Gugu karoti (Parthenium hysterophorus) ni mmea vamizi ambao una madhara mengi kwa binadamu, mazao, wanyama au mifugo pamoja na kuharibu uoto wa asili.
Gugu hili lina madhara mengi kama; Muwasho unaoweza kusababisha kujikuna na kupata malengelenge, ugonjwa wa pumu ukivuta vumbi lake, muwasho wa macho, mnyama kupasuka na kuvimba midomo kama akila majani.
Aidha gugu karoti husababisha maziwa ya ng’ombe kuwa machungu na kupungua uzalishaji, ubora wa nyama kupungua, kuzuia mbegu ya mazao kuota na kupungua kwa mavuno pamoja na kubadili uoto wa asili na kuua malisho.
Namna ya kudhibiti gugu karoti
- Ondoa mimea hii pembezoni mwa barabara kwani ni chanzo kuu cha kwanza cha kuenea mashambani.
- Ng’oa mimea yote kabla na hata baada ya kutoa maua.
- Baada ya kung’oa kusanya sehemu moja, acha ikauke na kisha choma moto.
- Hakikisha unang’oa majani na mzizi mkuu kwani mzizi ukibaki ardhini huchipua kwa upya.
- Tumia viumbe hai (biological agents (Zygogramma Bicolorata) kwa ajili ya kutekekeza mimea hii.
Maoni kupitia Facebook