- Kilimo, Udongo

Namna ya kutengeneza busta

Sambaza chapisho hili

Busta za asili ni nyongeza ya virutubisho kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa mmea ili kua na uzalishaji mzuri hususani pale ambapo mimea imeanza kuzorota kutokana na kupungua/kukosekana kwa virutubisho vya kutosha kwenye udongo, busta hizi zina sifa ya kuupa mmea virutubisho kwa haraka sana na kuleta matokeo mazuri kwenye mimea ndani ya muda mfupi(siku 3).

Aina za busta

  1. Busta za mbolea za asili/chai ya mmea(samadi/mboji)
  2. Busta ya lantana na alizeti pori/mwitu

Namna ya kutengeneza busta ya asili kwa kutumia samadi au mboji

Mahitaji
Chombo kama vile ndoo au pipa, kiroba (mfuko unaoruhusu maji kupenya), mti, maji, na mbolea hai (samadi au mboji).

Namna ya Kutengeneza

  • Pima mbolea nusu ya chombo utakachokitumia kisha weka mbolea hiyo kwenye mfuko uliouandaa
  • Ning’iniza mfuko wenye mbolea ndani ya chombo unachotumia kwa kuufunga kwenye mti unaokatiza juu ya chombo chako.
  • Jaza maji ndani ya chombo ulichoningi’niza mbolea kwenye mfuko.
  • Tingisha mfuko wenye mbolea ndani ya chombo kila baada ya siku moja (masaa 24) kwa siku 3.
  • Baada ya siku ya tatu kamua mbolea iliyopo kwenye mfuko ili kupata juice yake ambayo sasa itakua na virutubisho vyote vilivyokuwemo kwenye mbolea yako uliyoiweka awali..
  • Hapo utakua umepata busta ya asili ikiwa ni mbolea ya samadi au mboji katika mfumo wa limiminika

Matumizi

  • Tumia gramu 100 kwa kila mche kwa mazao yenye mashina yasiyo ya karibu (unaweza kutumia kikopo cha mafutakupima).
  • Au kwa mazao ya karibukaribu sana kama karoti au vitunguu, wekw busta yake kwenye bomba kisha pulizia kuweka unyevu kwenye udongo
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *