- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kuku, Kutuhusu, Masoko, Mazingira, Mifugo, Udongo, Usindikaji

NANE NANE 2022, UNAKOSAJE MAONYESHO HAYA, MKULIMA MBUNIFU KAMA KAWAIDA YETU TUTAKUWEPO KUKUJUZA KUHUSU KILIMO NA UFUGAJI

Sambaza chapisho hili

Hayawi hayawi sasa yamekuwa, nane nane hiyoo imekaribia. Nchini Tanzania, kila mwaka, wakulima na wafugaji hujumuika kwa pamoja kwa muda wa siku takribani kumi kuadhimisha sikukuu ya wakulima nchini. Sherehe hizi hufikia kilele siku ya tarehe nane mwezi wa nane.

Katika kipindi hiki wadau mbalimbali wa kilimo, huandaa mazao na bidhaa mbalimbali za kilimo kwa ajili kushirikisha bunifu mbalimbali na pia kujifunza kutoka kwa wengine.

Fursa hii muhimu husaidia wakulima kuangaza aina mbalimbali za mbegu, teknolojia za kilimo na pia kubadilishana mawasiliano kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa mazao na kupata masoko ya bidhaa zao.

Sherehe hizi za nane nane haziku-fanyika mwaka 2021 kutokana na janga la virusi vya Uviko 19. Ugonjwa huu umetikisa dunia na kuleta tafrani katika nyanja mbalimbali za kiuchumu.

Hata hivyo wadau wa kilimo tunaendelea kuwashauri kuchukua tahadhari hasa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi. Bado shirika la afya duniani linashauri watu kuhakikisha wananawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni kila wakati, kutumia kitakasa mikono pamoja na kuvaa barakoa.

Mkulima Mbunifu tunakuka-ribisha katika banda letu, tujifunze na kuhojiana ana kwa ana na pia kutakua na fursa ya kuona kwa vitendo kupitia wenzetu wa shamba la kilimo hai kutoka Mwanga, Kilimanjaro. Usikose, nane nane ni kwaajili yako.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “NANE NANE 2022, UNAKOSAJE MAONYESHO HAYA, MKULIMA MBUNIFU KAMA KAWAIDA YETU TUTAKUWEPO KUKUJUZA KUHUSU KILIMO NA UFUGAJI

    1. Habari,
      Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuwa miongoni mwa wasomaji wa makala zetu. Kuhusu kilimo cha mlonge bado hatujaandika ila tutafanyia utafiti tuweze kuandika taarifa sahihi kwa ajili yako na wakulima wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *