- Kilimo

Sindika machungwa kuepuka hasara na upotevu usio wa lazima

Machungwa ni moja ya mazao ya matunda ambayo yanalimwa sana kwa wingi katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Mwanza. Zao hili ni la chakula na biashara. Ikiwa huu ni msimu wa machungwa, wakulima hawana budi kujifunza namna mbalimbali za kusindika zao hili ili kuondokana na upotevu unaotokana na wingi wake na kukosekana kwa soko…

Soma Zaidi

- Kilimo, Mifugo, Mimea

Gliricidia: Mti wenye faida lukuki kwa mkulima

Gliricidia ni mti ambao kisayansi hujulikana kwa jina la gliricidia sepium ambao hutumika kwa ajili ya mbolea au kurutubisha ardhi. Mti huu wa gliricidia ni  jamii ya miti ya malisho ambayo majani yake hutumika kurutubisha udongo na kulishia mifugo hasa katika kipindi cha ukame. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kumudu kuzalisha wakati wa kiangazi pamoja na kudumisha hali…

Soma Zaidi

- Kilimo Biashara, Mafuta, Usindikaji

Usindikaji wa karanga kupata mafuta

Karanga hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali au kukaangwa ili kutumika kama vitafunwa lakini pia kusindikwa ili kupata mafuta, siagi na rojo. Karanga zina virutubisho vingi kama vile; maji asilimia 7, nguvu kilokari 570, protini gramu 23, mafuta gramu 45, wanga gramu 20, kalishamu miligramu 49, chuma miligramu 3.8, patasiamu miligramu 680, vitamini B miligramu 15.5 na vitamini A (I.U…

Soma Zaidi

- Mifugo

JAGEF wanaonesha njia katika usindikaji wa vyakula

“Kukaa mwenyewe na kufanya shughuli za ujasiriamali ni rahisi sana kuanguka, kutokutambuliwa au kuweza kupiga hatu, lakini mkiwa kwenye kikundi, mnapiga hatua kwa haraka sana na wepesi zaidi” Ndivyo alivyoanza kueleza mama Ester Moshi, mwenyekiti wa kikundi cha wasindikaji cha JAGEF katika kijiji cha Kikarara Old Moshi mkoani Kilimanjaro alipokuwa akielezea shughuli za kikundi hicho. JAGEF kilianza mwaka 2010 kikiwa…

Soma Zaidi

- Kilimo Biashara, Usindikaji

Kutoka kuzalisha maziwa mpaka kiwanda cha kusindika

Biashara ya maziwa ni biashara maarafu sana katika maeneo ya kanda ya kaskazini mwa Tanzania ambapo kuna wafugaji wengi.  Biashara hii imeweza kuwanufaisha wafugaji wengi ikiwa ni miongoni mwa zao la mifugo linalo wasaidia wafugaji kujikwamua kiuchumi. Uzalishaji na uuzaji wa maziwa ni kitega uchumi kizuri ikiwa itafanywa kwa kuzingatia kanuni, taratibu na kuzalishwa katika hali ya usafi. Biashara hii…

Soma Zaidi

- Kilimo

Fuata kanuni sahihi za kilimo upate mavuno bora

Wakulima walio wengi wamekuwa wakijikita zaidi katika matumizi ya mbolea    ili kupata matokeo mazuri katika kilimo,  na kusahau kuwa kanuni bora za uzalishaji pia huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka na kupatikana kwa mavuno yenye ubora. Nini cha kuzingatia ili kupata mavuno bora Ni lazima mkulima kufuata utaratibu wa uzalishaji wa mazao katika kila msimu wa kilimo. Hatua zifuatazo ni lazima…

Soma Zaidi

- Mifugo

Mayai yanaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu

Wakulima wanaowekeza kwenye mradi wa kuku, hupata hasara pale ambapo hawatunzi mayai ipasavyo. Mayai ni bidhaa hafifu na inayoharibika kwa haraka, hivyo, ni lazima ishikwe kwa uangalifu na kutunzwa vizuri baada ya kutagwa ili yasivunjike au kuharibika. Watu wengi wanaonunua mayai kutoka dukani watatambua mara moja kuwa mayai hayo yamevunjika au yameoza. Tatizo hili linaweza kutokana na utunzaji na uhifadhi…

Soma Zaidi

- Kilimo

Utupa: Mmea wa ajabu unaofaa kwa matumizi mengi

Utupa ni aina ya mmea unaopatikana zaidi sehemu zenye baridi hasa nyanda za juu na unastawi sehemu zenye mvua za wastani na nyingi. Mmea huu hauhimili ukame. Utupa hukua haraka na kusambaa kama usipodhibitiwa, baadhi ya nchi mmea huu umepigwa marufuku kupanda kwa sababu ya kutishia uoto wa asili. Matumizi Kufukuza panya / mchwa Mmea wa utupa ni moja ya…

Soma Zaidi

- Mifugo

Wanafunzi wa shule ya msingi kioga nao hawako nyuma katika kilimo

Ni miaka tisa sasa tangu kuanzishwa kwa jarida la Mkulima Mbunifu likiwa limejikita katika kutoa elimu kuhusu kilimo, ufugaji, pamoja na kilimobiashara kwa lengo la kusaidia jamii kujikimu kimaisha. Jarida hili, limeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, katika kufikisha elimu kwa wadau mbalimbali na kuonesha fursa nyingi zilizopo kwenye kilimo na ufugaji hasa katika kilimo hai. Mkulima Mbunifu pia limewafikia wanafunzi…

Soma Zaidi