Musa Hamisi anauliza: Za majukumu Mkulima Mbunifu, naomba kujua ni kipindi gani napaswa kuandaa mashimo na Je, naweza kupanda migomba aina 3 tofauti ndani ya shamba moja lenye ekari moja? Mkulima Mbunifu: Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma machapisho ya MkM. Migomba huhitaji Kiasi cha chini cha mvua kifaacho ni 100mm kwa mwezi au 1200mm…
Kilimo cha migomba
Musa Hamisi anauliza: Za majukumu Mkulima Mbunifu, naomba kujua ni kipindi gani napaswa kuandaa mashimo na Je, naweza kupanda migomba aina 3 tofauti ndani ya shamba moja lenye ekari moja? Mkulima Mbunifu: Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma machapisho ya MkM. Migomba huhitaji Kiasi cha chini cha mvua kifaacho ni 100mm kwa mwezi au 1200mm…
Mfugaji mashuhuri wa kuku wa kienyeji Singida
Kama ilivyo ada, Mkulima Mbunifu tumekuwa tukikufikishia taarifa toka kwa wakulima katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanaojishughulisha na kilimo ikolojia nia yetu ikiwa ni kuwawezesha wakulima wengine kujionea na kujifunza ni kwa namna gani wakulima wenzao wameweza kufanikiwa katika kilimo ikolojia. Miongoni mwa wakulima waliopata fursa ya kutembelewa na kuhojiwa na jarida hili ni mfugaji toka mkoani Singida ambaye anajishughulisha…
Kilimo cha mbogamboga chatia chachu kwa maendeleo ya elimu
Wakati Tanzania ikikabiliwa na changamoto katika kuhakikisha lishe bora kwa watoto hasa katika maeneo ya vijijini na mijini, kuanzishwa kwa kilimo cha mbogambogambogamboga katika shule za msingi kunaweza kuwa ni kichocheo cha mabadiliko ya namna bora ya kujenga na kuelimisha akili changa za vijana na kuwafanya wakue katika mazingira bora ya kufikiri na kudadisi mambo mbali mbali. Haya yanaweza kushuhudia…
MAONYESHO YA SIKU YA CHAKULA DUNIANI, NINI UMEJIFUNZA
Maadhimisho ya siku ya chakula duniani, yenye kauli mbiu “Haki ya chakula kwa wote, kwa maisha ya sasa na ya baadaye” Je, unafikiria nini kuhusu haki ya chakula kwa maisha ya sasa na ya baadaye? Kama ni mkulima au ni mfugaji unafikiuria nini kuihusu chakula?
Kusindika pilipili kali Pilipili husindikwa kupata unga wa pilipili, sosi na lahamu
a) Kusindika pilipili kavu kupata unga Pilipili kali huumiza macho na pia harufu ikivutwa huleta mkereketo ndani ya pua na kifua wakati wa kusaga ili kupata unga. Inashauriwa kuchukua tahadhari zifuatazo; Vumbi la pilipili kali huumiza macho hivyo inashauriwa kuvaa miwani ya kukinga macho na vumbi hilo wakati wa kusaga au kufungasha. Aidha, mtu anayejishughulisha na kazi ya kuchambua, kusaga…
Mwelekeo wa mvua za vuli (Oktoba – Disemba) na nini wakulima wafanye (Taarifa na TMA)
Uchambuzi wa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kipindi cha Oktoba – Disemba 2024, ushauri na tahadhari kwa wadau wa sekta mbalimbali kama vile kilimo na usalama wa chakula, mifugo na uvuvi, maliasili, wanyamapori na utalii, nishati na maji, usafirishaji (nchi kavu, kwenye maji na angani), mamlaka za miji, afya pamoja…
Umuhimu wa wataalamu kwa wakulima na wafugaji
Wataalamu wa kilimo na mifugo wamepata mafunzo ili kuendeleza mbinu za kilimo na mifugo kwa lengo la kutoa faida kwa wakulima na wafugaji. Baadhi ya wataalamu wanaweza kuona upungufu fulani au kuona kuwepo kwa mantiki kwenye baadhi ya mbinu za asili ambazo bado zinatumiwa katika uendeshaji wa kilimo na ufugaji na kuweza kuafikiana na wakulima hao juu ya kuziendeleza au…
TNAELEKEA MSIMU WA VULI, HAKIKISHA KUKU WAMEPATA CHANJO STAHIKI NA KWA WAKATI
Watu wengi wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa kuku bila kuzingatia kanuni bora za utekelezaji wa mradi huo. Moja ya mambo ambayo wafugaji mara nyingi husahau kuzingatia ni utoaji wa chanjo sahihi na kwa muda muafaka. Ni muhimu kufahamu mambo unayotakiwa kuzingatia katika kuwapatia kuku chanjo. Wakati wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya magonjwa,…
Kabla ya kuingia shambani kuzalisha andaa mpango biashara
Kila mara wakulima wanashauriwa kuweka kilimo katika mtazamo wa kibiashara. Wakulima wanaochukua na kuufanyia kazi ushauri huo, kisha kufanya shughuli za kilimo kitaalamu na kwa mtazamo wa kibiashara ,wanapata faida. Kuwa na wazo ni aina gani ya kilimo unayoweza kuifanya kibiashara pekee haitoshi. Huo ni mwanzo tu. Ni lazima kukusanya au uwe na pesa/mtaji kwa ajili ya kugharamia shughuli hiyo,…