Penye nia, pana njia. Usemi huu ni kweli na unatekelezeka. Hakika ni furaha ilioje kwa wapenzi wa jarida la kilimo hai ‘Mkulima Mbunifu’ kufikia miaka kumi (10) tangu lilipo anza kuchapishwa mwaka 2011.
Jarida hili limejizolea umaarufu katika maeneo mengi, hasa vijijini walipo walengwa, hasa vikundi vya wakulima wadogo wadogo ambao ndio wamekua walengwa wakwanza kunufaika na jarida hili. Lakini pia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi mbalimbali za kilimo, makanisa, mashule na vituo vya elimu vimekuwa mstari wa mbele kusambaza jarida hili kwa wakulima.
Hapo mwanzo, jarida lilisambazwa tu kwa njia ya posta ambayo bado imekuwa njia tegemezi kufikia wadau wengi vijijini. Sasa teknolojia imesaidia kupanua wigo wa usambazaji kwa njia ya mitandao ya simu, tovuti, whatsApp, pia njia ya uso kitabu (Facebook) nayo imekuwa maarufu zaidi hasa kwa vijana.
Baadhi ya wakulima wamekuwa maarufu kupitia jarida hili kwa kusoma na kufatilia, hata kubadilisha mfumo wa uzalishaji wa mazao na kupata faida zaidi sio tu kiuchumi bali hata kiafya ambapo ndio muhimu zaidi.
Kilimo hai ndiyo njia ya kufuata