- Mifugo

Namna ya kutengeneza chakula cha mifugo (silage)

Sambaza chapisho hili

Aina ya chakula hiki ni kizuri sana kwa ng’ombe wa maziwa, matokeo ya ongezeko la maziwa yataonekana kwa muda mfupi sana.

Pia chakula hiki huweza kupewa wanyama wengine kama kondoo,mbuzi,nguruwe n.k

Mahitaji:

  • Majani mabichi (nyasi au mazao ya nafaka)
  • Molases
  • Maji
  • Mfuko wa plastic (polythene bags), mapipa au shimo
  • Panga au mashine ya kukatia

Majani (chaff cuter).

HATUA ZA KUTENGENEZA SILAGE

Majani yakatwe na kuachwa kwa angalau siku moja ili kupunguza kiasi cha maji, ni vizuri kwa mazao ya nafaka kuvunwa wakati yametoa mazao tayari ili kuongeza ladha na virutubisho.

  • kata majani kutumia panga au mashine katika urefu wa inchi 1(2.5cm).
  • Tandaza chini karatasi la plastic au
  • Pima majani yaliyo katwa kiasi cha kilo 50-70 na uweke kwenye karatasi ulilotandaza.
  • Pima lita 1 ya molases na changanya na maji kiasi cha lita 1 hadi 3.
  • Nyunyiza mchanganyiko(molases na maji) katika majani uliyo yapima kiasi cha kilo 50-70, hakikisha sehemu zote zinapata molases kwa kuyageuzageuza.
  • Rudia hatua ya 1 hadi 5 hadi upate kiasi cha kukutosha.
  • Kama unatumia shimo, utachimba shimo la kuweka karatasi ya nayloni (polythene sheets) ili majani yasigusane na udongo. Pia unaweza kutumia mapipa ya plastic au mifuko ya nylon.
  • Chukua mchanganyiko wa majani na molases kisha hifadhi kwenye mapipa au mifuko ya plastic au kwenye shimo ulilo andaa, weka kwa kushindilia ili kuondoa hewa.
  • Ukisha weka kwenye chombo cha kuhifadhia kama pipa, mifuko ya plastic au shimo, funga kwa kukaza kuhakikisha hewa haingii ndani ili kuzuia kuoza.
  • Hakikisha shimo unafunika kwa karatasi ya nayloni na kuweka vitu vizito juu.
  • Hifadhi mbali na jua au mvua
  • Baada ya siku 30 hadi 40 chakula kitakuwa tayari kulisha mifugo yako.

ZINGATIA

Hakikisha maji na hewa haiingii ndani ya chakula chako wakati wa kuhifadhi.

Utakapo fungua toa kiasi cha kulisha kwa muda huo na kingine endelea kufungia na kuzuia hewa kuingia.

Wanyama wa maziwa wapewe angalau masaa 3 kabla ya

kukamua kuepusha harufu katika maziwa.

Silage nzuri itakuwa na kijani na

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *