Mkakati mzuri kwa wakulima wanaozingatia ikolojia ni kujifunza na kuelewa sababu ya magonjwa, athari zake ili kuweza kukabiliana nayo. Hii inasaidia kulinda mazao ya mimea, kudumisha usalama wa uzalishaji wa chakula.
Kwa kawaida, ni ngumu kuzuia ama kurekebisha tatizo ikiwa haujaelewa tatizo lenyewe. Ndio maana wakulima wanashauriwa kuwa makini shamba-ni kutambua kwa haraka uvamizi wa wadudu na pia magonjwa.
Maana rahisi ya magonjwa ya mimea ni kuwepo kizuizi, au usumbufu fulani unaosababishwa na magonjwa. Kutokana na sehemu ya mmea kupata usumbufu huo, seli za mmea zinaweza kufa au hata kusababisha mmea kufa kabisa. Jambo hili kwa kawaida husababisha kuathirika kwa kiwango cha mavuno, au kuwa na mavuno yasiyokuwa na ubora.
Magonjwa ya mimea yanaweza kugawanywa katika makundi mawili:
- Magonjwa yanayosababishwa na vimelea vya nje, au yana-yosababishwa na vimelea wengi-ne kama vile fangasi, bakteria, virusi na minyoo inayoshambulia mimea.
- Magonjwa yasiyosababishwa na vimelea (yasiyotokana na ma-ambukizi). Dalili zake hutokana na sababu mbalimbali, hii ni pamoja na madhara yanayotokana na madini, kutokuwepo na uwiano wa virutubisho, kukosea wakati wa kuvuna na kuhifadhi, vichocheo vinavyotokana na mazingira, kwa mfano, uchafuzi wa mazingira na madhara yanayotokana na dawa za kuulia magugu.
- Kiwango cha wadudu wana-osababisha magonjwa wanao-kuwepo
- Ugonjwa unaweza kuenea kwa kiwango gani
- Muda ugonjwa unaoweza kujite-ngeneza na kuenea.
- Mzunguko wa mazao ni moja wapo ya njia nzuri sana za udhibiti wa magonjwa, hii ni kwa sababu aina flani ya wadudu hushambulia na kuathiri aina moja tu ya mazao.
- Usafi wa mazingira hutegemeana na shughuli za kitaalamu za kilimo zinazolenga kutokomeza au kupunguza vichocheo vya maambukizi kwenye mimea au kwenye shamba. Hii inajumuisha kuondoa na kuharibu mabaki yote ya mavuno ambayo wadudu wanaweza kuishi pamoja na magugu yanayoweza kuwa wenyeji wa wadudu hao.
- Magonjwa pia yanaweza kupunguzwa au kudhibitiwa kwa kupanda aina ya mazao yenye uwezo wa kukabiliana na magonjwa au yanayovumilia magonjwa.
- Unaweza kubadilisha muda wa kupanda aina fulani ya mazao, ili kukwepa kipindi ambacho huwa na kiwango kikubwa cha mlipuko wa aina fulani ya magonjwa.
- Wakati huo huo aina fulani ya mimea huwavutia aina tofauti ya wadudu na magonjwa ambayo baada ya muda fulani hujijenga katika eneo hilo.
Maoni kupitia Facebook