Kilimo cha mboga

- Kilimo

Mahitaji ya uzalishaji wa mbogamboga

Mbegu Kwa matokeo mazuri ikiwemo ukuaji mzuri wa mbogamboga na mavuno mengi mkulima anashauriwa kutumia mbegu bora zilizothibitishwa. Mbegu hizo huwa na sifa zifuatazao: Hutoa mavuno mengi ya kiwango bora. Zina uwezo mkubwa wa kuota. Huhimili baadhi ya wadudu na magonjwa. Hukua kwa haraka, kwa usawa na ni imara. Ikolojia ya Eneo Eneo linalofaa kwa uzalishaji wa mbogamboga za majani…

Soma Zaidi

- Kilimo

Umuhimu wa mboga kiafya

Mboga ni mojawapo ya chakula bora kwani zikiliwa zenyewe kwa kuchanganya zina viini lishe tosha. Hata hivyo, mboga zimegawanyika katika makundi kutokana na sehemu ya mmea iliyo muhimu katika chakula cha binadamu na viini lishe vipatikanavyo. Sehemu za mmea wa mboga zinazotumika kama chakula ni pamoja na mizizi, shina, majani, matunda, maua na mbegu. Kazi muhimu za mboga kwenye chakula…

Soma Zaidi

- Kilimo, Kilimo Biashara

Ahamasika kufanya kilimo hai baada ya kusoma jarida la MkM

‘’Nimejifunza mambo mengi toka jarida la Mkulima Mbunifu hasa kuzalisha kwa misingi ya kilimo hai na nimeweza kutekeleza kwa vitendo ili wengine wajifunze kutoka kwangu”. Hayo ni maneno ya Bw. Kastuli Paulo toka kijiji cha Tumati, Wilaya ya Mbulu (Arusha), mkulima wa kilimo hai ambaye anajishughulisha na uzalishaji wa mazao mbalimbali kama vile viazi mviringo, mboga za majani ikiwamo chainizi,…

Soma Zaidi

- Kilimo

Liki (leek) moja ya mazao ya mboga yasiyoshambuliwa na magonjwa

Ni vyema kuchagua aina ya mazao ambayo hayana gharama kubwa kuzalisha, wakati huo huo yakiwa na faidi kubwa. Kwa mtindo huo utaweza kupata faida ya kutosha. Liki ni moja ya mazao ya mbogamboga, ambayo yanapata umaarufu mkubwa nchini Tanzania, kutokana na kuzalishwa katika maeneo mengi, na kuwa na soko la uhakika. Zao hili ni moja kati ya mazao ya mboga…

Soma Zaidi

- Mifugo

Fuata kanuni sahihi za kilimo upate mavuno bora

Wakulima walio wengi wamekuwa wakijikita zaidi katika matumizi ya mbolea    ili kupata matokeo mazuri katika kilimo,  na kusahau kuwa kanuni bora za uzalishaji pia huchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka na kupatikana kwa mavuno yenye ubora. Nini cha kuzingatia ili kupata mavuno bora Ni lazima mkulima kufuata utaratibu wa uzalishaji wa mazao katika kila msimu wa kilimo. Hatua zifuatazo ni lazima…

Soma Zaidi

- Mifugo

Mkulima Mbunifu imenihamasisha kuanza kufanya kilimo hai

“Nimeamua kuanza kufanya kilimo hai kwani ni rahisi, sitatumia dawa za kemikali wala mbolea za viwandani.  Nilikua nikifanya kilimo cha mazoea bila kujali afya yangu na watu wengine. Sikufahamu madhara kwa mazingira yani ardhi, mimea na hata wanyama”. Hayo ni maneno ya Godwin Zakaria Axwesso (52) anayeishi kijiji cha Bashay, wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha.   Alifanya kilimo cha kawaida…

Soma Zaidi

- Mifugo

Zikaushe mboga za ziada kwa matumizi ya baadaye

Kukausha mavuno kutoka shambani mwako, ni njia nzuri zaidi kukuwezesha kukabiliana na hali ngumu. Kukausha mboga na matunda ni njia rahisi sana ya uhifadhi inayotumika duniani kote. Hata hivyo, ili kupata matokeo mazuri na bora, baadhi ya kanuni ni lazima zifuatwe. Kukausha kwa jua Jua hutumika kwa mazao ambayo hayaharibiki yanapokaushwa kwa kutumia jua moja kwa moja, mfano maharagwe, karanga…

Soma Zaidi