuri hasa wakati wa usiku.
- Inaukinga mwili wako na magonjwa na kusaidia kupona haraka.
- Inasaidia kuimarisha mifupa, maneno, ngozi na viungo vya ndani kama utumbo na mapafu.
Vyakula vinavyompatia mwanadamu vitamin A
Mboga za kijani iliyokolea kama: mchicha, matembele, sukumawiki, majani ya maboga na majani ya mlonge.
Mboga za rangi ya njano na nyekundu kama: Maboga, viazi vitamu vya rangi ya njano na karoti.
Matunda ya rangi ya njano na nyekundu kama: Maembe yaliyoiva, fenesi na mapapai lililoiva.
Mazao ya wanyama: Mfano nyama nyekundu, maini, figo, samaki na mayai hutupatia vitamin A.
Ilikupata Vitamini A ya kutosha katika mlo wako: inatakiwa kila mmoja katika familia ale matunda na mboga za kutosha kila siku. Hakikisha unachagua mboga zenye rangi mbalimbali (kijani, nyekundu, njano)
- Kwa watoto wachanga chini ya miezi sita hupata vitamin A kutoka kwenye maziwa ya mama.
- Kuchanganya kiasi kidodgo cha nyama au samaki, maboga, au mboga za majani kwenye chakula cha mtoto huongeza kiwango cha vitamin A kwa watoto wenye umri zaidi ya miezi sita.
- Watoto wale mboga na matunda ikiwezekana mara 2-4 kwa siku.
- Vijana na watu wazima wale mboga na matunda ya kutosha kila siku.
- Akina mama wajawazito wanatakiwa kula kiasi kikubwa cha vyakula vyenye vitamin A kila siku.
Athari za upungufu wa vitamini A
- Kushindwa kuona vizuri hasa kunapokuwa na giza au mwanga hafifu.
- Ngozi kukauka au kupauka na wakati mwingine kuwa na vidonda huku nywele zikikosa afya.
- Kupata maambukizi ya magonjwa mara kwa mara hasa katika mfumo wa njia ya hewa na mfumo wa mkojo.
- Watoto wadogo kuugua surua kwa urahisi.
- Kudumaa kwa watoto kutokana na kukoma kukua na kuongezeka uzito.
- Ukuaji wa taratibu na wenye kasoro wa mifupa na meno.
Athari za kuzidi kwa matumizi ya vitamini A mwilini
Virutubisho vya vitamini A vikizidi mwilini navyo huweza kupeleka athari mbalimbali kama ifuatavyo;
- Kuhisi kizunguzungu pamoja na kichefuchefu.
- Kuhisi maumivu ya kichwa pamoja na mzio.
- Maumivu ya viungo na mifupaKupoteza fahamu.
- Mtoto aliye tumboni kuumbika kimakosakama mama mjamzito akizidisha matumizi ya dawa zenye vitamini A.
- Kunyonyoka nywele.
- Udhaifu wa mifupa ambapo huweza kupelekea kuvunjiakwa urahisi.
- Kukosa usingizi.