- Mifugo

Taarifa muhimu kuhusu ufugaji wa mbuzi

Sambaza chapisho hili

Mbuzi na kondoo ni wanyama ambao wanaweza kufugwa kwa gharama nafuu pia ni wavumilivu wa ukame na maradhi tofauti na ngo’mbe kwa kua wana umbile dogo wanaweza kufugwa katika eneo dogo na nguvu kazi ndogo na hata kwa wenye kipato kidogo.

Katika makala hii Mkulima Mbunifu inangazia kuhusu ufugaji wa Mbuzi. Makala kama hii inaweza kua umeshasoma, ila kwaajili maombi ya wasomaji wa jarida hili tutatilia mkazo uzalishaji, ukuzaji na lishe. 

Uzalishaji

Mbuzi wenye afya huingia joto mara kwa mara, na huweza kuwa na watoto wapatao watatu kila baada ya miaka miwili.

Kabla ya wafugaji kuanza upandishaji wa mbuzi ni vema kuzingatia yafuatayo:

  • Uzito na sio umri huamua wakati sahihi wa mbuzi kuanza kupandishwa, kwa ujumla, beberu huwa tayari wana ukomavu katika muda wa miezi minne.
  • Mbuzi huanza kupandishwa pale watakapofikia 3/4 ya ukomavu na uzani wa jamii hiyo ya mbuzi.
  • Beberu anaweza pandishwa kwa mbuzi jike 10 hadi 20, lakini kama atapandishwa kwa mbuzi wengi zaidi ubora haki hupungua.
  • Kwa ajili ya uzalishaji, beberu inabidi wawe na afya na sio mafuta mengi kwani hupunguza ubora wa manii (mbegu).
  • Mbuzi jike ambao wana afya, waliokomaa na ambao hawana mimba huingia joto katika siku ya 17 hadi 21, na hutakiwa kupandishwa ndani ya masaa 24 hadi 36 tangu kuingia joto. 

Kutambua mbuzi jike aliye na joto

  • Mbuzi anahangaika, hutingisha mkia wake pale anapoguswa katika maungo karibu na miguu ya nyuma na akisimama karibu ya beberu hukojoa.
  • Maungo ya nje ya uke wa mbuzi huwa mekundu kidogo na kuvimba.

Ukuzaji

Baada ya kuzaliwa

  • Watoto ni lazima kunyonya maziwa ya mama yenye virutubishi katika kipindi cha saa 24 baada ya kuzaliwa kwani yana kinga imara dhidi ya maambukizi.
  • Mbuzi ambao hukataa watoto hupaswa kuangaliwa mpaka pale watakapo anza nyonyesha. Hata hivyo, kukataa watoto inaweza kuwa ishara ya afya duni.
  • Kuwafuta watoto waliokataliwa na plasenta inaweza kumsaidia mama kuwakubali.
  • Watoto waliokataliwa au ambao ni yatima wanaweza kunyweshwa maziwa ya uzazi kwa kutumia mbuzi wengine au kutoka katika maeneo ya karibu.
  • Watoto waliofutwa na plasenta inaweza saidia kukubaliwa na mbuzi jike mwingine.
  • Maziwa ya uzazi yaliozidi yanaweza kuhifadhiwa katika nyuzi joto za sentigredi 4 kwa hadi miezi mitatu na kutumika kulisha watoto yatima au walio kataliwa.
  • Aina nyingine ya maziwa ya mbuzi, au maziwa ya ng’ombe yaliochanganywa na maji au hata maziwa ya unga yanaweza kutumika wakati maziwa ya uzazi yanapokuwa hayapo.

Hatua za kuanza kuwategeza mbuzi watoto

  • Katika umri wa miezi miwili hadi mitatu, yapasa kutenganisha watoto na mama zao kwa kuanza kuwalisha nyasi na nafaka.
  • Kulisha watoto na sehiu ya mmea safi ili kupunguza hatari ya maambukizo ya minyoo.
  • Watoto wanapaswa kula katika malisho bora na mama zao.
  • Watoto wanahitaji maji safi ya kunywa.
  • Watoto wanapaswa kuachishwa kunyonya na kuanza kujifunza kula majani na nafaka angalau miezi miwili kabla ya mama zao kupandishwa tena.

Kulisha na lishe

Mbuzi wanaolishwa vizuri huzalisha maziwa na nyama zaidi. Mbuzi jike katika mwezi wa mwisho kabla ya kuzaa anahitaji protini na vyakula vyenye nguvu zaidi ya mbuzi wa kawaida.

Maji

  • Mbuzi wa maziwa wanahitaji angalau lita 3-8 za maji masafi katika kipindi sahihi
  • Mbuzi wanao kula malisho makavu huitaji zaidi maji
    Nguvu
  • Vyakula vya nishati kama vile mizizi, ndizi, molasi, matunda, na keki ya mafuta huhakikisha kwamba mbuzi wapo hai muda wote.
  • Soya, pamba, alizeti, karanga na nazi hutoa nguvu mara 2 – 3 zaidi ya vyakula vya wanga kama majani na matawi ya miti.

Protini

  • Mbuzi huhitaji protini zaidi kuliko ile waipatayo katika malisho
  • Majani ya kijani, njegere na maganda ya mgunga, soya, pamba, njugu, na majani kutoka Leucaena, Sesbania, na Gliciridia ni vyanzo vizuri vya protini.
  • Takataka za kuku ni chanzo kingine kizuri cha protini.

Madini

  • Mbuzi wanahitaji kalsiamu, sodiamu, fosforasi, chuma, shaba na iodini.
  • Kijani cha majani ya miti, vichaka, na mbegu ya nafaka ni vyanzo vizuri vya fosforasi na kalsiamu.
  • Majani yenye weusi ni vyanzo vizuri vya madini ya chuma.
  • Mbuzi wenye ukosefu wa madini ya iodini wanaweza kuzaa watoto dhaifu, walioharibika na njiti.

Vitamini

  • Mbuzi wenye upungufu wa vitamini A hukabiliwa na matatizo ya macho, maambukizo ya ngozi na matatizo ya kupumua na shida katika mimeng’enyo ya cchakula.
  • Mbuzi wenye upungufu wa vitamin huzaa watoto dhaifu.
  • Pale mbuzi wanapokuwa katika malisho, hupata vitamini mbalimbali kutoka katika mimea wanayo kula.
  • Viazi vitamu hutoa zaidi vitamini A na majani ya viazi hivyo vitamu hutoa vitamini C.

 

 

 

 

 

 

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

10 maoni juu ya “Taarifa muhimu kuhusu ufugaji wa mbuzi

        1. Habari,
          Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala zetu. Tafadhali usiache kuwasiliana nasi ikiwa una swali au maoni

    1. Habari,
      Karibu sana Mkulima Mbunifu na tunashukuru kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida letu.

      Kuhusu ufugaji wa kuku na mbuzi, tunakukaribisha kusoma taarifa mbalimbali kwenye tovuti yetu hii ya http://www.mkulimambunifu.org na ukiwa na swali au maoni usisite kuwasiliana na sisi.

      Karibu

  1. Naomba kufahamu mbuzi akizaliwa mtoto jike anachukua muda gani na yy kuja kuzaa au kupandwa

    1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali toka Mkulima Mbunifu. Mbuzi jike anaanza kupandwa akiwa na umri wa miezi nane

    1. Asante sana
      Ndiyo inawezekana, kikubwa ni kuamua, kutafuta eneo la ufugaji, kuwa na mtaji wa kutosha kununua mbuzi na kulisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *