- Kilimo, Mazingira, Udongo

Tumia majivu shambani

Sambaza chapisho hili

Majivu yana kiwango cha wastani wa madini kwa mgawanyiko tofauti, potasiamu 5% – 7%, kalishamu 25% – 50%, fosiforasi 1.5% – 2% na madini mengine kwa kiasi kidogo. Pia mabaki ya chenga za mkaa kwenye majivu yanasaidia kunyonya baadhi ya sumu kwenye ardhi.

Matumizi

Tumia kiasi cha kilo 2.5 mpaka 5 kitumike kwenye eneo la mita za mraba 33 au futi 100 za mraba, na majivu yamwagwe wiki 3 – 4 kabla ya kupanda kitu chochote ardhini.

Madhara

Kila kitu kikitumiwa zaidi ya kiasi kina madhara na majivu pia yana madhara kwenye udongo kwa sababu yana hali ya kuwa alkaline zaidi (10 – 12 pH) kwa sababu baadhi ya mchanganyiko wake hauyeyuki kwenye maji.

Endapo utahitaji kuongezea kwenye mimea yenye upungufu wa madini kama fosforasi na potasiamu basi hakikisha majivu hayagusi mashina kwani yanaweza kuuungua hasa kama mimea ni michanga.

Pia majivu yana kiasi kidogo sana cha naitrojeni ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya mmea wowote ule, kwa hiyo hakikisha pia unatumia vyanzo vingine kwa ajili ya naitrojeni. Mimea jamii ya mikunde inafaa zaidi.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

2 maoni juu ya “Tumia majivu shambani

    1. Habari,
      Karibu sana Mkulima Mbunifu. Tunafurahi kusikia kuwa umejifunza kupitia makala ya majivu na sasa umefahamu umuhimu na matumizi ya majivu shambani.

      Karibu sana Mkulima Mbunifu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *