Kwa mtazamo wa kiekolojia, viumbe wote ni sehemu ya mfumo asilia bila kujali vinafanya nini. Kwa mkulima, viumbe vyote ambavyo hupunguza mavuno ya mazao yake huchukuliwa kuwa ni wadudu waharibifu.
Kilimo cha zao la mhogo, kama ilivyo kwa mazao mengine ya mizizi, kinazongwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za wadudu na magonjwa ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiasi cha mavuno, na ubora wa mazao.
Pia changamoto hii ya wadudu na magonjwa ya mihogo inaongeza gharama za uzalishaji ambazo hazikutarajiwa. Ni muhimu kwa mkulima kuwa na ufahamu wake ili aweze kuandaa mazingira bora ambayo yatachochea maambukizi na kuenea kwa wadudu na magonjwa ya mihogo.
Utitiri kijani wa mihogo
Utitiri kijani wa mihogo ni wadudu waharibifu wa mhogo nchini Tanzania na maeneo mengine ya Africa ambao husababisha hasara kubwa katika mavuno. Utitiri unaweza kuenezwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa urahisi kupitia majani, vikonyo na upepo. Mfumo wa mseto unahitajika ili kudhibiti wadudu na kupunguza uharibifu.
Njia za kitamaduni kama vile kutumia vikonyo safi, kupanda mapema katika msimu wa mvua na kilimo cha mseto na mbaazi, kunaweza kupu-nguza idadi ya wadudu.
Dalili muhimu
- Utitiri kijani wa mihogo huwa na rangi ya kijani mpaka manjano na huwa vigumu kuonekana kwa macho (huonekana kama vidoa vidogo vya rangi ya kijani-manjano).
- Utitiri hula upande wa chini wa majani machanga na mashina ya mhogo ya kijani kibichi. Tumia le-nsi ya mkono ili kuweza kuwaangalia utitiri upande wa chini wa majani, kwenye mishipa na karibu na mwanzo wa jani.
- Idadi ya utitiri huongezeka kwenye majani machanga wakati wa mwanzo wa msimu wa ukame na hushambulia mmea kwa kufyonza utomvu kutoka kwenye seli za ti-shu za mmea, ambayo husababisha madoa ya rangi ya manjano kuonekana kwenye majani kutokana na upungufu wa chlorophyll (kijani kibichi). Majani yanaweza kuwa na mabato na kufa.
- Dalili hizi zinaweza kuchanganywa na dalili za virusi vya cassava mosaic, lakini virusi vya cassava mosaic husababisha mabaka makubwa ya rangi ya kijani-manjano na umbo la majani huharibika. Mashambulizi makali ya utitiri kijani wa mihogo husababisha majani ya juu (au mapya) kufa na kuanguka na kilele cha mti wa mhogo huonekana kama mshumaa.
Kinga
Mambo ya kufanya kabla ya dalili kuonekana
Mbinu za kitamaduni
- Hakikisha kuwa vipandikizi safi vinatumika.
- Kagua chomozo mpya kwenye vikonyo vya mihogo kwa karibu ili kubaini uwepo wa utitiri.
- Panda mapema, mwanzoni mwa msimu wa mvua, ili kuwezesha ukuaji wa majani na mimea amba-yo inaweza kuhimili mashambulizi. Mimea ya mihogo ya umri kati ya miezi 2 na 9 hushambuliwa kwa urahisi.
- Panda mseto na mbaazi, kila miraba miwili au mitatu, ili kupunguza uharibifu na pia kuongeza uzalishaji.
Udhibiti na mambo ya kufanya baada ya dalili kuonekana
Mbinu za kitamaduni
- Utitiri kijani wa mihogo unaweza kudhibitiwa kiasili na kibaiolojia ikiwa ni pamoja na wadudu wanaokula utitiri kama Typhlodromalus manihoti Moraes.
- Wakati wa msimu, majani ambayo yanaonesha ishara ya utitiri lazima kuondolewa na kuharibiwa mbali na shamba. Baada ya kuvuna, haribu mabaki yote ya mazao yaliyoathirika.
Athari
Utitiri kijani wa mihogo ni wadudu waharibifu wakubwa wa mihogo. Wanaweza kupunguza mazao sana kwa kupunguza majani na kupunguza uwezo wa mmea kujitengezea chakula.
Kutokana na kupungua kwa ukuaji wa mimea, majani machache yanapatikana kwa mavuno kama mboga ya kijani na hasara ya mavuno ya mihogo inaweza kuwa kati ya asilimia 10- 80. Vipindi virefu vya ukame vinaweza kusababisha kuongezeka kwa idadi ya utitiri na kupunguza mazao zaidi.